Bunduki 9,300 zimenaswa katika machafuko ya karibuni nchini Iran

Msemaji wa Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa silaha 9,300 zimekamatwa wakati wa machafuko yaliyozuka hapa nchini hivi karibuni.

Kuanzia mwishoni mwa Septemba 2022, baadhi ya maeneo ya Iran yalikumbwa na machafuko; na katika siku zake za kwanza kabisa ilidhihirika wazi kuwa baadhi ya vyombo vya habari vina mkono katika kushamirisha na kuenea machafuko hayo.
Katika ghasia na machafuko hayo, viongozi wa kisiasa wa Marekani, utawala wa Kizayuni, baadhi ya nchi za Ulaya, vyombo vyao vya habari na vyombo vya habari vya upinzani vya Kifarsi vinavyoungwa mkono na nchi za Magharibi vilitumia kauli mbiu ya kudai kuunga mkono haki za wananchi wa Iran na kufanya kila waliloweza kuwasaidia na kuwaunga mkono wafanya fujo na wavurugaji amani na usalama wa wananchi.
Akizungumzia mpango wa maadui wa kuua na kuvuruga usalama nchini, Kamanda Mehdi Hajian, msemaji wa Kamandi ya Polisi amesema: zaidi ya silaha 9,300 hususan za kivita ziligunduliwa katika kipindi cha miezi mitatu ya machafuko ambazo maadui walikusudia kuzisambaza nchini.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Kamanda Hajian ameashiria vita vya mchanganyiko na operesheni za kuvuruga amani na usalama zilizotekelezwa na adui na akasema: kumimina silaha nchini kulionyesha kuwa adui aliingia na nguvu na uwezo wake wote kwa lengo la kutoa pigo kwa usalama na anga ya utambuzi juu ya mambo wa watu hapa nchini.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *