Idadi ya miili iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola yapindukia 200

Idadi ya miili ya watu iliyofukuliwa nchini Kenya ikihusishwa na mchungaji tata Paul Mackenzie anayeshukiwa kuwashawishi kufunga hadi kufa, katika kijiji cha Shakahola, katika Kaunti ya Kilifiki, imefika imepindukia 200.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wachunguzi nchini Kenya wamefukua miili mingine kadhaa na kufanya idadi ya waathirika wanaohusishwa na ibada ya kutokula wakiamini siku ya Kiyama imepindukia 200, ambapo wengi wao ni watoto.

Baadhi ya ripoti zinasema, kuna uwezekano wa idadi ya wahanga wa imani potofu za mchungaji wa kanisa la Good News International mhubiri tata wa Kikristo Paul Mackenzie kuongezeka kutokana na mamia ya watu kusadikiwa kutoweka na kutojulikana walipo.

Mackenzie bado hajatakiwa kujibu mashitaka, lakini mahakama iliamuru wiki iliyopiuta azuiliwe kwa wiki tatu nyingine wakisubiri uchunguzi zaidi kuhusu kile kinachoitwa “Mauaji ya Msitu wa Shakahola”.

Ingawa njaa inaonekana kuwa sababu kubwa ya vifo hivyo, baadhi ya waathirika  wakiwemo na watoto walinyongwa, kupigwa au kuzibwa hewa, kulingana na daktari mkuu wa serikali Johansen Oduor.

Tayari Rais William Ruto wa Kenya ameunda tume itakayochunguza mauaji hayo tata katika msitu wa Shakahola ambao uko katika shamba linalomilikiwa na kasisi aliyehusishwa na mauaji hayo. Tume hiyo itachunguza vifo vya watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa pote hilo la Kikristo lenye misimamo mikali ambalo kiongozi wake aliwaamuru wakae na njaa hadi kufa ili waweze kukutana na Yesu mbinguni, ingawa yeye mwenyewe aliendelea kula.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *