Mkuu wa Kamandi ya Ulinzi wa Kimtandao wa Ufaransa ametahadharisha kuhusu hatari ya ujasusi wa Marekani kwa bara Ulaya.
Jenerali Aymeric Bonnemaison Mkuu wa Kamandi ya Ulinzi wa Kimtandao ametahadharisha kuwa, ikiwa nchi za Ulaya zitaruhusu timu za ulinzi wa mtandao za Marekani kufuatilia mitandao yao, basi zitakuwa katika hatari ya kufanyiwa ujasusi na nchi hiyo.
Kabla ya indhari hii, Mkuu huyo wa Kamanda ya Ulinzi wa Kimtandao wa Ufaransa alisema katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari Alkhamisi iliyopita kuwa, kuongezeka harakati za timu za ulinzi wa kimtandao za Marekani kumeibua maswali katika kanali za Ulaya.
Jenerali Aymeric Bonnemaison Mkuu wa kamandi ya Ulinzi wa Kimtandao Disemba mwaka jana alizungumza katika mkutano wa faragha na Kamati ya Ulinzi ya Bunge la Ufaransa na kuzitaja oparesheni hizo za Marekani kuwa ni hujuma za uchokozi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Marekani ilikuwa na ushawishi mkubwa barani Ulaya katika fremu ya ushirikiano wa Trans- Atlanctic katika miongo ya karibuni. Hii ilitokana na nchi za ulaya kuhitajia misaada ya kifedha ya Marekani kwa ajili ya kuijenga upya Ulaya.
Aidha vitisho vya usalama viliondolewa pakubwa baada ya Vita Baridi kufautia kuanguka Umoja wa Kisovieti na mchakato wa kuziunganisha nchi za Ulaya ya Kati ha Mashariki katika taasisi za Ulaya kama vile Umoja wa Ulaya na Muungano wa Kijeshi za Nchi za Magharibi (Nato), lakini mahusiano ya kiusalama kati ya Brussels na Washington kwa mara nyingine tena yameimarika licha ya hatua za kichochezi za Nato khususan za kujitanua kwake kuelekea upande wa mashariki mwa Ulaya ambazo zimekabiliwa na radiamali kali ya Russia ikiwa nchi mrithi wa Urusi ya zamani.