Kuongezeka umaarufu wa Shahidi Haj Qassem Soleimani duniani, hasa barani Asia

Sambamba na kuadhimishwa mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes, habari na ripoti zilizochapishwa kuhusu kufanyika sherehe katika maeneo mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa uungwaji mkono na umaarufu wa jenerali huyo mashuhuri umeongezeka zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma, na hasa miongoni mwa vijana.

Katika uwanja huo, mipango na vikao maalumu vimefanyika katika miji tofauti ya Pakistan ambapo shakhsia wa kidini na kisiasa wa nchi hiyo wameshiriki katika vikao hivyo. Kundi la waungaji mkono wa mrengo wa mapambano nchini Uturuki waliokuwa wamevalia nguo zilizopambwa kwa picha za sura ya Shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia walionekana katika uwanja wa ndege wa Istanbul nchini Uturuki, wakiwa njiani kuja Iran kwa lengo la kushiriki katika kumbukumbu ya shahidi huyo.

Kamanda Soleimani aliuawa kigaidi katika shambulio lililofanywa na ndege za kivita za askari vamizi na wa kigaidi wa Marekani tarehe 3 Januari 2020  katika uwanja wa ndege wa Baghad katika hali ambayo shahidi huyo alikuwa amealikwa rasmi na viongozi wa Iraq kutembelea nchi hiyo kwa shughuli rasmi za kiserikali. Aliuawa shahidi akiwa na mwenzake Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq, Hashd al Sha’abi na wanamapambano wengine wanane.

Marekani ilidhani kwamba kwa kumuua shahidi kamanda huyo mkubwa wa Uislamu ingeweza kufunika nafasi yake muhimu katika eneo na kwamba kwa kumpachika shujaa huyo tuhuma bandia na zisizo na msingi, ingeweza kupunguza umaarufu wake katika nchi za Kiislamu. Kamanda huyo wa Uislamu alikuwa na mchango mkubwa na wa kipekee katika kuliangamiza kundi la kigaidi la Daesh lililoanzishwa na kudhaminiwa na Marekani kwa lengo la kuharibu jina la Uislamu.

Kundi hilo lilitekeleza unyama na ugaidi wa kitisha katika nchi za Asia Magharibi na hasa katika nchi za Iraq na Syria. Katika kusifu nafasi kubwa aliyokuwanayo Shahidi Soleimani katika uwnja huo, Allama Rajaa Nassir Abbas, Katibu Mkuu wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistana anasema: Sahidi Soleimani alikuwa akiichukulia Pakistan kuwa kiungo muhimu kilichokosekana katika kukamilisha muhimili wa mapambano. Alisifu mchango mkubwa alioutoa kamanda huyo mashuhuri wa Uislamu na kutumai kuwa juhudi zake zitaendelea kuhimiza na kuwashajiisha Waislamu waendeleze mapambano dhidi ya maadui wa Uislamu.

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani ambaye alitekeleza jinai ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, hakudhani kuwa mauaji hayo ya kigaidi yangemfanya shahidi huyo aenziwe na kupendwa kiwango hiki katika nchi za Kiislamu ambapo sasa anafuatwa na kuenziwa na mamilioni ya vijana na hivyo kuimarisha zaidi mti wa mapambano ya Kiislamu dhidi ya ubeberu wa kimataifa. Katika uwanja huo vijana wa Kashmir wameandaa vikao na maadhimisho makubwa ya kumuenzi Shahidi Qassem Soleimani ambapo wameapa kuendeleza njia na malengo yake. Katika upande wa pili, matabaka mbalimbali ya watu wa Afghanistan wameahudhuria kikao maalumu kilichofanyika katika kituo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Kabul na kutoa shukrani na heshima zao kwa mchango aliokuwanao shahidi huyo katika kudumisha njia ya Uislamu.

Maulana Muflih ambaye ni mwanzuoni mashuhuri wa Afghanistan anasema: Ni juhudi kubwa alizofanya Kamanda Soleimani ndizo zilitokomeza kundi la Daesh, na Trump alidhani kwamba kwa kumuua kamanda huyo angeweza kuharibu na kupotosha juhudi hizo mbele ya macho ya walimwengu na kudai kuwa ni Marekani ndiyo ililishinda kundi la kigaidi la Daesh. Pamoja na hayo jinai ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani iliwathibitishia kivitendo walimwengu kuwa ni Trump ndiye mkuu wa magaidi na kuwa Uislamu ndio utakaokuwa msindi wa mwisho.

Kwa vyo vyote vile, wataalamu waliowengi duniani wanasifu nafasi muhimu aliyokuwanayo Kamanda Qassem Soleimani na kuamini kuwa kuuawa kwake kunathibitisha wazi udhaifu na kushindwa Marekani na hasa Donalt Trump ambaye alikuwa akidhani kuwa angeweza kupora itibari ya kuangamizwa kundi la kigaidi la Daesh katika eneo kutoka kwa Shahidi Soleimani. Hii ni katika hali ambayo wajuzi wote wa mambo duniani wanasema kuwa huduma na mchango mkubwa alioutoa Shahidi Soleimani katika kupambana na ugaidi katika eneo ni wa kipekee na hauwezi kulinganishwa na wa mtu mwingine yeyote. Bila shaka kuangamizwa Daesh ambalo ni moja ya makundi ya kigaidii yanayodhaminiwa na Marekani ulimwenguni ni suala ambalo kwa yakini lilimkasirisha sana Trump na White House. Kwa msaada na ushirikiano wa nchi za eneo, Qassem Soleimani alifanikiwa kutokomeza na kulingamiza kundi la Daesh ambalo lilikuwa limetekeleza uporaji na ukatili wa kutisha katika eneo na hasa katika nchi za Iraq na Syria. Ni kutokana na sababu hii ndipo shujaa huyo wa Kiislamu akapendwa sana na mataifa ya eneo na hasa tabaka la vijana, jambo ambalo limeinua juu zaidi bendera ya mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa unaodhaminiwa na nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *