Chuo cha al-Azhar chalaani waziri Mzayuni kuvamia msikiti mtakatifu wa al-Aqswa

Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar cha nchini Misri kimelaani vikali hatua ya waziri Mzayuni mwenye misimamo ya kufurutu ada kuvamia msikiti wa mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu.

Taarifa ya Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri imeeleza kuwa, hatua ya waziri huyo ni ya kichochezi na inaonyesha kuingiwa na woga na wahaka mkubwa utawala ghasibu wa Israel na hivi sasa unafanya njama za kutwisha matakwa yake na kutumia nguvu ya silaha kubadilisha utambulisho wa kihistoria wa mji wa Beitul-Muqaddas na msikiti wa al-Aqswa.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo inasema: Historia haitausamehe utawala huo, waungaji mkono wake na watu wanaonyamazia kimya jinai na hatua za Israel zilizo za kibinadamu wala kimaadili mkabala wa matukufu ya Kiislamu na haki za wananchi wa palestina ambao kimsingi ndio wakazi asiili wa ardhi hizo.

Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimeitaka jami ya kimataifa kuchuukua misimamo imara na madhubuti zaidi kwa ajili ya kuhitimisha jinaii mtawalia za utawala ghasibu wa Israel na katikak kuyahami matukufu ya kidini katika mji wa Quds na ardhi zote za Palestina zinazokkaliwa kwa mabavu.

Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel mwenye misimamo mikali jana akiwa pamoja na maafisa usalama, aliuvamia msikiti wa al-Aqswa na kuwa Waziri wa kwanza Benjamini Netanyahu kutia mguu wake katika eneo hilo takatifu baada ya kupita miaka mitano.

Hatua hiyo mbalimba na kulalamikiwa huko Palestina, kieneo na kimataifa imetajwa kuwa ni ukiukajii wa wazi wa sheria katika eneo hilom takatifu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *