Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Delivered at: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 16 Februari, 2024
Hotuba ya 1: Mashia wa Imam Sajjad (a) na Shia wa tarehe 8 Februari 2024
Hotuba ya 2: Kutimiza agano na Mwenyezi Mungu, Mtume na Imam katika zama hizi ni kuunga mkono Palestina
Mwanadamu hana budi kuinuka duniani kwa ajili ya kusimamisha uadilifu. Mwenyezi Mungu anasema katika Suratul Hadid kwamba: Tumetuma Mitume pamoja na Kitabu, Mizan, Hikmah na kisha Chuma ili watu waweze kusimamisha uadilifu. maisha salama ya mwanadamu huanza baada ya kusimamisha uadilifu. Lakini mwanadamu hakujifungamanisha na utaratibu wa maisha aliyo muwekea Mwenyezi Mungu badala yake alitumia uhuru wa kuchagua aliopewa na Mwenyezi Mungu kufanya uvunjaji wa amri za Mwenyezi Mungu. Tunaweza kuona baba kama mzazi ambaye amepewa mamlaka juu ya watoto, na wazazi hutumia mamlaka haya kuwaweka watoto wao mbali na Mwenyezi Mungu. Mwanadamu pia amefanya hivi kwa pamoja. Wanataka mwanadamu asimamishe uadilifu na kisha Uimamu unakusudiwa kusimamisha uadilifu huu.
Tukitafakari juu ya historia ya Uimamu, mwanadamu amefanya kinyume na badala ya uadilifu walipendelea kuvuka mipaka, dhulma na Taghuti. Kwa mujibu wa Quran Taghuti ni yule ambaye ametoka nje ya mfumo uliowekwa na Mwenyezi Mungu. Watu waliwaacha Maimamu ambao walitakiwa kusimamisha uadilifu. Miongoni mwa Maimamu hawa mmoja wao ni Imam Sajjad (a) na leo ni siku ya kuzaliwa (Wiladat) ya Imam Sajjad (a). Mashia wana taarifa chache sana kuhusu Maimamu. Wakristo walihubiri dini yao na kuieneza kama misheni na sio taaluma, walipata mafanikio ambayo leo imekuwa ni dini kuu ulimwenguni . kwa Waislamu, Masunni wameeneza dini yao duniani kote lakini kwa Shia uenezaji na ulinganiaji wa Uimamu haujafanyika . Mashia wenyewe walisahau madhumuni ya Uimamu na chochote wanachuoni walichowasilisha ambacho kinajulikana kwa Shia tu. Tunaweza kusema kwamba zama nyingi ngumu za Uimamu zilikuwa zama za Imam Sajjad (a) na zilidumu kwa takriban miaka 35. Watawala kadha na mataghuti walipita na akatoa ahadi yake ya Uimamu. Imam Sajjad (a) alichukua Uimamu katika hali ngumu sana baada ya pambano la Karbala mnamo tarehe 10 Moharram . Katika hali hiyo hiyo ngumu, alianza kutoa mafunzo ya kiungu. Ugumu wa zama zaidi ya Ashura ulikuja baadaye aliporejea Madina baada ya kutoka kwenye kifungo cha umateka. Katika zama hizi, utawala ulikuwa kwa Yazid, aliwaua Ahlulbayt na kufanya dhulma kubwa ambayo Imam Sajjad (a) aliiona tangu mwanzo. Imamu Sajjad alianza zama za uimamu wake katika hali mbaya aliyo itengeneza Yazidi. Yaliyotokea kwa Imam (a) katika zama hizi tunaweza kuyachambua.
Tunaweza kuwagawanya watu katika makundi matatu; kundi la kwanza walikuwa Washami waliokuwa wafuasi wa Yazid. La pili lilikuwa ni kundi lililoungana na Abdullah Ibn Zubair, ambaye hakumkubali Imamu Sajjad (a). Walianzisha utawala wao wenyewe katika maeneo fulani kwa kuunyakua kutoka kwa Banu Umayyah. Kisha Abdullah ibn Zubair aliuawa na Marwan na utawala wake. Kundi la tatu lilikuwa ni watu wa kufah ambao hawakuwa wafuasi wa Syria na wala wa Abdullah Ibn Zubair. Walijiita Mashia. Wasyria, Yazidi, Watu wa Kufah wote walifichuliwa huko Karbala pia. Wafuasi wa Abdullah bin Zubair waliwekwa wazi kwamba hawakumkubali imam Sajjad kama Imam. Kundi la tatu ambalo lilimuandikia Imām Husayn barua nyingi, wote hawakuwa mashia bali miongoni mwa walio andika barua walikuwa ni makabila , wapiganaji wa kukodi na wanasiasa pia. Miongoni mwa hawa walimuandikia barua Imam Sajjad. Kulikuwa na baadhi ya mashia pia. Kulikuwa na matawi mawili makubwa ya Shia chini ya viongozi wawili. Kundi moja lilikuwa chini ya Sulayman ibn Surad Khuzai na kundi la pili lilikuwa chini ya Mukhtar ibn Thaqafi na kulikuwa na ushindani mkubwa baina ya wawili hawa. Ilikuwa ikiwa Sulayman atakuja katika uwanja wa vita fulani, basi Mukhtar alikuwa akiwataka wafuasi wake warudi nyuma na kwa njia nyingine. Ilitokea mara nyingi na hata mbele ya Muslim ibn Aqil. Baada ya kupita miaka mitatu ya tukio la Karbala, Mashia chini ya Sulayman walijuta kwa waliyoyafanya huko Karbala. Sulayman alimgomea Muslim akisema kwamba sisi hatukubali maamrisho ya mtu asiye maasumu na tutamsikiliza tu Imamu Husein (a) atakapokuja. Sasa walijuta na kuitwa tawwabina . kisha Sulayman alikusanya jeshi la watu 12000 wenye kutubia ambao walizingatia kuwa nafasi yao katika kilicho tokea Karbala ilikuwa ni uhalifu na wakaamua kwenda kulipiza kisasi. Mukhtar alilipinga hili na kuwatenganisha watu elfu sita hadi 8000kutoka kwenye jeshi la Sulayman, na kisha kubaki watu 4000tu ndio walioenda kupigana kama tawwabina. Mzozo mmoja uliotokea baina yao hapa ilikuwa kwamba Sulayman alitaka kupigana vita nje ya Kufah na iwe mpakani mwa Syria na Mukhtar akasema inabidi kupigana ndani ya Kufah. Hivyo hii waliifanya kuwa ni sababu ya Tawwabina kuondoka kuelekea Syria na walipambana na Banu Umayyah njiani na wakauliwa wote. Kisha Mukhtar alienda na kutoa bay’a ( kiapo cha utii) kwa Abdullah bin Zubair. Pamoja na hili kuna madai mengine yalianza ambapo kulianza harakati ya Umahdi wa Muhammad bn Hanafiyya. Imam Sajjad alikuwa Madina na Hanafiyya alikuwa Madina pia. Baadhi ya simulizi zinasema kwamba Hanafiyya alidai uimam na mjadala ulifanyika baina yake na Imam Sajjad(‘a). Alidai kwamba kama uimamu ulitoka kwa Imamu Hasan na kuja kwa Imam Hussain kwa sasahivi pia ni zamu ya kaka mwingine. Kisha Imam Sajjad alijadiliana naye na kumuomba kuacha madai yake hayo kwa ajili ya suala hili la Uimamu. Hii ilikuwa ni mada nyingine ambayo ilianza dhidi ya Imamu Sajjad.
Kundi moja lenye nguvu lilikuwa la Washami/ syria, kundi la pili lilikuwa chini ya Abdullah ibn Zubair na kundi la tatu lilikuwa ni la mashia ambalo lilikuwa chini ya Muhammad ibn Hanafiyya. Walitengeneza dhehebu la Qaisaniah na kudai kwamba Muhammad ibn Hanafiyya ni Mahd na alipokufa walidai kuwa kaenda Ghaiba.
Je ni mashia wangapi walibaki na Imam Sajjad(‘a) na kuendelea kubaki naye hadi mwisho. Kwa mujibu wa baadhi yahadithi zinasema kwamba watu 3,5,6 ndio watu waliobaki naye. Hawa ndio watu waliobakia wakiwa tayari kusikiliza na kutii amri za Imam. Hivi ndivyo Imam alivyoanza kipindi cha uimamu wake. Wafuasi wa Banu Umayyah walikuwa Syria na wafuasi wa Imam walikuwa Madina. Na mashia wengine waliobakia waparaganyika wengine wakaenda kwa Hanafiyya na wengine kwa Sulayman. Masunni walikuwa na Abdullah ibn Zubair. Mtoto wa Yazid bin Muawiyah ambaye aliwapendelea Ahlul Bayt aliuawa haraka na kisha baada yake akaja Umar ibn Abdul Aziz ambaye aliwaunga mkono na kwaaidia Ahlul Bayt aliuawa ndani ya miaka mitatu. Nguvu ya mashia iligawanya katika makundi mawili. Kundi moja lilikuwa chini ya Sulayman na wote waliuawa. Kundi la Mukhtar lilifanikiwa kwanza likiwa na Abdullah ibn Zubair , kisha wakaanzisha utawala ndani ya Kufa na kisha baada ya hapo wafuaswi wa Mukhtar waliuliwa na Abdullah ibn Zubair. Wafuasi wa Mukhtar hawakuuawa wote lakini sasa walienda wapi, kama vile Ibrahim ibn Malik Ashtar ambaye alikuwa ni ufunguo wa mafanikio ya Mukhtar alitengana nao na kwenda kutoa kiapo cha utiifu kwa Abdullah ibn Zubair. pindi Imam Sajjad alipoyaona haya tunaweza kuona hotuba yake aliyoitoa ndani ya Kufa. Bibi Zainabu na Ummu Kulthum, Faqtima bint Hussain na kisha Imam Sajjad (‘a).
Katika hotuba yake hii kwanza alijitambulisha kwa kusema mimi ni mtoto wa aliyeuawa mto Furat akiwa na kiu, ambao wamefanywa mateka wao na wake wao. Mimi ni mtoto wa wa aliyeuliwa akiwa na subira. Mimi ninajifaharisha kwa hili. Kisha akawaelekea watu wa Kufa na kuwaambia : hakika nyinyi mlitoa kiapo cha utii kwa Imam Hussain (‘a), lakini alipokujieni mlimuua. Ole wenu na hiki kitendo chenu. Vipi mtakutana na Mtume na kuinua macho yenu kumtazama usoni, kisha atakuulizeni kwamba mliua kizazi changu, mkakitia hofu kizazi changu na pindi Mtume(s.a.w.w) atakaposema nyinyi io katika umma wangu na wala hamna mafungamano na mimi. Msimuliaji anasema watu walianza kuomboleza na kuambizana kwamba tumeangamizwa, tumepoteza dunia na akhera yetu. Mwenyezi Mungu amrehemu anaye4 sikiliza mawaidha yangu na kuyakubali. Mtume mtukufu ni kigezo chetu chema . watu wa Kufa waote walisema sisi ni wenye kukusikiliza: Tupo tayari kutetea uimam wako na hatuna matarajio yeyote wala tamaa ya kupata chochote kutoka kwako kwa kuikubali uongozi wako na kukuunga mkono. Kamwe hatutakusaliti. Wewe tuamrishe tu ni kitu gani tunatakiwa kukifanya sasahivi. Sisi ni maadui wa wale ambao ni maadui zako. Vita yako ni vita yetu na amani yako ni amani yetu. Tutalipiza kisasi kwa Yazid na yeyote ambaye alifanya dhuluma kwa familia yako na tunatangaza kutoshirikiana nao.
Hawa walikuwa ni watu wa Kufa ambao Imam Sajjad aliwahutubia huku akiwa ni mateka. Baada ya kusikia hotuba hii walianza kutoa upya kiapo cha utii. Imamu Sajjad (‘a) aliwakatalia na kusema hapana nyinyi ni wasaliti na wavunja kiapo cha utii. Je mnataka kufanya kile mlichomfanyia baba yangu na babu yangu ‘Ali (a). Majeraha yangu yote hakuna ambalo limeshapona kwa maana sijasahau mlichokifanya. Jana mlimuua baba yangu kishahidi na Ahlul Bayt (‘a). Wito wa baba yangu bado upo masikioni mwangu pamoja na kelele za maumivu za wafuasi wake. Maumivu ya hawa wote bado yapo moyoni mwangu na koo langu limechoka kwa shinikizo. Sikilizeni mawaidha yangu nyinyi watu wa Kufa hamfanyi chochote kwa ajili yetu basi msifanye chochote dhidi yetu. Msiwe na sisi na lakini msiwe dhidi yetu pia.
Katika hotuba hii kundi lililo simama lilikuwa ni kundi linalo muamini Imam Sajjad(‘a). Kundi la tatu ambalo kulikuwa na watu Basra na baadhi yao wakiwa ni wa Yemen. Imamu Sajjad aliwaambia wafuasi ya kwamba msifanye lolote kwa ajili yetu na wala msiwe dhidi yetu. Ikiwa mtaungana nasi mtakuwa mmevunja viapo vyenu vya utii, na mkiwa dhidi yetu mtahesabika kuwa ni maadui zetu. Nyinyi sio wa kuaminiwa kwa chochote. Imam aliwataja kama walaghai, wavunja maagano ambao wanafanya vilevile kama walivyo mfanyia Imam Hussain (‘a). Hivi ndivyo kipindi cha uimam wa imamu Sajjad (a). Wako wapi sasa wafuasi wa Imam Sajjad leo? Hali ndiyo kama hiyo. Ni wangapi wamesimama na imamat. Uimamu ambao Mwenyezi Mungu ameuweka kama mfumo wa kusimamisha uadilifu, kuna dini ngapi hai. Tarehe 8 Februari mliandamanani wangapi wamebaki katika msimamo. Watu wa Kufa wanamuomba Imamu Sajjad awape amri baada ya siku nne tokea lilipo tokea tukio la Karbala, hivyo ni nini kilitokea siku nne kabla. Jana mlimtelekeza Imamu wenu na kumuacha peke yake na leo mnamdanganya imam. Siwezi kuwaamini kwa sababu pindi mtakapoona madaraka mtakwen da kwa Abdullah bin Zubair. popote pale mnapo paona kuwa ni penye nguvu ndipo mtakapo elekea. Ilibaki hivyo hadi kuisha kwa muda wa uhai wa Imam Sajjad walikuwa wakienda Madina kwa ajili ya ziara lakini hawaendi kwa Imam kukutana naye na wala yeye hakuwa tayari kukutana nao.
Leo ni siku ya kuzaliwa Imam Sajjad (a) je umeona kurasa za uimamu na ni kitu gani maimamu wanakutaka ufanye? Maimamu hawapendi tabia zetu tulizo nazo leo kwa sababu tunakwenda chini ya kila bango linalo inuliwa. Abdullah, Sulayman na Mukhtar yeyote anayeinua bendera yake tupo tayari kwenda chini yake lakini hatupo tayari kwenda chini ya bango la kipindi cha utawala wa imam. Kumuunga mkono imamu Mahdi maana yake ni kuunga mkono mfumo wa uimamu. Pindi Taghuti anapo kuiteni kwenye uchaguzi mwambieni tuna uimamu. Imam Sajjad alianza kipindi chake cha uimamu akiwa na wafuasi 6 kisha tazama ni wafuasi wangapi waliomfuata ipo katika historia. Acha tumalize cheni hii ya wasaliti wa uimamu na tuwe ni wenye kuunga mkono uimamu. Inatakiwa tuinuke kwa ajili ya uimamu. Kuna njia nyingi ambazo zinaweza kutumika kulifanya hili. Mnaweza kuna Maismailiya na Zaidiyya wanavyo simama na uimamu. Wale ambao wanaamini katika uimamu husimama imara, lakini hapa kati na kati kuna mashia wengi ambao wameacha uimamu na kwenda chini ya bendera ya kila Taghuti na tukio la tarehe Februari lipo mbele yenu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe taufiki tuufanyie kazi uimamu kama anavyotutaka Allah.
Hotuba ya 2
Ikiwa utaratibu wa ulinzi wa taqwa utaondolewa basi mwanadamu atabadilika na kuwa mbaya zaidi ya wanyama. Pindi linapotokea hili maadili yote ya mwanadamu huharibiwa. Kitu cha thamani cha kwanza kuharibiwa ni kiapo cha utii na kutekeleza majukumu. Na maadili mengine husimamiwa na hili. Ikiwa hakuna kujituma na kuwa na hima basi na maadili mengine hupotea. Masiku haya ya mazazi yanamaanisha kwamba inatakiwa turudie upya viapo vyetu vya utii kwa maimamu. Tunatumia matukio haya katika maadhimisho yetu kwa mambo yote mawili siku za kuzaliwa na siku za kufa kwao kishahidi. Maimamu wamefundisha namna ya kuwakumbuka lakini tunavyofanya sisi sivyo walivyo fundisha maimamu. Tunasherehekea na kuomboleza kupitia wataalamu. Haya ni masiku ya kutoa viapo vya utii ambapo tunatakiwa kujadidi kiapo cha utii na kisha tujitathmini kwamba je bado tupo katika kusimamia viapo vyetu au la. Wale ambao walikuwa na imamu Sajjad hawakutoa viapo vyao.
Katika hotuba ya kwanza nilitaja namna gani alivyowaita Imam Sajjad (‘a) kuwa ni wasaliti na wavunja ahadi ya utii na pia bibi Zainabu aliwaita watu wa Kufa kwa majina haya. Makr ina maana ya kuvunja kiapo cha utii na ana tabia ya usaliti. Wale ambao hufanya hivyo kwa uwazi ni wachupa mipaka. Kuna watu ambao hutengeneza sababu za kukimbia majukumu. Katika lugha ya Kiarabu Gadr maana yake ni mtu mwenye kuvunja kiapo cha utii. Yule anayetoa ahadi na kisha akawa hajatekeleza. Kinyume cha hili neno ni Wafa ambayo ina maana ya kutimia.
Agano la kwanza ni kumuabudu Allah, na kisha ni agano la kumtii Allah, kumtii Mtume na Maimamu. Leo wanachuoni we3nye tamaa wametengeneza hisia isiyo sahihi kwa kuleta demokrasia katika Uislamu. Wanasema viongozi halisi ni watu (raia) na wanaweza kumfanya yeyote kuwa kiongozi na atazingatiwa kuwwa ni kiongozi kwa mujibu wa sheria. Wilayah ni mamlaka na watu inabidi wamtii Allah, mitume na ulul Amr wanateuliwa na Allah na hawachaguliwi na watu. Kama sitekelezi ahadi, hivyo basi hatuwezi kutoa kiapo cha utii. Kila sku yetu inayopita bila sisi kuwa katika mfumo wa imamat inakuwa ni Gadr. Utiifu ni wafa.
Leo hii tunaweza kuona mpangilio wa Mwenyezi Mungu katika kila nyanja ya maisha. Katika hali ya ulimwengu wa Kiislamu leo kuisaidia Gaza ni utiifu na ni ukombozi wa agano. Amri ya Allah ni kuwaunga mkono wenye kudhulumiwa na kuwasaidia na kuwapinga madhalimu. Mtume anasema ikiwa Muislamu atamsikia Muislamu akiita wito wa kutaka msaada na akawa hajamsaidia basi sio Muislamu. Maimamu wanasema hivyo pia. Imamu Ali (a) anasema: usitazame dini ya wanaodhulumiwa bali itikia wito wa anaye dhulumiwa na kumsaidia. Hii ni dalili ya kiakili pia kwamba jukumu la mtu yeyote mwenye ufahamu anatakiwa kuwasaidia wanaodhulumiwa na yeyote atakaye acha kufanya hivyo hiyo ndio Gadr. Gadr ni kuvunja agano na Allah, Mtume na Maimamu. Yule ambaye anavunja agano ndiye kiumbe wa Allah aliyekuwa mbaya sana. Allah anaweza kuwasamehe wengine lakini sio wenye kuvunja maagano. Kuwa kwetu wafuasi wa maimamu, haifai kwetu kudai imamat kisha tukatenda vitendo vya wavunja maagano. Acha tupokee agano la uimamu na tunamuomba Allah awape ahuweni watu wa Gaza na Palestina kutokana na hii dhuluma.