Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni: Mwanajeshi aliyetekwa na Hamas mjini Gaza yuko hai

Benjamin Netanyahu amethibitisha ukweli wa video iliyopeperushwa kuhusu askari wa Kizayuni aliyekamatwa huko mjini Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alithibitisha hapo jana Jumanne kwamba mwanajeshi wa Kizayuni anayeshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza yu hai, jana Vikosi vya Al-Qassam vilipeperusha video yake.

Siku ya Jumatatu, wanajeshi wa al-Qassam, katika tawi la kijeshi la Hamas, lilitoa video ikimuonyesha Abraham Mangestu, ambaye amekuwa chini ya ulinzi wa Hamas tangu alipoingia Gaza mnamo mwaka 2014, akiomba msaada.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *