Kuongezeka kwa tofauti kati ya viongozi wa Tel Aviv/ Gantz ashiriki katika maandamano dhidi ya Netanyahu

Huku mashambulizi yasiyo na tija ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza yakiendelea na kushindwa kufikia malengo yaliyotangazwa hapo awali na utawala huo, ni dhahiri kwamba hitilafu baina ya viongozi wa Tel Aviv zinaendelea kushadidi.

Gazeti la Al Jazeera limeripoti kuwa, Benny Gantz, ambaye ni mjumbe wa baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni alichapisha picha yake inayoonyesha kwamba alishiriki katika maandamano ya familia za wafungwa wa Kizayuni yaliyofanyika mjini Tel Aviv.

Waandamanaji walioshiriki maandamano hayo, ambao idadi yao ilifikia maelfu kadhaa, walipiga nara dhidi ya Netanyahu na kutaka baraza lake la mawaziri liondolewe madarakani na kuandaliwa kwa uchaguzi wa mapema.

Wamesisitiza kuwa, baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni linapaswa kulipa kipaumbele suala la kurejea wafungwa wa Kizayuni na kuanza tena mazungumzo na harakati ya Hamas.

Kabla ya hapo vyombo vya habari vya Kiebrania viliripoti kushadidi hitilafu baina ya wajumbe wa baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni hususan Waziri Mkuu na Waziri wa Vita wa utawala huo.

Shirika la Redio na Televisheni la Israel lilitangaza kwamba Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa utawala huu, aliondoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri la Vita kwa sababu mkurugenzi wa ofisi yake hakuruhusiwa kuingia.

Kanali ya 13 ya utawala wa Kizayuni ilitangaza kuwa kabla ya kuondoka kwenye mkutano huo, Gallant alimtaka Netanyahu asisumbue kazi yake.

Katika upande mwingine, Kanali ya 12 ya utawala wa Kizayuni ikinukuu vyanzo vya kisiasa imetangaza kuwa, ofisi ya Netanyahu inaamini kuwa ofisi ya Gallant ilifichua yaliyomo katika vikao vyake vya faragha na Netanyahu.

Katika siku chache zilizopita, ripoti nyingi za hitilafu baina ya wajumbe wa baraza la mawaziri la vita la Netanyahu zimechapishwa katika vyombo vya habari vya Kizayuni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *