Idadi kubwa ya Wapalestina yatiwa nguvuni na jeshi la Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

Vikosi vya Kizayuni vinavyoikalia kwa mabavu vilianza oparesheni ya kuvamia, kusaka na kukamata Wapalestina  katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu kuanzia alfajiri ya leo (Jumatatu).

Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni waliwatia mbaroni ndugu wanne waliojulikana kwa majina Muhammad, Bara, Abdul Rahman na Momin Qarawi kutoka kambi ya “Noor Shams” katika eneo la mashariki la Tulkarm. Watu hawa wanne ni watoto wa Fathi Qarawi, naibu wa baraza la kutunga sheria la “Hamas”.

Vikosi vya uvamizi vilimkamata Abbas Zahir Sadouq mwenye umri wa miaka 16 kutoka kambi ya “Aideh” kaskazini mwa Bethlehem na mfungwa aliyeachiliwa hivi karibuni Mohammad Mahmoud Sukraneh mwenye umri wa miaka 23 kutoka makazi ya Nahalin magharibi mwa Bethlehem, baada ya kuvamia na kuwapekua.

Huko Nablus, wanajeshi waliovamia kitongoji cha Al-Makhfieh wakiwa na magari ya kivita na kumkamata tena mfungwa aliyeachiliwa hivi karibuni Saeed al-Sharidah.

Huko Hebroni, wavamizi hao walimkamata mfungwa aliyeachiliwa hivi karibuni aitwaye Moin al-Zohar na raia wengine kadhaa wa Palestina aitwaye Muhammad, Esaid na Imad al-Asafrah, Ahmed al-Harroub na Musa al-Qawasmi.

Vikosi vya Uvamizi vya Kizayuni viliwatia mbaroni vijana wawili walioitwa Abdul Moati al-Rimawi na Nihad Hamdan kutoka makazi ya Beit Sirha magharibi mwa Ramallah, pamoja na mvulana mdogo aitwaye Muhammad Abu Awad kutoka makazi ya Al Beira.

Mwezi uliopita wa Novemba, vikosi vinavyoikalia kimabavu vya Kizayuni viliwatia mbaroni Wapalestina 480 wakiwemo watoto 62 na wanawake 10 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Jerusalem na Ukanda wa Ghaza.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *