WHO: Tunatumai 2023 utakuwa mwisho wa janga la dunia nzima la Covid-19

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema, kuna matumaini kwamba janga la dunia nzima la ugonjwa wa Covid-19 litamalizika katika mwaka huu wa 2023.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni katika jedwali la dunia nzima la Corona, Marekani ndiyo inayoongoza kimaafa kwa kuwa na watu milioni 102,963,370 walioambukizwa virusi vya corona na 1,120,040 walioaga dunia kwa ugonjwa huo, ikifuatiwa na India yenye watu milioni 44,680,402 walioambukizwa.
Shirika la habari la Sputnik limemnakili Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom akieleza: “bila shaka, Covid-19 itabaki kuwa maudhui kuu itakayoendelea kujadiliwa, lakini ninaamini na ninatumai kuwa kwa juhudi mwafaka zitakazofanywa, mwaka huu utakuwa mwaka ambao hali ya dharura inayohusiana na afya ya umma itaisha rasmi.”

Adhanom amefafanua kwa kusema: “dunia hivi sasa iko katika ‘nafasi nzuri zaidi’ kuliko ilivyokuwa miaka michache iliyopita, kutokana na hatua zilizopigwa katika huduma za uchunguzi, utoaji chanjo na tiba ya ugonjwa huo”.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO ameongeza kuwa, pamoja na hayo, kungali kuna ufa mkubwa wa kukosekana usawa katika ‘upatikanaji wa vipimo, tiba na chanjo’; na kwa ujumla, Covid-19 kingali ni ‘kirusi hatari’ kwa afya ya binadamu, uchumi na jamii.
Janga la ulimwengu mzima la corona liliikumba dunia tangu mwanzoni mwa 2020. Ripoti za kwanza kuhusu mripuko wa ugonjwa huo zilitangazwa mjini Wuhan nchini China mnamo Desemba 2019.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *