Mashirika ya afya: Homa ya ini itaua zaidi kuliko ukimwi, malaria na kifua kikuu

Mashirika ya afya yametahadharisha kwamba, homa ya ini itakuwa tishio zaidi kwa maisha ya mwanadamu miaka michache ijayo ikilinganishwa na maradhi mengine.

Mashirika hayo yanasema, homa ya ini inaweza kuua watu wengi zaidi ifikapo mwaka wa 2040 kuliko ukiwmi, kifua kikuu, na malaria kwa pamoja ikiwa ugonjwa huo utaendelea kupuuzwa na kutofadhiliwa vya kutosha.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaripoti kila mwaka kwamba, homa ya ini, inaathiri zaidi ya watu milioni 350. Asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa na kufa kwa ugonjwa huo ni kutoka nchi zenye pato la chini na la kati.

Licha ya tiba ya homa ya ini aina ya C na chanjo dhidi ya homa ya ini aina ya B, watetezi wa ulimwengu usio na ugonjwa huu hatari na unaoodhofisha bado hawajafikia lengo lao.

“Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, tumeshuhudia mafanikio makubwa katika safari hii ya kutokomeza homa ya ini,” amesema Oriel Fernandez, mkurugenzi mkuu wa mpango wa homa ya ini duniani kwenye kituo cha Clinton Health Access Initiative au CHAI.

Kadhalika amesema, “gharama ya jumla ya kuponya mgonjwa ilishuka kwa asilimia 96 kutoka zaidi ya dola 2,500 kwa kila mtu hadi chini ya dola 80 kwa kila mtu aliyeponywa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *