Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali magharibi mwa Sudan

Jimbo la Darfur Magharibi la magharibi mwa Sudan limekuwa likishuhudia mapigano makali, huku mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea kufanyika.

Hayo yameripotiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ambalo limeongeza katika taarifa yake kwamba takriban watu 700 wameripotiwa kuuawa, 100 walijeruhiwa na wengine 300 wamepotea katika Jimbo la Darfur Magharibi baada ya kuzuka mapigano kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mapigano hayo ni yale ya siku mbili za Novemba 4 na 5 yaliyotokea kwenye eneo la El Geneina huko magharibi mwa Sudan. Ripoti nyingine zimeonyesha idadi tofauti na hiyo ya wahanga wa mapigano hayo kati ya majenerali wa kijeshi huko Sudan.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *