Nchi 14 za Kiarabu zinapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa katika nchi 14 za Kiarabu yanaonesha kuwa, akthari ya watu wa nchi hizo wanapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Mwaka 2020, nchi nne za Kiarabu za Muungano wa Falme za Kiarabu Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco, bila kujali jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina, zilianzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo wa Kizayuni kwa mashinikizo na uunganishi wa Marekani. Hatua hiyo ilikabiliwa na wimbi la upinzani katika nchi za Kiarabu na Kiislamu.
Kuhusiana na suala hilo na kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la habari la Palestina  la Shahab, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni katika nchi 14 za Kiarabu yanaonyesha kuwa, asilimia 84 ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wanapinga serikali zao kuutambua utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel.

Orodha hiyo inajumuisha nchi za Mauritania, Morocoo, Tunisia, Libya, Misri, Sudan, Algeria, Palestina, Lebanon, Jordan, Iraq, Saudi Arabia, Kuwait na Qatar.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Kituo cha Kiarabu cha Tafiti na Uhakiki wa Kisiasa, ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali, ambao ulihusisha watu elfu 33, asilimia 36 ya waliotoa maoni yao wamesema, wanaamini utawala ghasibu wa kikoloni unaokalia kwa mabavu Palestina ndio sababu kuu ya upinzani wao dhidi ya utawala wa Kizayuni, huku asilimia tisa nyingine ya waliotoa maoni yao wakisema wanahisi Israel ina nia ya kupora na kukalia maeneo zaidi ya Waarabu.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *