Mapema leo Jumatano wapiganaji wa Kipalestina wamekabiliana vikali na utawala wa Kizayuni katika eneo la Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Vyanzo vya habari kwa kuchapisha faili za video vimebainisha kuwa kufuatia shambulio la jeshi la Kizayuni dhidi ya makazi ya Qabatiya kusini mwa mji wa Jenin, sauti ya risasi na mapigano kati ya wapiganaji wa Palestina na vikosi vya utawala wa Kizayuni inaweza kusikika.
Wakati huo huo Vikosi vya Mashahidi wa Al-Aqsa vimetangaza kuwa, kumeshuhudiwa mapigano makali baina yao na vikosi vya utawala wa Kizayuni katika mji wa Qabatiya.
Jana jioni Jumanne, jeshi la Israel lilivamia nyumba za raia wa Palestina katika kambi ya Jenin na kupeleka washambuliaji kwenye paa za baadhi ya nyumba, na kuwakamata Wapalestina 3 kwa tuhuma za kupanga kutekeleza operesheni maalum.
Duru za Palestina zimeripoti kuwa, kufuatia mashambulizi ya wanajeshi wa Kizayuni katika kambi ya Jenin, wapiganaji wa Kipalestina walipambana na wanajeshi wa Kizayuni katika uwanda huo, ambapo Wapalestina 8 walijeruhiwa kwa risasi za Wazayuni.