Shirika la Misaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina limeonya kuwa, watoto wa Gaza wanakufa taratibu mbele ya macho ya walimwengu kutokana na njaa na utapiamlo.
Shirika la Misaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) lilionya tena Jumamosi kuhusu njaa na mzozo wa utapiamlo huko Gaza.
Katika kukabiliana na kifo cha Wapalestina kutokana na njaa na utapiamlo, UNRWA ilitangaza: “Watoto katika Ukanda wa Gaza wanakufa taratibu na mbele ya macho ya dunia.”
Shirika hilo la kimataifa liliongeza: “Hali ya Gaza ni mbaya sana na ni muhimu kwamba wafanyikazi wetu wawe na ufikiaji usiozuiliwa wa familia katika Ukanda wa Gaza ili kuokoa maisha.”
Katika hali ambayo Wapalestina waliopoteza maisha katika mashambulizi ya Wazayuni wameongezeka na kufikia mashahidi 30,410 na wengine 71,700 kujeruhiwa, habari zinaonyesha kuwa Israel hairuhusu vitu muhimu kuingia Gaza.
CNN leo imechapisha matokeo ya ripoti yake ya uchunguzi kuhusu hali ya Gaza, ambayo inasema kuwa Israel inazuia misaada ya kibinadamu kutumwa Gaza, ikiwa ni pamoja na dawa za ganzi, vifaa vya kuzaliwa na mifuko ya kulalia.
Ripoti hii ilichapishwa katika hali ambayo wanajeshi wa jeshi la Israel waliwauwa Wapalestina wasiopungua 122 waliokuwa wakisubiri kupokea unga kwa shambulio kwenye mtaa wa al-Rashid huko Gaza wiki iliyopita.