RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Familia ya Marehemu Rais Mstaaf wa Zanzibar Idrissa Abdulwakili katika kuitikia dua ya kumuombea marehemu ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, iliyofanyika katika kaburi la marehemu Kijijini kwao Makunduchi, wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja na kuhudhuria dua maalum ya kuwaombea Viongozi Wakuu na kuiombea Nchi Amani, dua hiyo iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mtegani Makunduchi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria.Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mhe. Galos Nyimbo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe Galos Nyimbo, alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja kwa ajili ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja leo 16-12-2023.
WAZEE wa Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika Mkoa huo mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini na kuhudhuria Dua Maalum ya kuwaombea Viongozi na kuiombea Nchi Amani, iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mtegani Makunduchi leo 16-12-2023.