Mzozo nchini Sudan umewakosesha makazi zaidi ya watoto milioni moja katika kipindi cha miezi miwili, ambapo takriban robo yao wamekua katika jimbo la Darfur.
Kwa mujibu wa ripoti za habari, Khartoum na maeneo kadhaa nchini Sudan yameshuhudia mapigano makali kati ya jeshi linaloongozwa na Abdul Fattah al-Barhan, kamanda wa jeshi la Sudan, na majibu ya haraka ya vikosi vya kijeshi vinavyoongozwa na Muhammad Hamdan Daghlo, tangu katikati ya Aprili. Pia, juhudi zote na makubaliano ya kusitisha mapigano yameshindwa hadi sasa.
Mzozo huu umezua migogoro katika moja ya nchi maskini zaidi duniani, ambayo imeathiri nyanja zote za maisha ya watu wa nchi hii ya watu milioni 45.
Kama ilivyo katika vita vyovyote vile, watoto wanakua miongoni mwa makundi yaliyo hatarini zaidi, na katika muktadha huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) lilisisitiza kuwa watoto “zaidi ya milioni moja” waliacha makazi yao na ripoti za watoto zaidi ya mia tatu na thelathini waliuawa, Na zaidi ya watu 1,900 kujeruhiwa kutoka na hali ilivyo nchini Sudan.
Wananchi wa Sudan wanakabiliwa na uhaba wa chakula na huduma za kimsingi, hasa huduma za matibabu, kwakua robo tatu ya hospitali katika maeneo ya vita ziko nje ya utaratibu.
Shirika hili hivi majuzi lilielezea wasiwasi wake, hasa kuhusu Darfur, na kuashiria kukatiwa na kutowezekana kwa upatikanaji wa eneo lililoko magharibi mwa Sudan, ambayo inafanya kuwa vigumu kupata taarifa sahihi na muhimu.
Vikundi vya kimataifa vilitoa tahadhari kuhusu Darfur, ambako takriban robo ya wakazi wa Sudan wanaishi.
Umoja wa Mataifa ulionya wiki hii kwamba kinachoendelea Sudan, hasa katika mji wa El Geneina, mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi, kinaweza kuwa “uhalifu dhidi ya ubinadamu”.
Kulingana na takwimu za hivi punde za mashirika ya misaada, watu 2000 wameuawa katika mzozo wa silaha nchini Sudan hadi kufikia sasa. Hata hivyo, kulingana na mashirika ya misaada, idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.
Migogoro hii pia imewakosesha makazi zaidi ya watu milioni 2.2, na kwa mujibu wa takwimu za hivi punde za Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, zaidi ya 520,000 kati yao wametafuta hifadhi katika nchi jirani.
Nchi ya Chad, ambayo inapakana na Darfur, ni kimbilio la wakazi wengi wa eneo hilo ambao wanatafuta kutoroka mzozo huo. Kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, karibu Wasudan 150,000 wameingia Chad tangu vita kuanza.