Jeshi la Kizayuni limefichua kuwa, wanajeshi 30,000 wa Israel wamechunguzwa na kutibiwa matatizo ya kiakili yaliyosababishwa na kushiriki katika vita dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Ripoti ya jeshi la Israel kuhusiana na suala hilo inaashiria kuwa kati ya wanajeshi hao 1730 wamekabidhiwa kwa taasisi husika baada ya kukutana na afisa wa afya ya akili wa jeshi hilo ili kupata matibabu ya ziada.
Pia, jeshi linalokalia kwa mabavu lilitangaza kuanzishwa kwa kituo maalum cha afya ya akili kwa ajili ya kutibu matatizo ya kiakili ya wanajeshi walioshiriki katika vita vya Gaza.
Kwa mujibu wa ripoti ya jeshi la Kizayuni, simu ya msaada ya jeshi hilo pia imepokea simu 4450 kutoka kwa wanajeshi waliokumbwa na matatizo ya kiakili kutokana na ushiriki wao katika vita vya Ghaza.