Licha ya Mahakama Kuu ya utawala wa Kizayuni kubatilisha uamuzi wa Aryeh Deri kuwa Waziri wa Afya na wa Masuala ya Ndani wa utawala huo kutokana na rekodi yake mbaya ya uhalifu; vyombo vya habari vya utawala wa Israel vimetangaza kuwa Benjamin Netanyahu amemuuzulu waziri huo.
Baraza jipya la Mawaziri la Benjamin Netanyahu tayari limeanza rasmi shughuli zake. Aidha kuwepo mawaziri wenye misimamo ya kufurutu ada na ya kibaguzi kwenye baraza hilo kumepelelea shakhsia mbalimbali wa Israel kutahadharisha kuhusu baraza hilo jipya la mawaziri. Wamesema kuwa Israel chini ya uongozi wa Netanyahu inaelekea kusambaratika.
Aryeh Deri Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa chama cha Shas alitazamiwa kuhudhuria kikao cha leo cha serikali ambapo katika upande mwingine, baadhi ya duru za habari za utawala wa Kizayuni zimetangaza kuwa, Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu amemfuta kazi Aryeh Deri katika kikao cha leo cha baraza la mawaziri kufuatia uamuzi huo wa Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mahakama Kuu ya utawala wa Kizayuni tokea Jumatano iliyopita ilitaka kutekelezwa hukumu ya kumfuta kazi Deri hata hivyo Netanyahu alikiuka uamuzi huo na kutoutekeleza. Katika upande mwingine, Netanyahu anajaribu kumteuwa Aryeh Deri kama waziri kupitia kubadili sheria ya msingi ya utawala huo ambapo kwa mujibu wake, hakutakuwa na haja ya idhinisho la Mahakama Kuu pale Waziri Mkuu na Bunge (Knesset) watakapotaka kumteuwa waziri serikalini.