Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kwamba oparesheni ya kujitolea kufa shahidi iliyofanywa na kijana wa Kipalestina katika eneo la Quds inayokaliwa kwa mabavu ni shambulio baya zaidi dhidi ya utwala huo katika miaka ya hivi karibuni.
Ijumaa iliyopita kijana wa Kipalestina aliyejulikana kwa jina la “Khairi Alqam, 21, aliwashambulia Wazayuni katika kitongoji cha Nabi Yaqoub Kaskazini mwa Al Quds na kuangamiza takriban 7 kati yao na kujeruhi wengine 10. Shambulio hilo lilitekelezwa baada ya ya jeshi la utawala haramu wa Israel kuvamia mji wa Jenin huku Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan siku ya Alkhamisi na kufanya jinai mpya, ambapo raia 11 wa Palestina waliuawa shahidi na wengine wasiopungua 20 kujeruhiwa.
Waziri Mkuu wa Israel. Benjamin Netanyahu, amesema katika majibu yake ya kwanza kwa operesheni ya kijana wa Kipalestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu kwamba: Jeshi, polisi na vikosi vya usalama vitafanya kazi kulingana na maagizo ya baraza la mawaziri.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amekiri kwamba operesheni ya kijana wa Palestina huko Quds imekuwa na mafanikio na kusema: Tumeshuhudia shambulio baya zaidi dhidi ya Israel katika miaka ya hivi karibuni. Netanyahu amesema operesheni za Wapalestina zinavitia wasiwasi vyombo vya usalama vya Israel.
Baada ya operesheni hiyo ya kishujaa ya Quds, baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vilimshambulia waziri wa usalama wa ndani wa utawala huo, “Itamar Ben-Gvir “, na kusema hatua zake za kichochezi ndio sababu ya kuongezeka mivutano katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na operesheni ya Ijumaa usiku huko Quds.