Waziri wa Ulinzi Ujerumani ajiuzulu baada ya makosa kadhaa

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht amejiuzulu Jumatatu huku wizara aliyokuwa akisimamia ikiwa chini ya mashinikizo ya kuipatia Ukraine silaha hatari.

Kujiuzulu kwake kulikuwa hitimisho la mashaka yaliyoongezeka juu ya uwezo wake wa kufufua vikosi vya jeshi la Ujerumani huku vita vikiendelea kati ya Ukraine na Russia.

Lambrecht alikuwa amekosolewa kwa miezi kadhaa kutokana na jinsi Ujerumani ilivyozembea kukabiliana na vita vya Ukraine.

Vita hivyo viliashiria mabadiliko makubwa katika sera ya ulinzi ya Ujerumani huku Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akitangaza mfuko wa euro bilioni kuboresha jeshi la nchi hiyo ambalo ni maarufu kama Bundeswehr.

Baada ya miaka mingi ya uwekezaji duni, Scholz mnamo Septemba aliapa kubadilisha jeshi la nchi hiyo kuwa “lenye zana  bora zaidi” huko Uropa.

Lambrecht alisema katika taarifa yake Jumatatu kwamba, “Leo nilimwomba Kansela anifukuze kutoka ofisi ya waziri wa ulinzi wa shirikisho.”

Lambrecht, haswa, alikosolewa hivi karibuni na vyombo vya habari na wanasiasa wa upinzani kwa kutotaja ipasavyo mateso ya Waukraine katika ujumbe wake wa Mwaka Mpya.

Lambrecht aliongeza kuwa “vyombo vya habari vimekuwa vikinijadili kwa miezi kadhaa na haviruhusu kuripoti na kujadiliana kuhusu wanajeshi, Bundeswehr na maamuzi ya sera ya usalama kwa maslahi ya raia wa Ujerumani,”.

Wakosoaji wake walimshambulia, miongoni mwa mapungufu mengine, juu ya kile walichokiona kama kushindwa kwake kufahamu uzito wa vita vya Ukraine.

Scholz amekubali kujiuzulu kwa Lambrecht, msemaji wa baraza la mawaziri la Scholz alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *