Serikali ya Uganda imetangaza kuwa, imepeleka wanajeshi wake katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kuwa tayari kukabiliana na waasi wa M23.
Taarifa ya jeshi la Uganda UPF imeeleza kuwa, wanajeshi wake wamepelekwa katika wilaya ya Kanungu, ambako waasi wa M23 wameendelea kuingia katika mji wa Ishasha, baada ya kuondoka Kibumba.
Kwa mujibu wa Lutein Kanali Robert Nahamya kamanda wa Brigedia ya 307 ni kuwa, wanajeshi hao walitumwa siku ya Alhamisi iliyopita, lengo likiwa ni kutoa usalama kwa raia wake wanaoishi kwenye eneo hilo la mpakani.
Taarifa kutoka DRC zinasema waasi wa M23 wameendelea kuchukua vijiji muhimu na maeneo ya masoko karibu kilomIta 20 na mpaka wa mji wa Ishasha.
Kwa mujibu wa jeshi la DRC na ripoti za usalama za umoja wa Mataifa, waasi wa M23 wameendelea kutuma ujumbe unaokinzana na kauli zao za juma lililopita, kuwa wataondoka bila masharti katika miji waliyokuwa wanaishikilia.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, ripoti ya kiintelijensia iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa, waasi wa M23 wameendelea kujiimarisha katika maeneo mengine ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha kuondoka katika miji ambayo wamekuwa wakiishikilia na kuikabidhi kwa jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Serikali ya Kongo imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23. Hata hivyo Kigali inakanusha vikali madai hayo.
Pamoja na hayo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema, wana ushahidi unaoonesha kuwa askari wa DRC wapo mashariki mwa DRC, ka ajili ya kuwaunga mkono waasi wa M23, au kufanya operesheni za kijeshi dhidi ya makundi mengine ya waasi.