Hati 20 za ushirikiano zasainiwa na maafisa wa Iran na China katika safari ya Rais Raisi mjini Beijing

Hati 20 za ushirikiano zimetiwa saini kati ya maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China katika hafla iliyohudhuriwa na marais wa nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hafla ya utiaji saini hati 20 za ushirikiano na hati ya maelewano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China imefanyika kwa kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa nchi hizo mbili na mbele ya Seyed Ebrahim Raisi na Xi Jinping, marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China.
Hati ya maelewano ya ushirikiano katika uga wa ushughulikiaji wa majanga, utalii, mawasiliano na teknolojia ya habari, mazingira, biashara ya kimataifa, haki miliki za kitaalamu, kilimo, usafirishaji bidhaa, afya na tiba, vyombo vya habari, michezo na turathi za kiutamaduni ni miongoni mwa nyaraka zilizotiwa saini kati ya maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China.

Rais Xi Jinping wa China leo asubuhi alimlaki na kumkaribisha rasmi Rais Seyed Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambaye ameitembelea nchi hiyo akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kiuchumi na kisiasa.
Katika hafla hiyo, mizinga 21 ilipigwa kwa heshima ya rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ujumbe wa ngazi za juu alioandamana nao, na wakati rais huyo alipoingia ndani ya jengo la bunge, alilakiwa kwa gwaride maalumu la

heshima lililoongozwa na walinzi watatu bunge hilo..

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *