Mamia ya wananchi wa Moroko walifanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hii wakiwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani vitendo vya Israel.
Gazeti la “Al-Arabi Al-Jadeed” limeripoti kuwa maandamano 100 ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina yamefanyika katika miji 52 ya Maghreb, na washiriki wa maandamano hayo walipiga nara dhidi ya Israel.
Kwa mujibu wa ripoti hii, mvua na upepo havikuweza kuzuia kuwepo waandamanaji hao, na wananchi wa Morocco wamelaani kuhalalisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel na kutaka kufungwa kwa ofisi ya uhusiano wa kidiplomasia ya Israel nchini humo.
Maandamano haya yalifanyika Maghreb huku maelfu ya raia wa Jordan wakikusanyika mbele ya ubalozi wa Israel mjini Amman kwa usiku wa sita mfululizo.
Waandamanaji wa Jordan, ambao walijaribu kushambulia ubalozi wa Israel mara kadhaa katika usiku uliopita, wanadai kusitisha uhusiano na Israel.
Gazeti la Israel la “Yediot Aharonot” hivi karibuni liliandika katika ripoti yake likiwanukuu maafisa waandamizi wa utawala huu kwamba Israel hivi sasa ina hali mbaya zaidi katika maoni ya umma wa walimwengu.
Jeshi la Israel limewauwa shahidi zaidi ya Wapalestina 32,400, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, wengi wa waliouawa shahidi ni wanawake na watoto.