Idadi kubwa ya wananchi wa Bahrain walifanya maandamano kupinga kuhalalishwa uhusiano kati ya serikali ya nchi yao na utawala wa Kizayuni katika mji wa Al-Draz ulioko magharibi mwa Manama, mji mkuu wa Bahrain.
Tovuti ya habari ya Manama Post iliandika: Maandamano haya yalifanyika siku ya Ijumaa baada ya sala ya Ijumaa katika mji wa Al-Draz, ulioko magharibi mwa Manama, mji mkuu wa Bahrain.
Huku wakipinga kuhalalisha uhusiano na utawala unaoikalia kwa mabavu wa Israel, waandamanaji hao wamesisitiza kuendelea harakati za wananchi dhidi ya kuhalalisha uhusiano na utawala huo ghasibu hadi kufikia malengo yao halali sambamba na kusimamisha demokrasia na haki ya kujitawala.
Waandamanaji pia walipiga nara huku wakitangaza mshikamano na wanazuoni wa kidini, na kuzingatia sera ya serikali ya Bahrain ya kuwashikilia na kuwachukulia hatua kuwa ni jambo lisilokubalika kwa hotuba za kidini.
Kwa mujibu wa IRNA, wamelaani pia kukamatwa kwa Sheikh Mohammad Sanqour, mmoja wa maimamu wa Ijumaa wa Shia wa Bahrain, na kuzitaka mamlaka za Bahrain kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Manama Post, vikosi vya usalama vya Bahrain viliwekwa kwenye barabara kuu inayoelekea mji wa Al-Draz na karibu na njia kuu za kutokea mji huu kabla ya swala ya Ijumaa.