Ofisi ya Habari ya Serikali ya Gaza ilitangaza kwamba idadi ya mashahidi wa waandishi wa habari imefikia 138 tangu Oktoba 7, 2023.
Kituo cha Habari cha Palestina kikinukuu Ofisi ya Habari ya Ghaza kimesema kuwa, idadi ya mashahidi waandishi wa habari huko Ghaza iliongezeka tena baada ya kuuawa shahidi Muhammad Abu Sakhil katika shambulio la Wazayuni dhidi ya hospitali ya al-Shafa huko Ghaza.
Wizara ya Afya ya Gaza ilitangaza kwamba baada ya wiki mbili za mashambulizi makubwa ya kijeshi kwenye hospitali hii na maeneo yanayoizunguka, hatimaye majeshi ya Israel yalirudi nyuma siku ya Jumatatu, na kuacha nyuma kiasi cha ajabu cha uharibifu na makumi ya mashahidi.
Katika taarifa ya wizara hii, imeelezwa kuwa maiti za makumi ya mashahidi zimetolewa kwenye vifusi vya hospitali hiyo na mazingira yake.
Tangu kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza tarehe 7 Oktoba, mchakato wa kuwashambulia waandishi wa habari wa Palestina umeshika kasi kwa ajili ya kuzuia kutangazwa ukweli na kupuuzwa.