Serikali ya Uingereza imepanga au kufanya mapinduzi katika nchi zaidi ya 27 duniani

Kituo kimoja cha utafiti nchini Uingereza kimefichua kuwa tangu vilipomalizika Vita vya Pili vya Dunia, serikali ya nchi hiyo imepanga au kufanya mapinduzi zaidi ya mara 40 katika nchi zaidi ya 27 duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, kituo cha utafiti cha Uingereza kiitwacho Declassified kimetangaza kuwa operesheni za kijasusi na kiintelijensia za nchi hiyo dhidi ya serikali za kigeni zimefanywa dhahiri au kwa siri, na nyingi zao zimeshindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kabla ya hapo, Declassified ilichapisha ripoti yenye ushahidi wa kuaminika ya uingiliaji wa jeshi wa Uingereza katika kila pembe ya dunia, ambayo inaonyesha kuwa London imetumia jeshi lake kufanya mapinduzi dhidi ya serikali za kigeni au kutishia kuingilia kijeshi, zaidi ya ilivyotangazwa na vyombo rasmi vya habari.
Kituo hicho cha utafiti cha Uingereza kimefichua pia kuwa, tangu mwaka 1945 hadi sasa, jeshi la Uingereza limeingilia kijeshi mara 83 katika nchi 47 duniani.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *