Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Delivered at: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya – 1 March, 2024
Hotuba ya 1: Amn, Adl, Khisb – ni mahitaji matatu muhimu ya jamii
Hotuba ya 2: kuishi kwa kila mtu kunategemea mfumo wa Imamat
Mwenyezi Mungu ameanzisha uadilifu kama msingi wa Taqwa (uchamungu). Kwa mtazamo wa Qur’an, muongozo wa Mtume( s.a.w) na mafundisho ya Ahlulbayt (‘a) ni kwamba uadilifu ni msingi wa ulimwengu, dini na uchamungu ( Taqwa). Mpangilio wa Mwenyezi Mungu kuhusu uadilifu ndani ya Suratul Hadid na katika Aya nyingine nyingi. Mwenyezi Mungu aliwatuma mitume na Bayyinat, vitabu, mizan na chuma ambavyo ni nguvu ambayo inabidi itumike kusimamisha uadilifu. Mambo mengine yote ni yenye kufuata uadilifu kama vile kuabudu, sheria za dini na matunda ya uadilifu ni maadili za fadhila zinazoheshimiwa. Uadilifu ndani ya Qur’an unamaanisha usawa ambapo kila kitu huwekwa mahala pake husika.
Kuna hadithi ya Imam Ja’far Sadiq katika Tahful ‘uquul, ambapo anasema ndani ya hadithi hiyo ya kwamba mambo matatu ni ya muhimu sana kwa sababu ni mahitaji muhimu ya mwanadamu. Kuna mahitaji mengine ya mwanadamu pia, kuna mahitaji ya msingi na kuna mahitaji ambayo ni yenye kufuata baada ya mahitaji ya msingi. Hata kama tunahitaji mambo yasiyokuwa ya kimsingi lakini pia tunahitaji kutimizwa mambo ya msingi. Ni kama ukitaka kutibu ugonjwa unahitaji kutimiza mahitaji ya kimsingi kama Dokta, Dawa na Hospitali.
Imam Sadiq (‘a) anasema kila mwanadamu anahitaji mambo matatu muhimu ambayo ubinadamu wake huyategemea ambayo ni Amn, Adl na Khisb.
Amn maana yake ni usalama ambayo ni hali ya kuwa kila kitu cha mwanadamu kinakuwa katika usalama , na mtu anakuwa ametosheka ya kwamba nyenzo zote ambazo kwazo mpangilio wa usalama hufanyika ni kupitia uaminifu ambao unamaanisha uhakika wa usalama
Adl inamaanisha usawa wa kijamii na usawa wa mtu binafsi ambao umeelezewa hapo awali.
Khisb asili yake inatokana na mti wa mtende ambao hutoa matunda mengi kwa muda mrefu bila ya kuzeeka. Hii inamaanisha ustawi. Kwa mujibu wa hadithi maisha ni mafanikio na wala sio kudorora . kuna watu ambao wana nyenzo za maisha kama yalivyo maisha yao na wengine ni wale ambao hawana nyenzo za maisha kulinagana na mahitaji yao. kwa mfano kama mtu hana nyumba , anapata chakula kidogo na mahitaji mengine muhimu ya maisha inamaanisha Uchumi wake umedorora. Ikiwa mahitaji muhimu ya maisha yametimizwa basi mtu huwa tayari zaidi kwa ajili ya kuyafikia Malengo ya maisha.
Tunaishi katika jamii isiyokuwa na usawa ambapo nyenzo ndio zimekuwa Malengo na Malengo yamekuwa ni nyenzo. Mfummo wa maisha ya mwanadamu yamejikita katika Malengo ambayo yanatakiwa siku zote ndio utme ambao upo mbele yake. Nyenzo zote katika maisha hutolewa ili kuweza kufanikisha lengo. Kuna jambo moja ambalo linafungamana na maisha kabla ya maisha haya na jengine ni baada ya maisha. Ebu chukulia mfano kwamba maisha ni kama gari ambao inabidi ifike kwenye baadhi ua malengo ambayo inawezekana kuwa ni baadhi ya miji Fulani. Mwelekeo wa gari uanelekea mji huo na litafika huko. Lakini ili gari iweze kutembea inahitaji nyenzo kadhaa ikiwemo dereva, petroli na nyenzo nyingine muhimu. Haya ni mambo muhimu yanayo hitajika ili gari itembee lakini lengo la gari sio petroli bali ni mji ambao upo mbele. Nyenzo zitaendesha gari na gari itamfanya mtu aweze kufika kwenye lengo lake. Hivi ndivyo maisha yalivyo, kuna baadhi ya vitu ni nyenzo na kuna lengo. Mwenyezi Mungu hakuumba gari za mashindano ambazo ni kwa ajili ya kujionesha. Na Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanadamu kwa ajili ya kufurahi na kucheza. Kila mwanadamu ameumbwa na Malengo ya kuumbwa na ili afikie Malengo ya kuumbwa Mwenyezi Mungu amempa maisha. Katika maisha haya kuna usalama, nyenzo na Malengo ambayo kupitia kwayo atatembea na kufikia lengo. Leo hii nyenzo za maisha ndio zimegeuka kuwa lengo kutokana na kukosekana kwa usawa katika jamii. Upatikanaji wa nyenzo hizi ndio umekuwa lengo lenyewe. Mwelekeo wa maisha umebadilika. Nyenzo inabidi ziwe nyuma lakini zimekuja mbele na lengo limekuwa nyuma. Kama ilivyokuwa lengo la gari petroli kisha kufanya mashindano ya mbio za magari kisha baada ya kujaza petroli kwa ajili ya maisha kutumia katika maisha yako yote ambayo itakuwa ni upuuzi na kupoteza. Qur’an tukufu inasema kwamba maisha ya dunia ni lahwu na la’ib ( pumbao na mchezo)ambayo tumeielezea mara nyingi hapo Kabla. Lahw maana yake ni yale mambo ambayo yakuweka mbali na lengo la maisha. Inawekana ikawa ni elimu, biashara na familia mambo yote haya yanaweza kumuweka mtu mbali na lengo la kuumbwa. Qur’an inasema kwamba Watoto wako na mali zako havitakiwi kukiutawala na kukutoa katika lengo. Katika Suratul Munafiqun Aya ya 9 inaelezea kinacho kusudiwa kuhusu maisha ya lahw.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ ۚ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ {9}
Enyi mlio amini! yasikusahaulisheni mali zenu wala watoto wenu na kumkumbuka Mwenyezi Mungu. na wanao fanya hayo basi hao ndio wenye khasara.
Ilha ( Tulhikum) ina maana ya mambo ambayo humshughulisha mtu kiasi kwamba anafikia hatua ya kusahau lengo. Kriketi sio lahhw kubwa zaidi bali ni utajiri na asasi unazo miliki, na lahw ya pili ni Watoto wako. Leo Ijumaa ni kitu kinatushughulisha? Ijumaa ni siku tukufu mna ambao Mwenyezi Mungu ametupa na imetajwa na Ahlulbayt (a) lakini katika siku hii ya Ijumaa tumeshughulishwa sana na hatuna muda wa kutekeleza mambo ya wajibu katika siku hii. Ni kitu gani kinatuweka mbali na kumtaja Allah? Ni mali na watoto. Hatuna muda kwa sababu ima tupo ofisini, biashara au Watoto. Hizi ndio lahw mbili ambazo humuweka mtu mbali na lengo. Sio kwamba lahw ni kucheza kamari tu, kushiriki michezo na kufurahi ambapo kuna muda wake maalumu. Lakini Watoto na mali ni lahw endelevu ambayo muda wote ipo nasi. Inatakiwa tuyatathmini maisha yetu na tuone ni kitu gani kimetushughulisha zaidi katika akili zetu: je ni Watoto, utajiri au vyote kwa Pamoja. Maisha yote yanatumika baina ya kuwa nyumbani na dukani. Maisha yote yanatumika lakini hukupigwi hata hatua moja kuelekea lengo. Allah amejaza ardhi nyenzo za maisha na mwanadamu amepewa akili ya kuweza kuzipata nyenzo ili aweze kutumia maisha kwa lengo lake. Ikiwa nyenzo hakuna basi maisha ya mwanadamu yatakuwa mbali na lengo . imekuja katika hadithi kwamba ufakiri umekaribia kumfikisha mtu katika ukafiri. Kuna baadhi ya wengine ambao wana muelekeo wa mali. Imam Ali (‘a) anaomba dua kwa Mwenyezi Mungu kwamba : Ewe Mwenyezi Mungu usinifanye kama wale ambao kutokana wingi wa riziki na fadhila wanakuwa ni wenye4 kupenda ufahari na usinifanye kama wale ambao kutokana na uchache wa umiliki na fadhila wanakuwa ni wenye kulaaniwa. Khisb inamaanisha ustawi na kuwa na maisha bora ambapo mtu anakuwa hana wasiwasi wa mahitaji muhimu ya maisha ambayo ni chakula, mavazi, nyumba, bili, dawa n.k.
Tumegawanyika katika haya mambo mawili na kwa yote hayo hatuna muda . wale ambao hawana mali wanalia na kusema kwamba lau kama tungepata njia ya kujipatia nyenzo za maisha au kupambana kwa ajili ya lengo. Kuna mambo matatu ambayo anayahitaji kila mtu. Amn, Adl na Khisb. Haya ndio mambo ya msingi ya jamii ambayo Imam Sadiq ameyaeleza. Ni muongozo 3wa kijamii kwa namna ambavyo jamii ya kibinadamu inahitaji misingi hii mitatu. Mambo haya matatu sio Malengo. Kudumisha mambo haya huandaa njia ya kuelekea lengo. Katika jamii isiyokuwa na usawa huwezi kutengeneza maisha ya faraja na utulivu. Hii ni kwa sababu uadilifu unapo kosekana hupelekea ugavi wa nyenzo kutokuwa wa haki. Baadhi wanakuwa ni matajiri wa kupindukia lakini wanabaki kuwa hawana chochote. Jamii yetu ni mseto ambapo tuna dini, maovu, tamaduni za Uhindu, matamanio, mila za mababu na kuna mchanganyiko wa mambo mengi. Katika jamii isiyokuwa na usawa hakuna kitu kinachokuwa kwenye nafasi yake na mahala pake. Hivyo ikiwa utaona kwamba lengo la elimu ni kupata kazi, basi kuitafuta ni nyenzo ya maisha. Kwa kuwa mgogoro halisi ni wa nyenzo na hili limetokea kwa sababu ya kukosekana uadilifu. Kwa sababu hii kuna mkusanyiko wa nyenzo kwenye sehemu moja na vipengele vingine vimetengwa. Ni ukweli kusema kwamba kuna asilimia ndogo ya watu wenye nyenzo za maisha, ambazo ni utajiri, anasa, asasi na mali kwa ajili ya vizazi vingi. Rasilimali ambazo zipo Pakistan zinatosha kwa nchi ikiwa zitagawanywa kwa uadilifu. Baada ya kuwa Pakistan imetengenezwa utajiri na mali zilirithiwa kutoka kwa Fued na kuna kikundi cha mabepari ambao walichuma mitaji yao kutokana na kufanya kazi kwa bidii. Katika kipindi hiki cha sasa utajiri haupo mikononi mwa mabepari na mabwana wa Fuedal ( mamwinyi). Mabepari walikuwa wakifikiri kwamba wao ndio wanaomiliki kila kitu na kuendesha nchi. Leo hii mali zote za nchi zinaendeshwa moja kwa moja au kwa njia isiyokuwa mubashara na baadhi ya watu . na watu waliokuwa wengi wanabaki wakiwa ni wenye kunyimwa nyenzo na mahitaji muhimu ya maisha. Leo hii watu wengi hawapati hata milo miwili kamili ya kila siku. Hawawezi kununua pea mbili za nguo kwa mwaka. Watu wengi hawana nyumba zao zenye utulivu na starehe. Khisb haiwezi kuwepo ikiwa hakuna uadilifu.
Amn pia hakuna Pakistani sio kwa tajiri wala masikini. Na hivyo ni kwa sababu hakuna uadilifu ambapo nguvu haitawanywi kwa uadilifu na haki. Hii imepelekea kukosekana kwa uswa katika jamii nzima kwa kuwa uadilifu ndio msingi wa kila kitu. Lakini bado Amn, Adl na Khisb sio lengo ba li ni nyenzo kwa ajili ya kufikia lengo la maisha. Nimetaja mara nyingi sana lengo la maisha na hii ni kwa sababu hili halipo katika mtaala wetu ambapo lengo la maisha hufundishwa. Mitaala inayofundishwa madrasa haina kazi katika uhalisia wa maisha yetu. Tunafundishwa mtaala wa kidini ambao hautufundishi chochote katika maisha yetu ya kiuhalisia na kivitendo. Mwanafunzi anayesomea madawa anajifunza vitu ambavyo kwavyo hutatua matatizo ya mamilioni elimu yao hunufaisha jamii japokuwa ni kwa malengo ya kibiashara. Lakini wasdomi wa dini wanaosoma elimu yao haiwasaidii katika uhalisia wa maisha yao na wala haisaidii jamii. Imam Sadiq (‘a) anasema kuna mambo matatu ambayo ni mahitaji ya kimsingi na mambo haya nabidi yaelezwe kwa undani ndani ya mtaala wetu. Hii ni misingi ya jamii. Tunakwenda kuuliza IMF ni namna gani jamii inatakiwa kuendelea. Kwanini usimuulize imam Sadiq namna ya kutatua matatizo katika jamii yetu? Atajibu kwa mambo matatu na je kama mambo haya matatu yatapatikana katika jamii yetu basi tutakua katika jamii zilizofaulu? Hii ni kwa sababu Amn, ‘Adl na Khisb vipo katika jamii nyingine lakini vimekuwa ndio malengo na wamesahau lengo halisi. Haya yote hutengeneza mazingira ambayo kupitia kwayo jamii itakuwa. Shughuli za ustawi wa jamii zinazofanywa ni mazingira ambayo ndani yake kunatakiwa kufanywa kitu kingine.
Kwa mfano, hali ya hewa ni yenye kubadilika sasa, msimu wa masika unakuja ambao ndani yake utapanda miti mipya. Lengo ni kupanda mitu kutokana na mbegu ambazo zinaweza kuzaa matunda baadaye au kukupa kivuli. Ili kuilea mimea hii unahitaji udongo uliolowa maji, kisha unahitaji hewa, mwanga wa jua na kila kitu katika hivi hutengeneza mazingira ya mmea kukua. Na jamii ipo kama hivi tu. Mambo haya matatu ambayo Imam Sadiq (‘a) ameyataja: Amn, ‘Adl na Khisb yanahitajika kwa ajili gani? Haya mambo yanahitajika ili kuyalea maisha ya mwanadamu na mwanadamu inabidi afikie malengo ya kuumbwa. Tunaweza kuona ulimwenguni je kizazi cha leo kinatakiwa kutathminiwa? Leo tunaweza kuona jamii ya binadamu ya kishenzi.
Tunahitaji mfumo wa uimam kwa ajili ya lengo hili. Imamat sio Meya au kiongozi wa nchi. Kazi ya imam ni kumtengeneza mwanadamu. Mambo mengine yote yaliyosalia ni mazingira. Ikiwa mambo haya matatu hayatakuwepo, basi mwanadamu hataweza kufikia lengo la maisha. Kwani uadilifu ndio msingi wa mafanikio lakini uadilifu pia hausimamishwi peke yake kama Amn na Khisb havijatajwa. Haya mambo yote yanahitaji kusimamishwa kwa pamoja. Tutataja hapo baadae ya kwamba uadilifu sio lengo bali ni nyenzo ya mwanadamu kwa ajili ya kufikia malengo ya maisha. Imamu ndiye mtunza bustani ya mmea huu. Leo hii waislamu hawana imam hivyo hata wanyama wanaona aibu kutokana nao. Madhehebu yanatengenezwa bila ya Imam. Hata mashia wanalelewa bila imam na tunaweza kuona hali zao. Wale ambao wamelelewa katika malezi halisi ya uimam ni kama Abu Dharr Ghaffari, ‘Ammar Yasir ni maajabu ya ubinadamu. Sisi hatutengenezwi chini ya uangalizi wa imam bali sisi tumejitengeneza wenyewe kwa jina la Imam. Yeyote ambaye anatengenezwa chini ya uangalizi wa uimamu hawezi kuabudia Taghuti anakwenda moja kwa moja kwa Allah.
Hotuba ya 2
Mtu hawi binadamu bila Taqwa na wakati wowote ikiwa kizazi cha mwanadamu kitakuwa bila Taqwa kitakuwa kimeharibu sehemu kubwa ya ubinadamu tu. Kizazi cha leo kinathibitisha namna gani mtu anaweza kuwa hatari kwa ubinadamu ikiwa hana Taqwa. Mtu hawezi kumharibu Mwenyezi Mungu lakini anaweza kuwaharibu binadamu, mwisho wake na akhera. Mtu amefanya hivi katika historia hata kama kuyataja haya hayatatunufaisha kwa kupata thawabu au adhabu kwa matendo yao. Kila mtu hutengeneza mwisho wake mwenyewe na Mwenyezi Mungu haingilii katika hili. Mwenyezi Mungu ametoa muongozo na ametoa kanuni na msingi ambayo kwayo mwanadamu hutengeneza mwisho wake. Hakuna yeyote anaye ingilia hili. Hivyo tunapaswa kuwa na wasiwasi juu yetu sisi wenyewe. Tunayo fursa na tutaondoka muda wowote. Inatakiwa tutengeneze akhera yetu kwa mikono yetu sisi wenyewe. Uthibitisho wa ubinadamu ambao umejiwasilisha wenyewe kwa kugawanyika katika vipengele tofauti tofauti.
Janga la sasa ni la Gaza ambalo ni kubwa zaidi japokuwa kua majanga mengine yanaendelea katika maeneo mbalimbali ikiwa ni dhuluma na kupotoka kwa jamii kunakoendelea katika kizazi cha sasahivi. Kinacho umiza zaidi ni Gaza ambapo tangia miezi mingi iliyopita wameendelea kuwa ni wahanga wa ushenzi. Kuna kundi moja la Mazayuni, Amerika, ulaya na baadhi ya nchi za kiarabu zinazoungana nao wapo kwenye kundi hilo moja. Biden ametangaza kwamba hivi karibuni Saudia itatangaza kuanzisha uhusiano mwema na kushirikiana na Israeli bila ya masharti. Pia nchi nyingine zinazofanana nayo ni kama Misrin na Uturuki ambazo zinatoa ushirikiano. Na nchi nyingine zilizobaki zipo kimya. Kwa mujibu wa mafunzo ya kiungu mwenye kudhulumu, kuunga mkono madhalimu na kubaki kimya mbele ya madhalimu wote hawa wanahesabika kuwa ni madhalimu.
Imam Sadiq(‘a) anasema kwamba uadilifu wa kiw3ango cha chini zaidi ni kuongea, kuitikia wito wa wanaodhulumiwa na kuwalaani madhalimu. Ikiwa hili halipo kwako pia basi wewe ni muasi aliyechupa mipaka na aliye potoka. Tangu wiki iliyopita madhalimu wameingia katika hatua mpya. Kwanza walikuwa wanashambulia miji kama Rafah, Gaza, Khan Yunus kisha wakashambulia kambi za wakimbizi. Jana wakimbizi wenye njaa walikuwa wamesimama kwenye safu kwa ajili ya kupata chakula na walishambuliwa kwa bomu ambapo Wapalestina wengi waliuawa katika safu hiyo. Tunaweza kuona ni nchi gani na imefanya nini katika masaa 24?wanachuoni na watawala wapo kimya. Na kisha kuna watu wenye chuki na vinyongo kama manawasibi na matakfiri ambao wanalaani hata wale wanaotoa msaada kwa wenye kudhulumiwa. Kwa kuwa Iran inawasaidia hawa wenye kudhulumiwa, basi hawa manawasib wanalaani Shia na sio Israel. Hii ina maaana kwamba inabidi uiunge mkono Israel ili wawaue watu wote na moyo wako upate amani ya moyo. Huu ndio ubinadamu wa leo. Ikiwa mti wa ubinadamu utakuwa pasina imam basi unaweza kuona matokeo yake. Wakati ambao unatumika pasina kuwepo kwa Imam hatutathmini ya kuwa kuna uharibifu unaotokea. Kazi ya imam sio kulipa bili na masuala ya umeme vitu ambavyo anaweza kuvifanya mtu yeyote. Bila ya Imam mtu hawezi kuwa binadamu bali wanabadilika na kuwa wanyama ambao wanaweza kuonekana. Tunaweza kuona kwamba kundi moja limekuwa wanyama, wengine ni wenye kuunga mkono, kundi lingine ni la watazamaji na kundi jingine ni lenye kulaani wenye kuwasaidia wanaodhulumiwa. Sasa ni kitu gani cha kwanza ambacho tunatakiwa kuwa tunakifanya. Ikiwa Allah wakati huu atatupa nguvu, fursa ya kufanya kitu hata kabla ya Sala ya Ijumaa inatakiwa tuanzishe mfumo wa utawala wa Imamat. Pindi itakapo anzishwa mfumo wa Imamat ulimwengu utapata amani na mtu atakuwa binadamu mwenye ufahamu wa ubinadamu. Wale ambao wamelelewa kwa mtazamo wa Banu Umayyah hawawapendi wale ambao wametoa msaada na kuwasaidia watu waliodhulumiwa Palestina. Huna hiari : inakuwa imeanzishwa kwamba inabidi uishi maisha yako chini ya Imamat. Kuna walioishi katika dunia ambapo maisha yanakuwa kwenye mfumo wa imamat. Katika kipindi cha utawala wa Imam Ali kulikuwa na mtazamo mmoja wa imamat. Alipokuwa akikamatwa mwanamke asiyekuwa Muislamu imam ‘Ali alikuwa akisema kuwaambia maswahaba: inabidi mfe kwa aibu, sasahivi hata kama wameshauawa watoto zaidi ya 30,000 Gaza hakuna anayeguswa na pia ni wenye kuwakemea wale ambao wanawasaidia wenye kudhulumiwa. Hatuna hiari ima tuwe chini ya Taghuti na Imamat.
Janga la Gaza limeweza kufichua mambo mengi na vigawanyo vya watu kwamba nani ni binadamu na nani ni mnyama. Hatuwezi kuhesabika kama binadamu kama hatutachukua kipimo cha Gaza kwa ajili ya kujitathmini wenyewe.