Laylatul Qadr- Kushuka kwa malaika kwa mwanadamu/ kuhusu Quds , march ndani ya miji kisha kuelekea Palestina: Hujjatul Islam Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya Ijumaa – 29 March, 2024

Hotuba ya 1: Laylatul Qadr- Kushuka kwa malaika kwa mwanadamu
Hotuba ya 2: kuhusu Quds , march ndani ya miji kisha kuelekea Palestina
Mwenyezi Mungu amefanya mipangilio maalumu kwa ajili ya mwanadamu ili aweze kuipata Taqwa na miongoni mwayo ni mwezi wa Ramadhani. Mpangilio uliotengenezwa ndani ya Ramadhani unatosha sana kwa mwanadamu kukuza Taqwa yake katika maisha haya. Na ndani ya mwezi huu mtukufu mipangilio ya juu iliyo pangwa ndani yake ni Saumu. Imam Sajjad katika dua hii anataja kuhusu baraka hii ambapo amewasilisha hili katika ufahamu mkubwa ambao hutoa maarifa kwa waumini kuhusu mwezi huu.

فَأَبَانَ فَضِيْلَتَهُ عَلَى سَائِرِ الشُّهُورِ
Akabainisha ubora wake juu ya miezi mingine

بِمَا جَعَلَ لَهُ مِنَ الْحُرُمَاتِ الْمَوْفُورَةِ وَالْفَضَائِلِ الْمَشْهُورَةِ،
Kwa matukufu mengi aliyoyaweka na fadhila nyingi zilizo mashuhuri

فَحَرَّمَ فِيْهِ ما أَحَلَّ فِي غَيْرِهِ إعْظَاماً،
Basi akaharamisha ndani yake alicho kihalalisha katika miezi mingine kwa kuutukuza,

وَحَجَرَ فِيْهِ الْمَطَاعِمَ وَالْمَشَارِبَ إكْرَاماً،
Na akaharamisha ndani yake kula na kunywa kwa kuupa heshima,

وَجَعَلَ لَهُ وَقْتاً بَيِّناً لاَ يُجِيزُ جَلَّ وَعَزَّ أَنْ يُقَدَّمَ قَبْلَهُ،
Na akauwekea muda maalumu ulio wazi, Mwenyezi Mungu aliye tukuka haruhusu kuutangulia

وَلا يَقْبَـلُ أَنْ يُؤَخَّرَ عَنْهُ،
Na hakubali kuuchelewesha

ثُمَّ فَضَّلَ لَيْلَةً وَاحِدَةً مِنْ لَيَالِيهِ عَلَى لَيَالِي أَلْفِ شَهْر،
Kisha akaupa ubora usiku mmoja katika masiku yake kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja

وَسَمَّاهَا لَيْلَةَ الْقَدْرِ،
Akauita usiku wa cheo;

تَنَزَّلُ الْمَلائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإذْنِ رَبِّهِمْ مِنْ كُلِّ أَمْر،
“huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya mola wao mlezi kwa kila jambo,

سَلاَمٌ دَائِمُ الْبَرَكَةِ إلَى طُلُوعِ الْفَجْرِ،
Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri” (97:4-5)

Ndani ya mwezi huu, Allah ameufanya mwezi kuwa bora kuliko miezi mingine kwa fadhila zake zilizo wazi kama inavyoweza kuonekana kwa kila mtu kwa uwazi kabisa. Je kuna ishara zipi ambazo kwazo tunayapata haya? Ni mambo matukufu mengi ambayo yamewekwa kwa ajili ya mwezi huu . Hurmat, Haram, Ihtiram, Marhumu maneno haya yote yanatoka kwenye mzizi mmoja ambapo maana yake halisi huendelea kuhifadhika na kupatikana mabadiliko madogo. Kuna adabu maalumu zilizo ainishwa kwa ajili ya mwezi huu na ndizo ambazo zinaupa utukufu mwezi huu.
Allah ameweka fadhila nyingi zinazo fahamika kwa mwezi huu. Mambo ambayo yanaruhusiwa katika miezi mingine, yamekatazwa ndani ya mwezi huu. Kama mtu atafanya hayo mambo yaliyo katazwa basi io tu kwamba ni dhambi bali ni kukufuru utakatifu wa mwezi huu. Kwa ajili ya utukufu wa mwezi huu Allah ametukataza kula na kunywa tangia alfajiri hadi kuzama jua ambapo huanza tangia muandamo wa mwezi hadi mwisho wa mwezi wa Ramadhani. Ramadhani ni wakate wa fursa na sio kitendo. Saumu ni kitendo kwa ajili ya Allah ambapo Allah ameweka wakate wake maalumu. Allah haruhusu kuongeza au kupunguza katika mwezi huu. Kuna matendo ambayo yana masharti ya kutendekea katika muda maalumu. Kuna baadhi ya wajibu ambazo zinaweza kutekelezwa wakate wowote na yanakubalika kama kurudisha mkopo kwa mtu ( kulipa deni) isipokuwa kama mtakuwa mmekubaliana muda maalumu. Na kuna mambo ya wajibu ambayo inabidi yatendeke katika wakati maalumu na yana umaalumu wake. Maulama wanasema mwanadamu anatakiwa atende matendo kwa wakate maalumu na wakate hapa ni kielelezo tu cha ambapo unawasilishwa kitendo, lakini kuna baadhi ya mambo ambayo muda una maana yake ambapo ikiwa kitendo hakitafanyika katika wakate wake hupoteza thamani yake. Ndani ya Ramadhani wakati huwa muhimu zaidi na una athari. Allah anataka wakate huu ambapo unatakiwa kufanya hiki. Kama ilivyo pia katika Sala za kila siku ambapo unatakiwa kuzisali kwa wakate maalumu.
Kisha Allah ameipa Ramadhani ubora mwingine zaidi ambapo kuna usiku mmoja mnalaumu ambao ni bora zaidi ya miezi 1000. Kama tutautazama usiku mmoja ambao unakuwa ni masaa kumi au kumi na mbili kuwa na ubora kushinda miezi 1000. Usiku huu unaitwa usiku wa Laylatul Qadr, usiku wa cheo ambapo ndani yake Malaika na Ruhul Quds hushuka kwa idhini ya Allah wakiwa na mambo yote yanayomhusu mwanadamu. Usiku huu ni usiku wa amani hadi asubuhi. Malaika hawa hu8shuka na amri Allah juu ya wale ambao Allah anawataka miongoni mwa waja wake. Na hiki ndicho kilele cha fadhila za mwezi huu. Miezi elfu moja ni sawa na miaka 83 ambapo ni mzuri wa maisha mazuri. Kama tutafanya mahesabu ya uwajibikaji tunapoteza wakate kiasi gani? Wanafunzi wetu wanasema hatupati muda. Nilifanya kazi na kisha nikawambia muna muda kiasi gani. Kama unapo amka asubuhi unaitumia muda mwingi ukiwa kitandani kwa sababu ya uzembe na wakate huu unakuwa unapotezwa. inatakiwa tujihesabu na kujua kuwa je ni maeneo gani mengine tunapoteza muda. Tunapoteza muda mwingi katika matendo ya kimazoea ya kila siku kama kula, kuaongea na kulike katika simu za mkononi, tazama ni kiasi gani umeongea na simu kitu ambacho hakikuwa na faida yeyote. Kama utahesabu utapata hata yule mtu anaye shughulishwa zaidi hupoteza masaa nane hadi kumi kila siku. Leo kama inavyosemwa ndani ya vyombo vya Habari ni kwamba asilimia 40% ya vyakula hupotea aidha ni wakate wa kupikwa au wakate wa kula. Na kwa mujibu wa takwimu kuna watu bilioni 2 hawapati chakula inavyopaswa. Katika kipindi cha Hijja kuna mashirika makubwa ambayo hukusanya chakula kinachotupwa na mahujaji. Inabidi tuhesabu hilo kama kilichotupwa ni wakate, nyenzo, umri, chakula, maji, umeme n.k.
Kuna tahadhari ambayo imetolewa ulimwengu mzima kuhusu upungufu wa maji. Leo hii kuna maeneo mengi hakuna mvua na baadhi ya maeneo ipo mvua chache na maji huyapata kwa kuchimba visima. Tunapoteza maji mengi wakati tunapokuwa tunachukua udhu. Kitu kikubwa zaidi tunachokipoteza ni umri. Kama tuna miaka themanini kwa kigezo hiki unaweza kuona tumepoteza miaka mingapi ya umri wetu? Kama mtu atafanya kazi kwa bidii usiku na mchana kwa muda wa miaka themanini , hawezi kupata faida kama ambayo anaipata kwa usiku mmoja wa Ramadhani. Allah amekupa fursa ya kipekee ya kuweza kufanya safari ya miaka 83 kwa usiku mmoja. Huu ni usiku wa cheo na vipimo. Malaika hushuka na usiku hubaki ukiwa na amani hadi asubuhi. Malaika hawashuki kwa anayekimbia. Ndani ya Qur’an mwanadamu ameelezewa kuna na uhusiano wa kina na malaika. Malaika wana uwezo wa kutenda mambo katika ulimwengu mzima na sio majini. Bila ya kuwepo malaika hakuna kazi ambayo binadamu anaweza kuifanya peke yake. Pamoja na mahusiano haya makubwa baina yetu na malaika, je tuna ufahamu kuwahusu kiasi gani? Je uliwahi kukutana na malaika katika maisha yako? Hali ya kuwa wapo na wewe katika kila hatua na kila kazi. Kwanini bado wewe ni mgeni kwa viumbe hawa? Malaika wapo wanaofanya kazi ya kufikisha matakwa ya Allah. Malaika wana mahusiano ya moja kwa moja na mwanadamu bila kujali dini au dhehebu. Na hata kwa wasiokuwa binadamu. Matone ya mvua hushuka kupitia malaika. Ni kiumbe ambaye ana mahusiano ya karibu sana na sisi, lakini sisi tumekaa mbali sana na hatujui pia, wakumbuke au washukuru. Katika usiku huu Malaika hushuka kutoka kwa ajili ya kumtimizia mwanadamu alichokiomba. Na miongoni mwa Malaika hao ni Ruhul Quds, kiongozi wa malaika ambao hushuka chini kwa ajili ya huduma maalumu kwa waja wa Allah. Huwa anakuja na baraka, amani, usalama na maamuzi na hutekeleza amri ambayo wameagizwa na Allah. Malaika walihusishwa katika kuumbwa kwa mwanadamu. na walihabarishwa juu ya kuumbwa kwa mwanadamu nao waliweka pingamizi pia. Hii ni kwa sababu wana mahusiano ya kina na kazi yako itaongezeka. Mwanadamu atafanya ufisadi, kumwaga damu ambao inabidi kutatua tatizo hili. Kisha Allah aliwafahamisha uhalisia wa mwanadamu ambapo baada ya hapo walijisalimisha kwa mwanadamu. malaika wanamfanyia mwanadamu mambo yote. Kama una mahusiano na mtumishi ambaye amewekwa na Allah, basi magumu yote siku zote yatakuwa yanapatiwa ufumbuzi. Malaika ni watumishi ambao huendesha mambo ya mwanadamu. malaika hawa hushuka katika usiku wa Laylatul Qadr. Hivyo tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya kuwapokea malaika na tunatakiwa kukutana na ambaye atayafanya magumu yetu kuwa mepesi. Katika usiku huu Allah ndiye anaamua na malaika huja kutekeleza. Hii ni taufiki yako utachagua kuipoteza Laylatul Qadr au uifanye sehemu ya hatima.

Hotuba ya 2
Kwa ajili ya Taqwa Allah ameweka mpangilio wa Ramadhani ambapo chanzo kikuu chake ni Saumu. Saumu ina mafungamano makubwa na ya kina na Taqwa. Saumu maana yake ni kuacha kwa kukusudia mambo ambayo yalikuwa yanaruhusiwa. Hili linafanywa na Allah ili kuendeleza na kutia nguvu, kuondoa unyonge ambayo ni nguvu ya utashi. Unapaswa kuacha mambo yote ambayo Allah amekutaka uyaache tangia alfajiri hadi usiku katika mwezi mzima wa Ramadhani. Mtu anapofanya jambo kwa kukariri kwa muda wa wiki tatu hadi sita, jambo hilo huwa sehemu ya ndani ya mwanadamu. Allah ameweka wiki nne hizi ka ajili ya kuitia nguvu nia na utashi wako. Jambo kubwa zaidi ni kuacha kitu unachokipenda na kukitamani. Matamanio yana nguvu za kutengeneza muhemko na kuuzuia muhemko huu unahitaji nguvu ya utashi. Ndani ya dini na Akhera kila kitafanywa na mtu kupitia nguvu ya nia. Hivyo inabidi tuimnarishe nguvu yako ya utashi ndani ya mwezi huu.
Katika miaka hii Ramadhani ni muhimu sana kwa sababu kila mtu ameona na anaendelea kuona namna gani Waislamu tulivyokuwa wanyonge. Vita ya Gaza imeweza kufichua na kuwaumbua Waislamu wote lakini pia ubinadamu kwa ujumla. Licha ya madai hayo yote ulimwengu umeshuhudia na kuona namna viongozi wa Kiislamu walivyokuwa dhaifu, wasomi, watu na Waislamu wenye shauku wa Pakistan. Tunafahamika sana kwa shauku na kusimama kwa ajili ya vitu vidogo. Mpakistan anaweza kuchoma vitu vyote ikiwa mtu ataitukana Qur’an, lakini Pakistan nzima imeungua na hawakufanya kitu chochote. Hii ni kwa sababu nguvu ya utashi ni dhaifu. Bado hatujakuza kiini cha saumu ambacho ni nguvu ya utashi. Vita ya Badr ilipiganwa tarehe 17 ya mwezi wa Ramadhani. Hii ilikuwa ni vita ambayo ilitengeza mpango wa vita vingine. Qur’an ilikubali na kupongeza vita ya Badr na kuwapa heshima masahaba walioshiriki vita ya Badr. Walipigana vita vya maamuzi magumu ambapo walikuwa na mapanga mawili na farasi wawili. Idadi ya Waislamu ilikuwa ni 313 ambapo wengi wao walikuwa ni wazee ambao iliwabidi kupambana na jeshi la majemadari ambao walikuja kwa nia ya kuwamaliza Waislamu, lakini Waislamu walishinda kwa nguvu ya utashi. Waislamu walihamaki sana walipowaona maadui. Allah aliwasaidia Waislamu hawa kupitia Malaika. Malaika waliongeza nguvu ndani ya utashi wa Waislamu na wakapigana. Leo hii Waislamu wapo bilioni 2 na wana nchi zenye nguvu kubwa na kijitawi cha Wazayuni kimewatukana Waislamu ambapo jambo hili litabaki katika historia. Inatakiwa tuondoe uchafu huu kwa Waislamu na nafasi Nzuri zaidi ya kuweza kufanya hivyo ni mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ikiwa watu 313 waliweza kufanya hivi basi na sisi tunaweza kufanya. Mmoja wa makamanda wa Palestina alisema akiwa anataja jina la Pakistan kwamba ebu vuka mipaka yenu na muelekeo huku Palestina. Wameliomba jeshi la Pakistan na mashirika kuchukua hatua kali.
Ijumaa ijayo ni siku ya Quds ambapo tunatakiwa kujiandaa tangia sasa. Tunapaswa kufanya mambo ya maamuzi magumu siku hii ya Quds. UNSC walitangaza kusitishwa vita lakini Amerika hakupiga kura. Israel halikubali hili. Siku ya Quds ni ya waumini ambao wataonyesha na kuitangaza nguvu yao ya utashi siku hii. Mazingira inabidi yaandaliwe nchi nzima na sio tu ndani ya mitandao ya kijamii. Inabidi tuwape ujumbe ndugu zetu wa Palestina kwamba kama Allah alivyo watuma Malaika siku ya Badr, hivyo basi waumini wa Pakistan watakujieni kwa ajili ya kuwasaidia. Namna Israel wanavyodai ya kwamba tutaimaliza Hamas na Palestina na tutawapa nguvu waumini wa Pakistan ambao wataisambaratisha Israel. Inabidi tuchukue haki za Quds mwaka huu.
Popote ulipo unatakiwa kumuomba Jirani yako ahudhurie siku ya Quds. Watu hawafahamu na wewe ndiye unabidi uwafahamishe. Kama tutaandamana katika miji yote ya Pakistan, basi Allah atakubali nia zetu na hatua ya pili itakuwa ni kuandamana kuelekea Palestina. Waumini wote inabidi wabaki wakiwa wamejiandaa na kumuomba Allah hatima hii kwamba ima tunaopaswa kuyatoa maisha yetu au kutoa huduma zetu ambazo zitawaokoa Wapalestina.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *