Khartum ilitangaza kuwa haina pingamizi kwa kanuni ya ujenzi wa kituo cha jeshi la wanamaji la Urusi nchini Sudan, na suala hili linapaswa kuidhinishwa katika bunge jipya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Sadegh Ali alisema kuwa mamlaka ya Sudan haina pingamizi lolote kwa ujenzi wa kituo cha jeshi la wanamaji la Urusi nchini mwao.
Alisema kando ya mkutano wa kidiplomasia huko Antalya kwamba “hatuna pingamizi la msingi kwa makubaliano yaliyofanywa katika serikali iliyopita, kwa sababu ni ahadi kwa nchi yetu.”
Mnamo Desemba 2020, makubaliano ya kiserikali yalitiwa saini kati ya Moscow na Khartoum juu ya uanzishwaji wa kituo cha usaidizi wa vifaa ili kukidhi mahitaji ya meli za Jeshi la Wanamaji la Urusi katika jiji la Port Sudan.
Lakini kutokana na mzozo wa ndani wa kisiasa katika nchi hii na kuvunjwa kwa bunge, upande wa Sudan bado haujaweza kukamilisha hatua za mwisho za kuidhinishwa kwake.
Balozi wa Urusi mjini Khartoum, Andrey Chernovil, alithibitisha Februari mwaka jana kwamba “Sudan bado haijaweza kukamilisha mchakato wa kuridhia makubaliano ya kuanzishwa kwa kituo cha jeshi la wanamaji la Urusi katika Bahari Nyekundu.”
Mkuu wa Diplomasia ya Sudan alieleza kuwa baada ya uchaguzi, bunge jipya la nchi yake litapitia makubaliano na Urusi kuhusu kuanzishwa kwa kituo cha jeshi la majini nchini humo.
Ali Sadegh Ali alisema kwamba bunge jipya linapaswa kuundwa ili kupitia upya mkataba huu na anashauri serikali kuliachie suala hili kwa bunge lililochaguliwa.