Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) ametangaza kuwa, nchi hiyo iko tayari kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya mazungumzo.
Dmitry Peskov msemaji wa Ikulu ya Russia ameeleza kuwa, Moscow ipo tayari siku zote kutatua matatizo mbalimbali kwa njia ya mazungumzo; ambapo Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin mara kadhaa amebainisha juu ya azma ya nchi yake kuwa tayari kufanya hivyo.
Msemaji wa Kremlin ameongeza kuwa, bila shaka chaguo bora zaidi ni kufanikisha malengo yetu kwa njia za amani, kisiasa na kidiplomasia. Peskov aidha amesisitiza kuwa, katika hali ambayo sheria za Ukraine zinamzuia rais wa nchi hiyo kutofanya mazungumzo yoyote na Russia; hakuna mazingira yoyote ya kuweza kufanyika mazungumzo huku nchi za Magharibi pia zikiizuia Kiev kufanya hivyo.
Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imetangaza kuwa inaitaka Russia iondoea wanajeshi wake katika maeneo yote ya Ukraine kama sharti lake muhimu zaidi ili ifanye mazungumzo na Moscow. Wakati huo huo Moscow inasisitiza kuwa inajikita zaidi kwa masharti yake na busara ya wazi ili kufanya mazungumzo na Ukraine.