Licha ya kuwepo uhusiano, Morocco yakataa misaada ya Israel kwa waathirika wa tetemeko la ardhi

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco imetoa jibu rasmi la kukataa tangazo la utayarifu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wa kutoa misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo.

Kufuatia tetemeko kubwa la ardhi la 7.20 katika kipimo cha Rishta lililotokea nchini Morocco usiku wa manane wa kuamkia Ijumaa, ambalo limeua watu elfu mbili na kumi na mbili na kujeruhi wengine elfu mbili na hamsini na tisa kulingana na takwimu zilizotolewa hadi sasa, kuna watu wengi ambao wangali wamekwama chini ya vifusi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco imetangaza kuwa hauhitajiki msaada wowote wa utawala wa Israel.

Uhusiano wa Morocco na utawala wa Kizayuni ulianzishwa tena tarehe 10 Disemba 2020, baada ya kusimamishwa kwa muda wa miaka 20. Sababu ya kuvunjwa uhusiano huo mwaka 2000 ilitajwa kuwa ni kuibuka kwa Intifadha ya Pili ya Wapalestina.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *