Katibu Mkuu wa harakati ya Asaib Ahlul Haq nchini Iraq ametilia shaka riwaya na ripoti rasmi iliyotolewa na vyombo vya dola kuhusu shambulizi lililolenga makazi ya Waziri Mkuu wa nchi hio, Mustafa al Kadhimi mjini Baghdadi siku chache zilizopita
Faraan: Qais al Khazali amesema kuna shaka katika riwaya rasmi inayosimilia jaribio la kuuliwa Waziri Mkuu, Mustafa al Kadhimi, na kwamba yeye anaamini kuwa kuna upande mwingine wa nje ya nchi uliohusika na jaribio hilo ukishirikina na Marekani.
Katibu Mkuu wa Asaib Ahul Haq amesema kuna ulazima wa kufanyika uchunguzi makini na wa kina wa kupata ushahidi katika jaribio hilo la mauaji na kusisitiza kuwa, kulenga nyumba ya Waziri Mkuu ni sawa na kulenga mfumo wa kisiasa na nchi ya Iraq.
Vilevile Khazali alipinga tuhuma kwamba makundi ya Iraq yamehusika katika jaribio hilo la mauaji na kusisitiza kuwa: “ndiyo maana tumetaka kufanyike uchunguzi wa kuaminika.”
Jumapili iliyopita vyombo vya usalama vya Iraq vilitangaza kuwa, jaribio la mauaji kwa kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya makazi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mjstafa al Kadhimi limefeli na kwamba, kiongozi huyo hajapata madhara yoyote katika shambulio hilo.