Maoni tofauti kuhusu makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia

Taasisi na nchi mbalimbali zilikua na maoni tofauti kuhusu makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia.

Qatar

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar amempongeza Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran kwa kufikiwa kwa mapatano hayo.

Siku ya Ijumaa, Mohammad bin Abdulrahman Al-Thani, katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Iran, alieleza kuridhishwa kwake na maendeleo mapya ya uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia na kumpongeza Amir Abdullahian kwa suala hili.

Katika ujumbe huu, Amir Abdullahian pia amempongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar.

Iraq

Vilevile Baraza la Mawaziri wa Iraq  lilizingatia makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia ya kuongeza mshikamano baina ya nchi hizo mbili za Kiislamu na kutangaza kuwa suala hilo litaathiri usalama na uthabiti wa eneo.

Vilevile, Seyyed Ammar Al-Hakim, ambaye ni kiongozi wa mtiririko wa hekima ya kitaifa wa Iraq ameashiria kua juhudi na nafasi ya kiujenzi ya Iraq katika kufikia maendeleo hayo katika uhusiano huo baina ya Iran na Saudi Arabia, na kubainisha kuwa, hii inaonesha kuwa Iraq ina itapata urahisi katika masuala mengi ambapo ni jambo ni jambo muhimu sana kwa Iraq hususan katika kusaidia kuziba uhusiano kati ya maslahi ya nchi katika kanda na kutambua maslahi yake katika suala hili.

Seyyed Ammar Hakim vile vile amesisitiza ulazima wa kutekelezwa sera ya mizani na wastani na akasema: Bila ya sera ya mizani na wastani, hakutakuwa na utulivu.

Misri

Katika kujibu mapatano hayo kati ya Iran na Saudi Arabia, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Misri ilitoa taarifa na kusema: “Tunatumai kuwa makubaliano hayo yatarejesha na yatasaidia kupunguza mvutano katika eneo.”

 

Lebanon

Nchini Lebanon, Mkuu wa Chama cha Maendeleo ya Kisoshalisti Walid Jumblatt katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii amesisitiza kuwa China inaunga mkono makubaliano hayo kati ya Saudi Arabia na Iran ambayo yanachukuliwa kuwa mafanikio makubwa katika kupunguza mivutano katika eneo la Mashariki mwa nchi za Kiarabu.

Marekani

Aidha Serikali ya Marekani ilijibu mnamo siku ya Ijumaa kuhusu taarifa ya pamoja ya pande tatu iliyotolewa kuhusu kuanzishwa tena kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Iran na Saudi Arabia.

John Kirby, mratibu wa mawasiliano katika Baraza la Usalama la Taifa la Marekani amesema: Wasaudi wametufahamisha kuhusu mawasiliano yao na Wairani, lakini hatukuwa na jukumu lolote katika makubaliano hayo. Lakini Washington inafahamu ripoti kuhusu kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tehran na Riyadh.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *