Yemen: Jinai za Israel huko Jenin ni ishara ya kushindwa mpango wa mapatano

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Yemen imetangaza kuwa, jinai za utawala haramu wa Israel katika mji wa Jenin ni ishara ya wazi ya kugonga mwamba juhudi na mipango ya utawala huo katili ya kupenya katika mataifa ya Kiislamu kupitia tawala zilizofanya usaliti.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Yemen  mbali na kulaani jinai za siku ya Alkhamisi za Israel huko Jeni imebainisha kuwa, jinai hizo ni ukiukaji wa wazi kabisa wa sheriia za kimataifa hususan Tangazo la Geneva.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, mauaji na jinai kama hizi haziwezi kudhoofisha azma ya irada ya taifa la Palestina na kwamba, bila shaka chaguo pekee la kukabiliana na Wazayuni maghasibu ni muqawama na mapambano.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, inaonekana kuwa, utawala haramu wa Israel umeshindwa kufikia malengo yake kupitia mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida ambao imefikia na baadhi ya mataifa ya Kiarabu yaliyoamua kulisaliti taifa la Palestina.

Alkhamisi ya juzi askari wa utawala wa Kizayuni huku wakisaidiwa moja kwa moja na maafisa wa usalama wa kikosi cha Shabak, walishambulia kambi ya Jenin, ambapo walikabiliana na wanamapambano wa Palestina waliosimama kutetea haki na usalama wa familia zao. Katika shambulio hilo, Wapalestina 10 waliuawa shahidi na wengine 16 wakajeruhiwa.

Licha ya kuwa vyanzo vya habari vya Kizayuni vimetaja sababu ya kutekelezwa hujuma hiyo na askari katili wa Israel kuwa ni katika juhudi za kukamatwa mwanachama mmoja mashuhuri wa Harakati ya Jihad Islami na vile vile kuzuia operesheni za muqawama wa Palestina, lakini jinai hiyo inahusiana moja kwa moja na misimamo ya kupindukia mipaka ya baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu linalotawala sasa katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *