Kuongezeka juhudi za wapatanishi kwa ajili ya kusitisha vita Yemen

Juhudi za pande za kigeni kwa ajili ya kufanikisha usitishaji vita huko Yemen zimeongezeka sambamba na kuanza mwaka huu mpya wa Miladia.

Tarehe 21 mwezi Disemba mwaka jana Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen alidokeza kuhusu kuwasili nchini humo ujumbe wa Oman kwa lengo la kuwasilisha mapendekezo mapya kuhusu usitishaji vita nchini humo. Ujumbe wa Oman uliondoka katika mji mkuu wa Yemen baada ya mashauriano na viongozi wa ngazi ya juu wa Sana’a akiwemo Mahdi al Mashat Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa na kuwasilisha kwa viongozi wa Yemen misimamo ya muungano vamizi wa Saudia.

Ukiendelea na safari yake ya pili katika kipindi cha karibu miezi miwili iliyopita, ujumbe wa Oman wiki iliyopita ulifanya ziara huko Sana’a mji mkuu wa Yemen na kuanza mazungumzo kati yake na viongozi wa nchi hiyo. Ujumbe huo uliondoka Sana’a baada ya kukamilisha ziara yake ya siku nne na bila ya kutangaza matokeo ya kikao chake na Muhammad Abdulsalam Mkuu wa Timu ya Mazungumzo ya Yemen.

Muhammad Abdulsalam amethibitisha suala la Oman kuwa mpatanishi ili kufanikisha usitishaji vita huko Yemen na kueleza kuwa wamejadiliana na ujumbe wa Oman kuhusu mipango ya masuala ya kibinadamu; masuala ambayo yatapelekea kuboreka hali ya wananchi wa Yemen na kuandaa utangulizi wa kufikiwa amani, uadilifu na kuhitimishwa uvamizi na mzingiro dhidi ya Yemen. Hans Grundberg Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen pia baada ya kumalizika ziara ya ujumbe wa Oman mjini Sana’a Jumatatu iliyopita aliwasili Sana’a kwa ajili ya kuchunguza suala la kurefusha muda wa usitishaji vita huko Yemen.

Katika hali ambayo Grundberg anafuatilia suala la upatanishi katika mgogoro wa Yemen. tovuti ya utafiti ya Uingereza hivi karibuni ilifichua uhakika uliokwenda mbali zaidi kwamba, kwa mujibu wa nyaraka za tovuti hiyo, wakati Martin Griffiths alipokuwa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen alikuwa akiwasiliana na Shirika la Ujasusii la Uingereza la MI6.

Jitihada za kutekeleza usistishaji vita huko Yemen zinaendelea ambapo usitishaji vita nchini humo ulifikiwa tangu tarahe Pili Aprili mwaka jana kwa usimamizi wa Umoja wa Mataifa; ambapo usitsihaji vita huo ulikuwa umerefushwa muda wake miezi miwili nyuma na kuongezwa tena muda mara mbili. Mapatano hayo yalitazamiwa kurefushwa tena muda wake kwa mara ya tatu mwezi Oktoba mwaka jana lakini muda huo haukurefushwa kutokana na kushindwa kukidhiwa matakwa ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen kwa mujibu wa mapatano ya usistishaji vita ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa usitishaji huo, uwanja wa ndege wa Sana’a ulitakiwa kufunguliwa tena na vikwazo vya meli zinazoingia bandari ya Hodeidah viondolewe na mishahara ya wafanyakazi wa serikali ambao walikuwa hawajalipwa kwa miaka mingi kutokana na vita ilipaswa kulipwa, lakini Saudia, alitekeleza baadhi tu ya ahadi zake kuhusiana na suala hilo katika kipindi cha miezi 6 ambayo usitishaji vita ulikuwa unatekelewa. Kwa hakika, Saudi Arabia haikuheshimu usitishaji vita kikamilifu, na hilo liliifanya Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen iamini kwamba usitishaji vita huo haukusaidia lolote katika kupunguza mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo.

Sambamba na vita hivyo, Saudi Arabia pia inatumia mzingiro wa kidhulma iliyoiwekea nchi hiyo kama chombo cha kutoa mashinikizo dhidi ya serikali na watu wa Yemen. Wayemeni wanaamini kwamba usitishaji vita utakuwa na manufaa wakati, pamoja na kusimamisha vita, utaondoa mzingiro uliowekwa na wavamizi dhidi yao. Mwanadiplomasia mmoja wa Yemen alisema hapo awali: “Sanaa inasisitiza juu ya masharti yake kuhusu malipo ya mishahara ya wafanyakazi wote, kuondolewa vizuizi na marufuku ya usafiri wa anga pamoja na kuanza tena uzalishaji wa mafuta nchini humo.”

Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya vyanzo vilitangaza kuwa Saudi Arabia ilikuwa imeamua kulegeza msimamo na kukubali masharti ya Yemen kuhusu usitishaji vita. Mtazamo wa Wasaudi ni kwamba, kuendelea vita si tu sio kwa maslahi yao, bali kutawafanya waendelee kunasa kwenye kinamasi walichojitengenezea wenyewe huko Yemen na hivyo kugharamika zaidi kifedha na katika masuala mengine yasiyo ya kimaada.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *