Hamas yaafiki kufukuzwa kwa wajumbe wa Kizayuni kutoka kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika

Msemaji wa Hamas, Jihad Taha amesema: Harakati ya Muqawama wa Kiislamu (Hamas) inaafiki kufukuzwa kwa Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya utawala wa Kizayuni na wajumbe wa ujumbe aliofuatana nao kutoka katika ukumbi wa mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Ameongeza kuwa: Tunashukuru kwa mafanikio na juhudi zote zilizofanywa kuzuia uwepo na ushiriki wa utawala wa Kizayuni katika mkutano huu wa kilele wa Afrika, juhudi zinazoendana na maadili na kanuni za Umoja wa Afrika.

Sami Abu Zahari, mjumbe wa uongozi wa harakati ya Hamas nje ya nchi pia alisisitiza kwamba kufukuzwa kwa ujumbe wa utawala ghasibu kwa mabavu kutoka makao makuu ya Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika huko Addis Ababa ni jibu sahihi kwa majaribio yake yasiyofanikiwa ya kupenyeza jumuiya kubwa ya kimataifa kama hiyo. kama Umoja wa Afrika, ambao unashikilia kuwa una historia ya kuunga mkono malengo ya Palestina.

Ikumbukwe kuwa shirika la habari la Palestina “Shahab” lilichapisha mkanda wa video wa kufukuzwa kwa ujumbe wa Israel katika ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ujumbe huo wa utawala wa Kizayuni uliingia kwa siri katika ukumbi wa mikutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika na kuongozwa na vikosi vya usalama kutoka nje ya ukumbi huo.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *