Mahakama Tunisia yamhukumu kifungo jela kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Ghanushi

Mahakama ya Tunisia imemhukumu Rashid Ghanushi, kiongozi wa chama cha Kiislamu cha An-Nahdhah na mmoja wa wapinzani wakuu wa Rais Kais Saied, kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la uchochezi. Hayo ni kwa mujibu wa Monia Bouali, wakili wa kiongozi huyo wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini humo.

Ghanushi, mwenye umri wa miaka 81 ambaye alikuwa spika wa bunge la Tunisia kabla ya kuvunjwa na Rais Saied mnamo Julai 2021, alikamatwa mwishoni mwa mwezi wa Aprili akisubiri kusikilizwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake ya tuhuma za kupanga njama dhidi ya usalama wa serikali.

Mapema mwezi huu Ghannouchi alikataa kufika mbele ya mahakama, kupinga kile alichokitaja kuwa ni  kesi za ubambikizaji kwa sababu za kisiasa.

Spika huyo wa zamani wa bunge la Tunisia ni miongoni mwa zaidi ya wapinzani 20 wa kisiasa wa Kais Saied, wakiwemo mawaziri wa zamani na wafanyabiashara waliokamatwa tangu mwezi Februari mwaka huu.

Itakumbukwa kuwa, Rashid Ghanushi alirejea Tunisia kutoka uhamishoni Januari 2011 na kulakiwa kwa shangwe baada ya kiongozi dikteta wa muda mrefu rais Zine El Abidine Ben Ali kukimbia nchi kufuatia wiki kadhaa za maandamano.

Mnamo Oktoba 2011, chama cha An Nahdhah kiliibuka kama chama kikubwa zaidi katika uchaguzi wa kwanza wa bunge la Tunisia tangu kuondolewa kwa Ben Ali, na kupata asilimia 37 ya kura.

Ilikuwa ni mwaka 2019 Ghanushi alipogombea nafasi ya uongozi ndani ya serikali, na kuwa spika wa bunge la nchi hiyo…

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *