Kuanza tena uchunguzi kuhusu mlipuko wa bandari ya Beirut

Duru za habari za Lebanon zimetangaza kuwa hakimu anayechunguza kesi ya mlipuko uliotokea mwaka 2020 katika bandari ya Beirut ameamua kuanzisha tena uchunguzi wa kesi hiyo.

Tareq Al-Bitar hakimu anayechunguza mlipuko katika  bandari ya Beirut ameamua uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo uanzishwe tena. Baadhi ya duru za habari zimearifu kuwa, al Bitar ameamua kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya watu 8 wapya akiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Serikali na Mkurugenzi wa Usalama wa Umma.

Wakati huo huo hakimu anayeshughulikia faili la kesi hiyo ameamua ameagiza kuachiliwa huru watu 5 kati ya waliokuwa wanashikiliwa kuhusiana na kesi hiyo.

Inafaa kuashiria kuwa, mlipuko mkubwa ulitokea tarehe 4 mwezi Agosti, 2020 katika bandari ya Beirut na kuuwa watu wasiopungua 200 na kujeruhi zaidi ya 6,500. Aidha watu laki tatu walipoteza makazi yao kufuatia madhara yaliyosababishwa kwa nyumba za raia.

Mlipuko huo ulikuwa mkubwa sana kwa kadiri kwamba nguvu ya uharibifu wake inakadiriwa kuwa sawa na kilo toni  1.2 za TNT. Mlipuko huo katika bandari ya Beirut huko Lebanon unatajwa kuwa moja ya milipuko mikubwa zaidi isiyo ya nyuklia kuwahi kutokea hadi sasa. Mlipuko huo uliisikika pia hata nchini Cyprus yapata umbali wa kilomita 240 kutoka mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Baada ya kupita karibu mwezi mmoja na nusu tangu ulipotokea mlipuko huo Jeshi la Lebanon pia lilitangaza kuwa, kwa mujibu wa chunguzi zilizokuwa zimefanyika wakati huo, majengo zaidi ya elfu 75 yaliharibika kufuatia mlipuko katika bandari ya Beirut. Benki ya Dunia pia ilikadiria kuwa, mlipuko katika bandari ya Beirut mwaka 2020 ulisabababisha hasara ya dola bilioni 4.6.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *