Hali katika jela za utawala ghasibu wa Kizayuni katika kukabiliana na kuuawa shahidi Sheikh Khizr Adnan, mateka wa Kipalestina katika jela za utawala huo ghasibu, inaripotiwa kutokuwa shwari, na wafungwa wa Kipalestina waliitikia pakubwa habari za kuuawa shahidi Khizr. Adnan.
Ripota wa habari mjini Ramallah ameripoti kuwa jela za utawala huo ghasibu zilishuhudia mapigano makali kati ya maafisa wa jela zinazokaliwa kwa mabavu na wafungwa wa Kipalestina.
Vikosi vya utawala wa Kizayuni vimewajeruhi makumi ya wafungwa wa Kipalestina katika jela ya Ofer kwa kuwafyatulia gesi ya sumu na kutumia marungu kuwakabili wafungwa hao.
Ripota wa mtandao wa Al-Alam amesisitiza kuwa, njia zote za mawasiliano zimekatika katika jela ya Ofer na jela nyingine za utawala wa Israel nazo ziko macho baada ya kutangaza habari ya kuuawa shahidi Sheikh Khizr Adnan.
Sheikh Khizr Adnan aliuawa shahidi ndani ya jela baada ya siku 86 za mgomo wa kula.
Ripota wa Al-Alam alisema: Miji yote ya Ukingo wa Magharibi ilifunga maduka yake kujibu kifo cha kishahidi cha Sheikh Khizr Adnan kwa mgomo wa jumla, na taasisi nyingi rasmi na zisizo rasmi na vituo pia vilijiunga na mgomo huu.