Madaraka na utajiri ndio mambo mawili ya msingi kwa jamii:Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Delivered at: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya 1: madaraka na utajiri ndio mambo mawili ya msingi kwa jamii
Hotuba ya 2: Gaza – uthibitisho wa kutelekezwa taqwa na waislamu wote ulimwengu mzima
Taqwa ni mfumo kamili wa maisha ndani ya mfumo wa uongofu kwa ajili ya kuishi kwa usalama . Taqwa haiwekwi kama somo tofauti bali inahusishwa na kila kipengele cha maisha. Mwanadamu anapokula chakula, anapojenga nyumba, anaposafiri, anapopumzika, anapofanya kazi kwa bidii na kitu kingine chochote anahitaji ulinzi na mfumo. Nguzo ya msingi ya mfumo huu wa usalama wa Taqwa ni Uadilifu.
Kipengele muhimu katika maisha ya mwanadamu ni maisha ya kijamii ambapo ndio asili ya mwanadamu. Uadilifu ni kipengele muhimu ambacho kimewekwa kwa ajili ya dini, jamii, ulimwengu, mfumo wa kiungu na uchamungu pia.
Katika Suratul Maidah Mwenyezi Mungu anasema uadilifu ndicho kitu ambacho kipo karibu zaidi na uchamungu na inasisitizwa sana kwamba hutakiwi kuacha kufanya uadilifu popote. Kama utaacha kufanya uadilifu dini na jamii vitaharibiwa. Allah anasema katika Suratul Hadid:
لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنْزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنْزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ {25}
Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.
Mitume walipewa mambo manne ambayo ni : KITABU, BAYYINAT, MIZAN ili waweze kusimamia jamii ya mwanadamu na sambamba na hayo tuliwapa mitume chuma kwa lengo hilo hilo. Kwa kuwa katika jamii zao walihitaji upanga ili kuweza kusimamia uadilifu. Muhimili wa maisha ya mwanadamu ni jamii na mambo mengine yote ni yenye kufuata. Ikiwa tutapata uadilifu kwenye jamii basi uadilifu utaenea maeneo yote. Tunafanya juhudi mbalimbali ili kuleta uadilifu ndani ya jamii katika vipengele vilivyo chaguliwa, kwa mfano tunatazama uadilifu tunapokuwa tunamtafuta imamu wa sala ya jamaa, Ijumaa, hakimu, Imam na kiongozi n.k.. mtu hutaka kusimamia uadilifu peke yake ndani ya jamii kama yetu ambayo uadili haupewi kipaumbele kama kipengele muhimu cha jamii. Katika jamii ya namna hii watu binafsi hujitahidi na kujaribu kusimamia uadilifu lakini juhudi zao huwa zinafeli. Kwa mfano barabara iliyoharibika na kukatika lakini sehemu ya wapita kwa miguu ikawa katika hali nzuri. Lakini hii haina maana kwa sababu magari makubwa hayawezi kupita katika barabara iliyokatika katika na kuharibika. Hata kama utatoa mrejesho ya kuwa barabara ya watembea kwa miguu ipo katika hali nzuri haitasaidia. Hivyo basi hata kama tutamtafuta imamu wa jamaa muadilifu imamu huyo hatakuwa na ufanisi. Ni kama kuleta vifaa vizuri vya kupamba nyumba hali ya kuwa kuta za nyumba ni mbovu na haifai hata kuishi katika sehemu kama hiyo. Hivyo kama utataka kuipamba nyumba basi inabidi kuitengeneza nyumba nzima. Shakhsiya hizi zote nzuri ambazo zinapatika mitaani ni sehemu ya jamii na sio msingi wa jamii. Kama unataka kuitathmini jamii yeyote anza na msingi wa uadilifu. Ikiwa utakuta kuna uadilifu basi hii itakuwa ni jamii ya kibinadamu na unaweza kukisia uwepo wa mambo mengine yote. Lakini ikiwa hautakuta uadilifu lakini ukaendelea kutafiti mambo mengine ya jamii, basi hayo mambo yote yatakuwa ni uongo. Ikiwa utasema jamii hii ina watu wachamungu lakini haina uadilifu, hivyo ni vipi inawezekana kuimarika uchamungu bila ya uadilifu?
Katika jamii kuna mambo mawili ambayo hubeba hadhi ya kimsingi, katika mambo yote mawili jamii iliyo na uadilifu au jamii isiyokuwa na uadilifu ambayo ni fisadi, iliyochupa mipaka ( faasidi, fasiki,faajir). Mambo hayo mawili ni madaraka na jambo la pili ni uchumi. Madaraka ndicho kipengele muhimu zaidi katika jamii. Ikiwa tutaona kivitendo kwamba jamii nzima ipo chini ya udhibiti wa serikali. Hiyo ipo katika hadithi ya kwamba watu hufuata dini za watawala wao. Dini ya kivitendo sio walioisoma au kuiona madrasa bali ni dini ya watawala wao. Ikiwa kiongozi ni muadilifu, basi dini ya watu itakuwa ni uadilifu, lakini ikiwa kiongozi ni fisadi basi watu watakuwa mafisadi pia. Dini ni sheria ambazo hufanyiwa kazi. Mnasoma somo la Uimamu lakini kivitendo mnafuata dini na sheria gani? Je ni Tauhid? Hapana ! mnaishi chini ya mfumo wa demokrasia. Kivitendo watu wanafuata maagizo na ilani za utawala ulimwenguni kote.
Jambo la pili ni utajiri ambao unachukua nafasi ya kimsingi katika jamii. Muundo, mfumo wa jamii ni nyenzo, rasilimali ambazo ni zinarudi kwenye utajiri. Ikiwa hakuna uadilifu ndani ya uongozi na mtaji basi haitawezekana kusimamisha uadilifu katika jamii kama hiyo na kukuza maadili kama inavyotaka Qur’an.
Jamii tunayoishi ndani yake na jana ilikuwa ni siku ya uchaguzi ambayo ndani yake watu waliandika hatima yao katika siku ya mab’ath. Mab’ath ni siku ambayo ufunuo wa mtume ulianza na unaendelea hadi siku ya Kiyama. Bi’tha ni kitendo endelevu ambacho huanza kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambapo Mwenyezi Mungu aliwaamsha na kuwatuma mitume na mitume wanatakiwa kuamsha umma katika hali endelevu. Ikiwa mtageuza utawala kuwa ni uwanja wa mashindano na sehemu ya kujaribu kwa kila mtu, ni kama kuwepo na watu mia moja wenye njaa sana ukawapa chakula na kuwataka wagawane. Katika ndoa zetu baadhi wana utaratibu wa kuweka chakula cha jioni kama buffe ambacho kila mtu hujihudumia. Wakati wa kupata chakula cha usiku unapofika, baadhi ya watu hukishambulia na wale ambao wana aibu hawaambulii chochote. Unaweza kujaribu na kuyaona haya yote. Umeweka utawala miongoni mwa watu wenye njaa na yeyote anaweza kutumia nguvu yake kunyakua. Pindi mapambano ya madaraka na mashindano yanapoanza huvuka mipaka ya kibinadamu. Katika mapambano haya unatakiwa kuwaondoa wapinzani wako ili kuweza kufikia madaraka. Je inawezekana kwa jamii kama hii kuwa ni jamii iliyo tengamaa. Pindi uwaniaji wa madaraka unapokuwa miongoni mwa watu, hubadilika na kuwa chanzo cha umwagaji damu. Leo hii hali ya nchi serikali imekuwa ndio nyenzo ya madaraka na nguvu na watu hutumia kila njia iwezekanayo ili kuyafikia madaraka hata kwa kuwaua wengine. Na katika uwanja wa pili ambao ni mtaji ikiwa utafungua mlango huu pia unaweza kuona yanayo tokea.
Jamii imebadilika na kuwa ni jamii ya matabaka kupitia haya mambo mawili na uadilifu hauonekani popote. Unawezaje kutaraji udini ndani ya jamii kama hii.
Wanyonge wanataka kuhama nchi na wahalifu wanafikiri ya kuwa jinai na uhalifu ndio njia pekee ya kupata maslahi yao. Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kusimamisha uadilifu hakuweka utawala kati na kuwataka watu wapate madaraka na wala Mwenyezi Mungu hakufanya hivi kwa ajili ya mtaji ili watu wapate mali jinsi wapendavyo. Mfumo aliouweka Mwenyezi Mungu kwa ajili hii ilikuwa ni uimamu. Pindi mitume wanapokuja na Bayyinat basi baada yake uadilifu utakuja. Kwa kila dini yeyote ambaye ataonekana kuwa na chembe ya tamaa ya madaraka, hadhi na uongozi yupo nje ya uadilifu. Wenye njaa ya madaraka, wanaotamani sio waadilifu maana yake hawafai kwa majukumu ya kijamii. Hawezi kuwa Imamu wa jamaa, shahidi, kiongozi, hakimu na wajibu wowote mwingine wa kijamii na majukumu ya kidini. Yeye ni mtu asiyestahiki.
Yeyote mwenye kujipendekeza mwenyewe ili kupata kura ni mwenye tamaa ya madaraka. Hii ni kwa sababu madaraka na utajiri ndio vitu anavyo tamani na ni fisadi zaidi kulingana na anavyo jieleza kuelekea vitu hivi. Katika demokrasia utawala wa imamu upo mikononi mwa watu. Na kwa mfumo wa uimamu utawala upo mikononi mwa Imamu.
Wali maana yake ni mtunzaji. Mamlaka kama baba ni wali wa mtoto. Mwenyezi Mungu ameweka wilayat kwa ajili ya yule ambaye hana mwelekeo na tamaa ya madaraka au mali, basi kwa nini awe Imam? Katika hili Imamu ‘Ali (a.s) anasema: kama Mwenyezi Mungu asingekuwa katimiza hoja kwa kuja kwa watu kwangu na kutoa kiapo cha utii, ningeyaacha madaraka haya nyuma ya mgongo. Mimi sio mwenye tamaa ya kuongoza. Ikiwa madaraka yatatoka kwa Allah basi yanakuwa ni majukumu na kwa madaraka haya inabidi nisimamishe uadilifu. Lakini katika jamii ambayo haya mambo mawili yanakuwa ni uwanja wa mashindano basi tija yake ni kutengeneza matabaka. Mnaweza kuliona hili baada ya uchaguzi kunazalika uadui kiasi gani, chuki ingawa wamechukua nafasi katika kila nyumba. Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu aliwatuma mitume ili kupitia kuwatii muweze kusimamia uadilifu./ hivyo basi imamu muadilifu huwapeleka wanadamu kumuelekea Mwenyezi Mungu na uadilifu ni miongoni mwa majukumu yake ya msingi ya imamu. Madaraka sio kwa ajili ya kuwagawa watu, kufanya sherehe na kuwatia mbaroni wengine ambao sio uimamu. Inatakiwa tujue ABC za uimamu. Ikiwa tutajadili uimamu kisha tukakimbilia kwa Taghuti ili kuweza kupata madaraka na utajiri kwa namna yeyote iwezekanavyo basi hii haitakuwa jamii ya kibinadamu na wala sio jamii ya kidini. Kama hakutakuwa na uadilifu maana yake itakuwa ni jamii ya ufisadi na wahalifu.
Mashindano ya uchaguzi yameharibu jamii vibaya zaidi ya magaidi walivyofanya. Imamu huja na kuunganisha makundi kama , Aus na Khazraj waliunganishwa na kuwa umma mmoja na imamu anasema nitakuongozeni. Sio kwamba imamu atakuja na kukuta kuna makundi mawili na yeye akaongeza makundi mengine mawili na kisha kuwaambia haya shindaneni. Huu sio uwanja wa dini na ndipo ushenzi utaanza. Banu Umayyah waliwachukulia Ahlul Bayt kama chama cha kisiasa na kutaka kuwaangamiza moja kwa moja ili kuimarisha madaraka na utawala wao. Hizi ndizo kanuni ambazo Mwenyezi Mungu aliziweka ili kusimamisha uadilifu.
Hotuba ya 2
Amri ambayo imetajwa sana ndani ya Qur’an ni kuwa na Taqwa. Ittaqu ni wajibu kwa mujibu wa wasomi. Hii ina maana kwamba taqwa ni wajibu na sio pendekezo. Hatuwezi kuona kitabu cha Taqwa ndani ya Fiqh. Ndani ya Fiqh tuna kitabu cha Salat, Sawm, Zakat, Hajj na kuna vitabu katika juzuu nyingi kuhusu maadili na tamaduni ambapo kuna Aya chache kuhusu hivyo vitu ndani ya Qur’an. Lakini kitabu cha Taqwa kipo wapi ambayo imetajwa sana ndani ya Qur’an? Tumeiweka Taqwa katika mada ya maadili. Panapokuwa na amri ya utii inakuwa ni maudhui ya Fiqh. Hakuna mpangilio katika hili. Ikiwa tutachambua tafsiri za Qur’an za kila dhehebu, hatutapata ndani yake sentensi mbili za taqwa. Mambo mengine huwa yanaelezwa kwa undani zaidi, lakini inapokuja katika suala la Taqwa hawaelezei. Ikiwa Fiqh na Tafsiri havijaelezea haina maana kwamba umuhimu wake umetoweka na haupo. Qur’an inatilia mkazo uchamungu zaidi. Huu ndio mpanglio wa Mwenyezi Mungu ambao hatujaupa umuhimu na kuutelekeza moja kwa moja japokuwa ndio ulikuwa mfumo wa Mwenyezi Mungu. Taqwa ina maana ya usalama na ulinzi na sio kujizuia. Kuna baadhi ya maeneo ambayo usalama na ulinzi vinahitaji kujizuia hivyo hapo kujizuia hakuwezi kumaanisha Taqwa.

Nchini Pakistani tuna shauku kubwa ya kidini. Kuna mvuto mkubwa wa dini na watu hawana mchezo katika maswala ya dini. Lakini ukiona namna watu wa itikadi kali walivyoiacha dini hata wasiokuwa na dini hawafanyi kwa kiwango hicho. Kama wewe ni mtu wa dini basi hutakiwi kulegeza katika Taqwa. Ulipiga kura je ulizingatia Taqwa? Ulienda chini ya miguu ya mafisadi na wahalifu wachupa mipaka. Ulitakiwa kuzingatia Taqwa katika uchaguzi. Katika demokrasia hata kama wagombea wote wana uchamungu ( Taqwa) je una haki ya kumchagua kiongozi? Kwanza eleza ni katika mambo gani una haki ya kumchagua kiongozi. Huna haki hata nyumbani kwako, mke wako hakupikii kila unachokipenda. Una haki ngapi katika biashara na kazi? Una haki ngapi kama muajiriwa? Je wanaweza kufanya mabadiliko huko? Lakini kwa kuwafanya kuwa viongozi ndio unazingatia kuwa ni haki yako. Ikiwa unataka kupiga kura bado unatakiwa kuzingatia.
Tunazingatia Taqwa popote na katika kila shughuli na uchumi. Kwanini unaikimbia Pakistan? Kiongozi wa mwaka 2018 alisema kwamba Wapakistan wote na hata watu wa Ulaya wote watakuja Pakistan kwa ajili ya kufanya kazi. Mlimpa kura, je haya yote yalitokea? Ebu tazama hali ya Wapakistan baada ya hapo. Kama hukuzingatia Taqwa basi subiri uone hali yako.
Taqwa iliachwa kimataifa na ubinadamu ulipaswa kuiona Gaza. Huu ni ushahidi wa kwamba Taqwa inapokuwa haipo hakuna kinachoweza kubaki salama na kuhifadhiwa. Uchamungu huhifadhi maadili ya kibinadamu, huruma na mambo yote yaliyopotezwa. Ni aibu kiasi gani kwamba mamia ya watu wanakufa kila siku . na hadi sasa wanalenga na kushambulia kambi za wakimbizi. Ulimwengu mzima unawasilisha mambo haya kwenye vyombo vya habari. Nani anaweza kusema hawa ni binadamu? Pindi inapokuwa hakuna Taqwa mtu hupoteza utu wake pia. Hili limethibitishwa kwamba hakuna ubinadamu. Ulimwengu wa Kiislamu leo ni kama msukule ambao haupo popote. Kuna unafiki, aibu na ushetani haya yote yapo ndani ya ulimwengu wa Kiislamu. Kibla chao kimezingirwa na sehemu ya mwili wao inauliwa kama hivi. Miaka michache iliyopita kulikuwa na kiangazi chenye jua kali sana Australia, hakukuwa na maji. Ndani ya Australia kulikuwa na wanyama hasa kama ngamia ambao walikuwa wakinywa maji. Waaustralia walianza kuwaua ngamia ili kuhifadhi maji. Ulimwengu mzima ulipiga kelele kukataza kuwaua wanyama kwa kisingizio cha maji. Na unaona kila siku namna gani wanyama wanazidi kulindwa. Tembo wa Islamabad ambaye aliumwa ni kiasi gani walimuhudumia na kumjali, kwenye vyombo vya habari tembo huyu alipewa kipaumbele sana. Wanaonyesha huruma sana kwa mbwa na paka lakini sio kwa binadamu? Wale ambao huzingatiwa kuwa ni ulimwengu wa Kiislamu , viongozi wao, wanasiasa wao, maulama wao na majeshi yao wanaweza kuona thamani yao sasa mbele ya Gaza. Na bado tunaendelea kuwaheshimu hawa wanaodai kuwa ulimwengu wa Kiislamu ambao Qur’an inasema ni wabaya zaidi kuliko wanyama? Yeyote anaye itazama Gaza haongei.
Wazayuni wapo jumla ya watu milioni 8 na nyinyi mpo watu milioni 200, lakini milioni 8 hawa wanakufanyieni dhihaka na nyinyi bado mnadai kuwa ni watiifu kwa Mtume na Ahlulbayt? Allah amesema nitakudhihirishieni hadhi yenu siku ya hukumu ( Kiyama). Imamu Husein ni kiongozi wenu hivyo popote ambapo dunia itawaendea sivyo basi mnatakiw3a kumfuata Imamu wenu. Maimamu wameshakuonesha kwa njia za wazi na safi kuhusu majukumu yako pindi dhulumu inapoingia. Leo hii Wapakistan dini yao ipo mikononi mwa wanasiasa wao na majenerali wao na kwa kuwa wao hawana mpango na Palestina basi na Wapakistan nao wamewafuata wao. Hakika sala ya Ijumaa mwenyezi Mungu ndiye anaifanya kuwa wajibu na sio serikali. Hivyo basi kama unamtii Mwenyezi Mungu basi kazi ya muhimu zaidi kwa waislamu wote, waumini, Shia na Sunni ni kuwaunga mkono na kuwasaidia hawa wanaodhulumiwa, nyanyua sauti na uwasilishe maumivu yao, waadhibu madhalimu na kuwazuia kufanya fujo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *