Njia ya Ramadhani inaongoza kwenye kupata radhi za Mwenyezi Mungu: Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Mkuu wa Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa katika : Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya Ijumaa – 15 March, 2024

Hotuba ya 1: Njia ya Ramadhani inaongoza kwenye kupata radhi za Mwenyezi Mungu
Hotuba ya 2: Vipi Sawm (kufunga) kunakuza Taqwa ndani ya mwanadamu?
Mwezi wa Ramadhani ni mpangilio wa Taqwa na ndio mwezi wenye taathira zaidi. Mwezi wa Ramadhani ni warsha ya Taqwa ambapo kwa kipindi cha muda mfupi mtu anaweza kuamilisha nyenzo nyingi ambazo zinamsababishia yeye kupata Taqwa na hivyo kuweza kupangilia maisha yake kwa mujibu wa Taqwa ili aweze kuishi maisha yake yote kama alivyoishi ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Moja ya chanzo cha kupata Taqwa na kuufahamu mwezi wa Ramadhani ni Dua ya 44 ya Imam Sajjad (‘a) ambayo anaisoma kwa ujio wa mwezi wa Ramadhani.
Imam (‘a) anasema katika Dua
الْحَمْدُ للهِ الَّذِي هَدَانَا لِحَمْدِهِ
Sifa njema ni za Mungu aliye tuongoza ili tutaje sifa zake
وَجَعَلَنَا مِنْ أَهْلِهِ، لِنَكُونَ لِإِحْسَانِهِ مِنَ الشَّاكِرِينَ
Na ametuweka miongoni mwa watu wenye kumsifu, ili tuwe ni wenye kushukuru ihsani zake

وَلِيَجْزِيَنَا عَلَى ذلِكَ جَزَآءَ الْمُحْسِنِينَ
Na ili aweze kutulipa juu ya hilo malipo ya watendao mema

Anamsifu Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye kutuongoza kunako kumsifu. Na katika Dua nyingine Imam Sajjad (‘a) anasema maneno haya haya katika kumshukuru Allah ambapo anamshukuru Allah kwa kumpa fursa na ya kuwa ni mwenye kumshukuru Allah. Ametuhesabu sisi kuwa miongoni mwa watu wenye shukurani kwa neema zake. Hatuhesabiwi kuwa miongoni mwa watu ambao sio wenye kumshukuru Allah kwa fadhila zake. Imam (a) anawasilisha dhana tatu; kwanza ni tawfiiq ya kushukuru, pili kutuhesabu kuwa miongoni mwa watu wenye kushukuru na tatu ni malipo ambayo Allah atatulipa.

وَالْحَمْدُ للهِ الَّذِي حَبَانَا بِدِينِهِ،
Na kila sifa njema ni zake Allah aliye tuneemesha kwa dini yake,

وَاخْتَصَّنَا بِمِلَّتِهِ، وَسَبَّلَنَا فِي سُبُلِ إحْسَانِهِ،
Akatufanya kuwa maalumu kwa mila yake, na akatuelekeza kwenye njia za wema wake,

لِنَسْلُكَهَا بِمَنِّهِ إلَى رِضْوَانِهِ،
Ili kupitia wema wake tuweze kuishika njia ya kutufikisha katika radhi zake,

حَمْدَاً يَتَقَبَّلُهُ مِنَّا، وَيَرْضَى بِهِ عَنَّا.
Shukurani ambayo atatukubalia na kuturidhia kwayo!

Katika paragrafu hii ya pili Imam anaendelea kumsifu Mwenyezi Mungu kwa kutupa neema na zawadi ya dini. Ni neema ya pili ambayo ameweza kuitoa makhsusi kwa waumini, Waislamu kuwa watu wake. Katika lugha ya Kiarabu Millat ina maana ya njia, Imani au chuo cha kifikra. Njia ya Mwenyezi Mungu ni Milla ya Ibrahimu au mtume wetu mtukufu (s.a.w) na hii ndio njia ambayo kwayo waja wa Allah wanaweza kumfikia na Allah ameitenga njia hii kwa ajili yetu. Wengine pia wanayo njia hii lakini hawakuifanyia kazi. Sio kwamba Mwenyezi Mungu alitengeneza dini kwa ajili ya Waislamu, waumini na wafuasi wa mtume (s.a.w) na kuwatenga wanadamu wengine. Wenye kuhutubiwa na dini ya Allah , Qur’an na Mtume (s.a.w) ni wanadamu wote Wakati njia hizi za wokovu zinapowekwa kwa ajili ya ubinadamu wote basi wengine hawajaipata njia hii isipokuwa Umma wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo wakati tukitembea kwenye njia hii Mwenyezi Mungu ametufanya kuwa makhsusi. Kisha Allah ameweka njia ya neema zake, kwa kutuweka katika njia hii ili tuweze kupita njia hii na kufikia radhi zake.
Ridhwan ina maana ya raha iliyoongezeka au tunaweza kusema asili ya furaha. Tunatoa sifa hizi ambazo zinakubalika kwetu. Kigezo alichokiweka Allah katika kutoa riziki sio kwamba mtu anatakiwa kuwa Muislamu mzuri. Nk. Badala yake amemuangalia kila mmoja kama kiumbe. Inatosha tu kuwa ni kiumbe ili kuomba chochote kutoka kwa Allah. Allah ametoa riziki na fadhila bila ya masharti na hakusema kuwa nitakupeni tu ikiwa mtakuwa waumini wazuri. Hivyo basi Allah ametoa riziki kwa makafiri, wanafiki na hata kwa maadui zake mwenyewe. Kwa kuwa Allah ni Mola Mlezi ( Rabb) ni jukumu lake kutoa mahitaji kwa kila mmoja. Lakini katika hatua ya pili ya kukubali ameweka masharti. Anasema pindi mtakapotaka kuzirudisha hizi fadhila kwangu, basi hapo kuna sharti kwamba nitakubali tu kutoka kwa wachamungu ( Muttaqeen). Taqwa ni sharti la kukubalika matendo. Na hapo ndipo ambapo mwanadamu hunyesha ujuzi wake ili kurudisha ambacho Allah amempa na kukifanya kiwe ni chenye kukubalika. Ikiwa mtu atafanya basi atakuwa ni mwenye kipawa kwa kutimiza masharti yote. Na baada ya kukubaliwa basi humpendeza Allah.
Kukubaliwa na kuridhiwa ndizo hali mbili ambazo Allah ameweka kwa ajili ya waumini. Inatakiwa ufanye matendo yako yawe ni yenye kukubaliwa na yenye kuridhiwa na Allah pia. Kila mtu hutaka kuwaridhisha wengine na wengine nao wameshughulishwa na kutaka kuwaridhisha wengine pia. Wazazi, watoto, marafiki, wafanya biashara, watu wengine na maulama. Siku zote hutaka kuwafurahisha na kuwaridhisha watu ili waweze kuchukua maslahi kutokana na furaha na ridhaa ya watu kama kutengeneza pesa, kupata heshima, kukubalika na maslahi mengine binafsi. Kuwafanya watu wasiwapende hiyo wanaizingatia kuwa ni adhabu. Wanamzingatia mtu kuwa hajafanikiwa kama hajaweza kuwaridhisha na kuwafurahisha watu. Nimesoma hii hadithi ya kwamba mtu anaye mkasirisha Allah katika kuwafurahisha watu basi Allah humfanya kuwa ni mwenye kuelemea kwa watu. Kwa ujumla huwezi kuwaridhisha watu na Allah kwa pamoja katika jambo moja. Hapa ndipo kunakuwa na wanaotaka kumridhisha Allah kisha wanapata kutoridhiwa na Allah. Namna alivyokuwa Imam Sajjad ( ‘a) katika mahakama ya Yazidi ambapo mzungumzaji aliwekwa juu ya mimbari ili kutoa hotuba ili kudhibiti hali. Mzungumzaji alimsifu Allah kwa kumpa Yazidi heshima na kuwadhalilisha wengine. Imam Sajjad (‘a) alimsimamisha mzungumzaji na kumwambia umemkasirisha muumba kwa ajili ya kumfurahisha kiumbe. Na hiki ndicho kitu ambacho tunakifanya usiku na mchana. Kila mtu yupo kwenye fikira za kuwaridhisha watu, lakini wewe unatakiwa kutafuta radhi za Allah. Hadithi hiyo hiyo inasema kuna mtu mwingi ambaye anawakasirisha watu kwa ajili ya kumridhisha Allah basi huyu Allah huchukua mambo yake yote na kumtimizia. Hii ni kwa sababu hakujali kuwakasirisha watu kwa ajili ya Allah. Kupata radhi za Allah ni jambo muhimu sana kwa waumini lakini kivitendo sisi hatuweki umuhimu katika kutafuta radhi za Allah katika jambo lolote. Tunatumia maisha yetu katika kuwafurahisha mke, mume, watoto, wazazi, ndugu, ukoo, majirani, vyama vya siasa, viongozi, watu na imamu wa msikiti anafanya ili kuwafurahisha wafuasi wake. Hawatoi umuhimu kwenye kumfurahisha na kutaka radhi za Allah.

وَالْحَمْدُ لِلّه الَّذِي جَعَلَ مِنْ تِلْكَ السُّبُلِ شَهْرَهُ شَهْرَ رَمَضَانَ،
Na kila sifa njema anazistahiki Allah ambaye amechagua kutoka katika njia hizo mwezi, ambao ni mwezi wa Ramadhani

شَهْرَ الصِّيَامِ، وَشَهْرَ الإِسْلاَم، وَشَهْرَ الطَّهُورِ،
Mwezi wa kufunga, mwezi waa kujisalimisha (Islam), mwezi wa tohara,

وَشَهْرَ التَّمْحِيْصِ، وَشَهْرَ الْقِيَامِ،
Mwezi wa kuweka kipimo cha majaribu, mwezi wa kusimama kwa ajili ya sala,

الَّذِي أُنْزِلَ فِيْهِ الْقُرْآنُ هُدىً لِلنَّاسِ،
“Ambao imeteremshwa humo Qur’an kuwa ni uongofu kwa watu,

وَبَيِّنَات مِنَ الْهُدى وَالْفُرْقَانِ،
Na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi” (2:185)!
Katika paragrafu hii Imam Sajjad (‘a) anawasilisha sifa za mwezi wa ramadhani. Kipaumbele imekuwa ni kumshukuru Allah kwa kutuwekea njia ambazo zinatupeleka katika kuzipata radhi za Allah. Anasema moja ya njia hizo ni mwezi wa Allah ambao ni mwezi wa Ramadhani. Sifa ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani ni kwamba Ramadhani ni njia. Unapoingia katika mwezi huu, fadhila ambazo tunazipata ni njia ambayo Allah ametupatia. Ikiwa mtu atapata kitu bila kukifahamu kitu vizuri basi ima atakipoteza au atakiharibu. Ni kama Qur’an ikiwa tutakuwa na ufahamu sahihi wa Qur’an basi hatutaweza kuipoteza na kuitumia vibaya. Tunaheshimu sana Qur’an lakini kutokana na ufahamu mdogo tumeipoteza. Tunaitumia kufanya istikhara( kutaka ushauri kutoka kwa Allah), kuapia, kuwasomea khitma maiti au kutafuta thawabu. Qur’an ni mwongozo na inapotea ikiwa hatutachukua uongofu ndani yake hata kama tutaisoma ili kuwafanya watu wengine waisome maishani. Ni kama katika mwezi wa Ramadhani. Tunaweza kuona ni miezi ya ramadhani mingapi Allah ametupa tangia kipindi tulipo pevuka na kubalehe. Mtoto hukua kiakili na kuanza kupata uwezo wa kupambanua kizuri na kibaya. Kuna kipindi cha utoto ambapo watoto hukosa ufahamu huu na hivyo huongea ya sawa na ya makosa kwa pamoja pasina kupambanua. Hiki ni kipindi cha kukosa ufahamu na utambuzi ambacho ni kati ya miaka kumi 10 na kumi na mbili 12 japokuwa kuna wengine wanakuwa ni wa kipekee wana ufahamu mzuri. Inawezekana pia kuwa mtu anaweza kushindwa kukuza ufahamu wake hata kama atafikisha miaka 100 na watu wa namna hii ni watu maalumu. Tunapaswa kuwatazama watoto kwa ukaribu zaidi pindi akili yao inavyo pevuka na kuwazoezesha kutekeleza matendo ya kidini. Watoto wanaweza kufunga sawmu. Ikiwa mabinti ambao ni dhaifu wanatakiwa kufunga hali ya kuwa bado wana umri wa miaka 9 , anatakiwa afunge, sasa kwanini kijana wa miaka 9 asifunge sawmu hali yakuwa binti wa miaka 9 anafunga?
Kuna msomi mmoja asiyekuwa wa Kiislamu kutoka nje alikuja Pakistan na kusema kwamba Allah ametufanyia mambo kuwa mepesi kwa ajili yetu, hivyo unatakiwa kufanya kitu ambacho ni rahisi kwako. Kama sala ni ngumu kwako basi usisali. Kama funga ni nyepesi kwako basi funga. Alikuwa anahubiri kigezo hiki kwamba chochote unachokiona chepesi kwako fanya na chochote ambacho ni kigumu achana nacho. Kwa mtazamo wa huyu msomi dini ni biashara.
Allah ametumia neno “ Kulfat” kwa ibada. Allah amemfanya mwanadamu kuwa mukallaf ambayo ni hatua kubwa na ya juu ambayo ni baraka kubwa kwa mwanadamu. “Kulfat” maana yake ni ugumu ambao mwenyezi Mungu ameuweka kwetu, lakini kwa kiwango gani? Ni kiwango cha uwezo uliopewa. Kwa mambo ambayo huna uwezo wa kuyafanya mambo hayo hayawi wajibu kwako. Katika kufunga kuna ugumu na hivyo funga imefanywa kuwa wajibu. Sala, udhu na mambo mengine yote zaidi ya tamaa na furaha hakuna kitu kilichokuwa rahisi. Kutafuta elimu kuna ugumu. Allah hataki akuone ukiwa umepumzika na kustarehe. Ni dini gani ambayo unawafundisha watu?
Mwenyezi Mungu amekupa njia ya Ramadhani ambayo unaanza kwa watoto ambao ni wenye akili ya kuweza kupambanua baina ya kizuri na kibaya. Hiki ni kitendo cha kidini ambacho matokeo yake hayafikiwi lakini ni kwa ajili ya kuanza kumfanya mtoto kuishika njia ya kufunga.
Imam Sajjad (‘a) anasema kila sifa njema anazistahiki Allah kwa kutuonyesha njia na safari moja ya Ramadhani. Hivyo je ni katika umri gani tunatakiwa kupanda gari hili. Kuanzia miaka ya kuwa na akili ya utambuzi hata kama adhabu nakuja baadaye katika umri wa miaka kumi na tano. Ikiwa mtoto hatawekwa kwenye njia ya dini basi ataingia kwenye njia ya shetani. Hivi ni kwa sababu shetani hasubiri mtoto afikie balehe. Qur’an inasema kwamba shetani huanza mashambulizi yake kwa mwanadamu mapema sana kuanzia wakati wa kabla ya kutunga ujauzito. Shetani anataka mtoto azaliwe katika njia yake. Humshambulia mtoto akiwa tumboni kupitia kutokuwa na maadili, asiwe msafi, mama fisadi. Ramadhani inabidi ijulikane kama njia ambayo tunatakiwa kupita. Njia hii inaishia katika radhi za Allah. Pindi mtu anapoudiriki mwezi wa Ramadhani na kuufunga kwa uzuri huzifikia radhi za Allah. Pindi mtu anapo pata radhi za Allah anakuwa kapata kila kitu. Imam Hussain (‘a) anasema aliyekupata wewe kapoteza nini? Mtu ambaye amepata radhi za Allah amepata ulimwengu mzima na ambaye hajapata radhi za Allah basi atakuwa hajapata chochote. Tunamuomba Allah atujaalie tupite safari ya utumwa kwa muongozo wa Imam Sjjad (‘a).

Hotuba ya 2
Saumu ( kufunga ) ni mpangilio mmoja wa mwezi wa Ramadhani
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ {183}
Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu , kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu
Katika Surah Baqarah, Aya ya 183 Allah anawahutubia waumini ya kwamba mmefaradhishiwa funga kama walivyo faradhishiwa watu waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allah ( Taqwa). Kama Taqwa itapatikana hii ndio maana ya Sumu na la sivyo itakuwa ni njaa tu. Kuna adabu na mipaka ya saumu ambayo ikiwa Allah atatupa taufiki tutaiwasilisha kupitia dua ya imam Sajjad (‘a). Ulinzi huu wa Taqwa unaweza kupatikana kupitia saumu. Tangia tulipoanza sala za Ijumaa tuliwahi kutaja na pia wanazuoni wakubwa kama Mutahhari amesema kuwa maana ya neno Taqwa imewasilishwa kimakosa kama kuogopa au kujizuia. Siku chache zilizopita kuna dokta alitujia, yeye ni katika Ahlu Sunna na ana ratiba ya masomo kwa wanafunzi wa chuo. Kwa kuwa uasi wa imani unaenea vyuoni na tulisema unafanya kazi kubwa. Alisema kuna kipindi mimi mwenyewe nilikuwa muasi wa imani na kuiacha dini. Nilikwenda nje ya nchi kwa ajili ya elimu ya juu zaidi na katika kipindi hicho nilitubu na kurudi kuwa Muislamu tena. Sasahivi anajifunza dini kwa utafiti na kuna kikundi kamili. Alikuwa akisema kwa kurudia namna gani tunavyowafanya wanafunzi kuwa karibu na dini, lakini nilitaka kujua ni namna gani ulikuwa muasi na kuacha dini. Alikuwa na tahadhari sana na hazungumzi kwa uwazi. Nataka kujua kwa nini vizazi vyetu vipya wanakuwa waasi wa dini.
Alijibu kwa kusema tulikuwa na profesa ambaye hakuwa na dini na alikuwa akitutengenezea mashaka katika akili zetu na tulipokuwa tukienda kupeleka mashaka hayo kwa wasomi hawakuwa na majibu na hili lilikuwa likikuza imani yetu kwa huyo profesa. Baadhi ya wasomi wa dini walikuwa wakitutukana, wengine walisema hizi ni njama lakini hakuna mtu aliyekuwa akitoa jawabu japo jepesi. Pindi tulipokosa kupata majibu tulisogea na kujiunga na njia ya uasi ( ulahidi). Nimewasilisha ushahidi huu ili kuthibitisha kwamba tafsiri mbaya ya dini huwafanya watu kuiacha dini. Shahidi Mutahhari ametoa rejea ya kitabu kimoja maarufu cha maadili kama kitabu cha upotoshaji. Anasema kwa sababu mtazamo wa dini umeelezwa kimakosa na misingi ya maadili potofu na hivyo basi mtu akisoma kitabu hiki atapotea. Mutahhari alikuwa amekasirishwa na maana ya Taqwa ambayo imetafsiriwa kuwa ni kuogopa na kujizuia. Kama utatathmini Aya ya 183 utapata hili kuwa ni kweli. Lengo la saumu limefanywa kuwa ni Taqwa. Kama Taqwa ni kuogopa je kufunga kunatengeneza uoga? Au hukuza uwezo wa kubaki na ulinzi wa maana halisi na sahihi ya Taqwa? Kwa hiyo, je saumu imefanywa kuwa wajibu ili uogope? au ukuze kujizuia? Au ni kwa ajili ya kukuza uwezo na nguvu ya kubaki umelindwa na kuhifadhika.
Katika mwezi wa Ramadhani mchana wake unatakiwa kubaki katika hali ya kufunga saumu. Unaweza kufunga mwaka mzima lakini saumu ya lazima ni ya mwezi wa Ramadhani. Saumu ni kwa ajili ya mchana lakini ndani ya Ramadhani ni mchana na usiku pia. Saumu hukuza nguvu kubwa ya uchamungu. Unapoingia ndani ya uhalisia wa saumu ndio utajua nini kinapata nguvu zaidi ndani yako. Unaweza kusema kwamba mtu hudhoofika wakati wa saumu. Kwa hiyo uwezo wa ulinzi huongezeka vipi? Nguvu halisi ambayo Allah amempa mwanadamu kama msingi unaompa ubora juu ya viumbe vingine ni nguvu ya nia au utashi ( Irada). Mwanadamu ana nguvu ya utashi na hii ndio siri ya mwanadamu. Hata kama mwili utakuwa dhaifu lakini kama nguvu ya utashi na nia ni imara anaweza kufanya mambo mengi magumu. Na kama nguvu ya utashi ni dhaifu basi hataweza kufanya hata jambo dogo. Kwa nguvu ya utashi mtu hulinda maisha yake. Hivyo basi, msingi wa Taqwa ni uwezo wa nguvu ya utashi. Nguvu hii ya utashi hutiwa nguvu na kuimarishwa na saumu. Na pindi nguvu ya utashi inapokuwa imara basi mtu kupitia kwayo anaweza kupata mpango wa ulinzi. Hivyo basi Mwenyezi Mungu ameifanya saumu kuwa wajibu ili maisha yako ya dunia na akhera yaweze kuwa salama. Tunamuomba Allah atujaalie saumu za namna hii. Na kupitia saumu huweza kuamsha hisia zilizo kufa. Sisi wote ni miili iliyokufa ambayo inapumua, na ishara za hili ni kwamba hisia za ubinadamu zimekufa na uthibitisha wa hili ni kwamba mbele ya uwepo wa watu bilioni 8 ubinadamu upo unachinjwa ndani ya Gaza na watu wote wamekaa kimya kama watazamaji.
Siku chache zilizopita mtu mmoja Uturuki aliua paka mmoja mtaani kwa kumpiga teke na cccyv camera zikanasa tukio hili na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Watu wa Uturuki waliandamana ili kumfungulia mashtaka mtu huyu, na mtu huyu alihukumiwa kwenda jela kwa miezi 15. Mtu huyu alifungwa jela na kuwa na tabia njema jela kisha ndio akaachiwa kabla ya kutimiza muda wake wa adhabu. Wakati alipo achiwa watu waliandamana tena katika mitandao ya kijamii, wakaja pia mbele ya mahakama na hali ya Uturuki ilibadilika na kuwa mbaya sana hadi Erdogan alilazimika kuingilia na kutoa amri mtu huyu afungwe tena na aongezewe adhabu yake. Unaweza kuona kwamba Uturuki ni nchi ya Kiislamu na kwa kuuawa paka kulipazwa sauti nyingi. Hiyo hiyo Uturuki, Pakistan na nchi nyingine za Kiislamu unaweza kuona hotuba zao, futari. Mamia ya watoto, wanawake na wanaume wanakufa kila siku Gaza na hakuna yeyote anayezungumzia kuwahusu. Hii ina maana ubinadamu umekufa. Hizi hisia zilizokufa zinaweza kuamshwa na saumu. Moja ya faida ya saumu ni kuamsha ubinadamu uliokufa ndani mwetu. Tunamuomba Allah awape uokovu wale wenye kudhulumiwa kutokana na hawa madhalimu na awaangamize.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *