Kijana mwingine wa Kipalestina auliwa shahidi na Wazayuni; jumla ya mashahidi 4 katika kipindi cha saa 24

Wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni wameuuwa shahidi kijana mwingine Mpalestina kwa kumpiga risasi katika kitongoji cha Qabatiya kusuini kwa mji wa Jenin jana Alhamisi.

Kijana huyo wa Kipalestina alijeruhiwa kwa risasi wakati wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliposhambulia kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan; ambapo habari kuhusu kifo cha Habi Mohammad Ikmail aliyekuwa na umri wa miaka 25 zilienea baada ya kijana mwingine wa Kipalestina kuuliwa shahidi kwa risasi katika hujuma nyingine ya uvamizi wa wanajeshi wa Kizayuni.

Wizara ya Afya Palestina imeripoti kuwa, Habib Mohammad Ikmail aliaga dunia kutokana na majeraha aliyopata kwa kupigwa risasi kichwani katika shambulio huko Qabatiya umbali wa kilomita sita kusini mwa mji wa Jenin. Ikbail alitangazwa kufariki dunia akiwa hospitalini huko Jenin.

Mapema jana raia mwingine Mpalestina kwa jina la Samir Ouni Harbi Aslan aliuliwa shahidi na wanajeshi wa Israel wakati akijaribu kuwazuia wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kumtia nguvuni mwanae wa kiume katika kambi ya wakimbizi ya Qalandiya kaskazini mwa mji wa Quds. Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza kuwa, Mpalestina huyo aliyekuwa na miaka 41 alipigwa risasi kifuani katika hujuma ya uvamizi ya wanajeshi wa Israel.

Kila uchao wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwa visingizio mbalimbali  huwashambulia wananchi madhulumu wa Palestina kwa kuwaua, kuwajeruhi au kuwatia nguvuni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *