Hamas: Kuharibu nyumba za wafungwa ni kitendo cha kigaidi

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilitangaza kuwa, kitendo cha adui cha kuharibu nyumba ya Osama al-Tawil, ambaye mmoja wa wafungwa wa Kipalestina na mmoja wa watekelezaji wa operesheni ya Shafi Shimron; ni cha kigaidi.

Hazem Qassem, ambaye ni msemaji wa Hamas amesema kua Vitendo vya wavamizi hao vilizidisha hamasa zaidi ya wapiganaji wa taifa la Palestina na historia itaandika kwamba operesheni hii ilikuwa ni hatua ya kuwaangamiza kabisa maadui kutoka Shafi Shimron na vitongoji vya walowezi wa Nablus ili hatimaye walowezi hao waweze kuondolewa kutoka kwenye ardhi hiyo ya Palestine.

Alitoa salamu za upinzani uliosimama dhidi ya jeshi la Kizayuni lililoshambulia Nablus na kusifu ujasiri wao.

Wanajeshi wa utawala huo ghasibu walilipua na kuiangusha nyumba ya mfungwa Osama al-Tawil baada ya kuvamia mji wa Nablus siku ya Alhamisi asubuhi.

Mzozo mkali wa silaha kati ya upinzani na wavamizi huko Nablus

Kufuatia mashambulizi ya wanajeshi wa Kizayuni dhidi ya Nablus ili kuharibu nyumba ya mateka Osama Tawali, wapiganaji hao wa muqawama waliingia katika mzozo mkali kwa matumizi ya silaha.

Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina lilitangaza kuwa hadi kufikia sasa watu wawili wamejeruhiwa katika mapigano hayo ya Nablus.

Kulingana na IRNA, mmoja wa waliojeruhiwa alipigwa risasi kichwani na yuko katika hali mbaya sana.

Kikosi cha Quds cha Nablus pia kilitangaza kwamba wapiganaji wa muqawama waliwapiga risasi wavamizi hao kwenye barabara ya al-Marij katika mji wa Nablus na mapigano makali ya silaha yanaendelea katika eneo hili.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *