kama maulama hawawezi kutoa fat’wa ya Jihad – watu wanayo fatuwa kutoka kwenye Qur’an na Mtume(s.a.w): Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(mkuu wa Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya Ijumaa – 5 April, 2024

Sermon 1: Dua ya Imam Sajjad (a) – ulinzi wa viungo katika mwezi huu
Sermon 2: kama maulama hawawezi kutoa fat’wa ya Jihad – watu wanayo fatuwa kutoka kwenye Qur’an na Mtume(s.a.w)
Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni moja ya fursa na mpangilio wa Allah ambao ameufanya kuwa ni mazoezi ya kuipata Taqwa ili mwanadamu aweze kuwa tayari kuishi mwaka mzima akiwa na Taqwa. Ni kawaida kwa wale wote ambao kazi yao ni ulinzi kufanya mazoezi, ili waweze kubakia wakiwa tayari kwa ajili ya kufanya ulinzi wa mipaka yao mwaka mzima kama vikosi vya kijeshi.

Imam Sajjad (a.s) katika dua yake ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani anaelezea nyanja nyingi na utambulisho wa Ramadhani kama shukurani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutupa taufiki hii. Ikiwa siri ya Ramadhani itaeleweka vizuri kwetu kama ilivyoelezewa ndani ya dua hii, basi kuipata Taqwa itakuwa rahisi kwa sababu masiku aya yamewekwa kwa ajili ya sisi kuipata Taqwa na sisi tuna utayari kwa ajili yake.

Imam Sajjad (a) anaendelea

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّد وَآلِهِ،
Ewe Mwenyezi Mungu, mbariki Muhammad na watu wa nyumbani kwake,

وَأَلْهِمْنَا مَعْرِفَةَ فَضْلِهِ وَإِجْلاَلَ حُرْمَتِهِ
Na tupe maarifa ya kujua ubora wake, na kutukuza utukufu wake,

وَالتَّحَفُّظَ مِمَّا حَظَرْتَ فِيهِ
Na kujilinda n uliyo yakataza
وَأَعِنَّـا عَلَى صِيَامِـهِ بِكَفِّ الْجَـوَارِحِ عَنْ مَعَاصِيْكَ،
Na utusaidie tuweze kuifunga kwa kuzuia viungo vyetu visikuasi,

وَاسْتِعْمَالِهَا فِيهِ بِمَا يُرْضِيْكَ
Na tuvitumie katika yanayo kupendeza ,

حَتَّى لاَ نُصْغِىَ بِأَسْمَاعِنَا إلَى لَغْو،
Mpaka tusiweze kusikiliza kwa masikio yetu upuuzi,
وَلا نُسْرِعَ بِأَبْصَارِنَا إلَى لَهْو،
Na usiyafanye macho yetu kukimbilia kutazama mamboya kipuuzi,

وَحَتَّى لاَ نَبْسُطَ أَيْدِيَنَا إلَى مَحْظُور،
Na hata tusinyooshe mikono yetu kwa yaliyo katazwa,
وَلاَ نَخْطُوَ بِأَقْدَامِنَا إلَى مَحْجُور،
Na tusipige hatua kwa miguu yetu kuelekea yaliyo katazwa,
وَحَتَّى لاَ تَعِيَ بُطُونُنَا إلاَّ مَا أَحْلَلْتَ،
Na matumbo yetu yasibebe isipokuwa uliyo halalisha
وَلا تَنْطِقَ أَلْسِنَتُنَا إلاَّ بِمَا مَثَّلْتَ
Na ndimi zetu zisitamke isipokuwa yale uliyo yatolea mifano,

وَلا نَتَكَلَّفَ إلاَّ ما يُدْنِي مِنْ ثَوَابِكَ،
Na hatufayi isipokuwa yale yenye kutusogeza karibu na thawabu zako

وَلاَ نَتَعَاطَى إلاّ الَّذِي يَقِيْ مِنْ عِقَابِكَ،
Na hatupeani isipokuwa yale yenye kutukinga na adhabu yako

ثُمَّ خَلِّصْ ذَلِكَ كُلَّهُ مِنْ رِئآءِ الْمُرَائِينَ وَسُمْعَةِ الْمُسْمِعِينَ،
Kisha yatakase hayo yote kutokana na kujionyesha kwa wenye kujionyesha na utajo kwa wenye kutaka utajo,

لاَ نَشْرَكُ فِيهِ أَحَداً دُونَكَ،
Hatukushirikishi na yeyote ndani yake

وَلا نَبْتَغِيْ فِيهِ مُرَاداً سِوَاكَ.
Na hatutafuti ndani yake lengo lolote isipokuwa wewe!
Imam (‘a) anaanza paragrafu hii kwa kitendo ambacho ni bora kukifanya wakati wowote, nacho ni kumsalia Mtume (s.a.w) na kizazi chake kitukufu. Ubora ambao umeupa mwezi wa Ramadhani. Imam (a) tafadali tufafanulie, na tuongoze kuwa ni8 namna gani mwezi huu unau bora kuliko miezi mingine. Kama ulivyo ufanye mwezi huu kuwa mtakatifu basi tupe fursa ya kutekeleza haki zake na kuheshimu utakatifu wake. Ewe Allah tupe ulinzi wa kujikinga na yale yote ambayo umetutaka tujikinge nayo.
Taqwa ni ulinzi. Anasema katika mwezi huu tunaomba utulinde na vitu ambavyo umetukataza kuvikurubia. Na tusaidie tuweze kuviweka viungo vyetu mbali na kukuasi na kutokuwa vitiifu kwako. Allah ametutaka tutafute usaidizi kutoka kwenye Sabr na Salaat. Lakini hatufanyi haya kwa sababu tunayazingatia kuwa ni mambo ya kupata thawabu za kiroho. Msaada wa kushirikiana unahitajika sana katika dunia hii. Siku zote huwa tunachukua msaada kutoka kwa watu hata kama mtu atasaidia basi atakusaidia kwa kukufedhehesha. Katika Dua Abu Hamza Al-Thumali, Imam Sajjad(a) anasema: kama hunisaidii, basi nitakuwa tegemezi kwa wengine na kwanza watanidhalilisha. Usinifanye niwe tegemezi kwa ambaye atanifedhehesha. Watu wana njia za kusaidia lakini wana ukosefu wa uwezo. Hivyo basi ikiwa hutaki kuwasaidia watu basi usikatae kwa kuwadhalilisha. Lakini Allah ameweka njia za kupata msaada kutoika kwake ambazo ni Sabr na Salaat pasina kuwa na udhalilishaji wowote. Hatujatazama mwelekeo wa sala ya namna hii. Tunasali tu kwa ajili ya kupata thawabu za kiroho hali ya kuwa Allah amefanya kila ibada ina faida za kidunia kama ilivyo na faida za kiroho ambapo msaada mkubwa huhitajika. Faida za nje ni rahisi na zipo kwa ajili ya kila mtu. Kwa mfano tunataka tusali sala ambayo kuna uwepo wa moyo wote ndani ya sala ambapo ndicho kilele cha Sala ambapo moyo hautavurugwa kwa muda. Lakini Sala huanza kwa uwepo wa kimwili, ambapo inamaanisha kwamba unatakiwa kuwepo kimwili wakati unaposali na kutimiza masharti yote ya sala, ukifanya hivyo utakuwa umepata nusu ya malengo ya Sala. Ikiwa mtu hawezi kufikia uwepo wa kiroho na akili yake ikawa inawaza mambo mengine, basi moyo wake hautabakia na uwepo, lakini pia hapaswi kuzingatia kwamba sala yake imepotezwa. Masharti ya uwepo wa kimwili ni kuwepo kuanzia katika vitangulizi vya sala kama kutawadha, kuvaa vizuri, kuwa na nidhamu na kusimama kwenye safu haya yote tunaweza kuyafanya. Hii ni nidhamu ambayo Allah anaitaka na Mwenyezi Mungu ameifanya Sala kuwa kama msaada wetu na yenye kutusaidia. Inatakiwa tuchukue msaada kutoka kwa msaidizi. Tunapanga mipango mikubwa lakini kisha tunaiacha kwa sababu hatuna usaidizi kutoka kwa watu. Watu huja baadaye Allah ndiye wa kwanza katika kutusaidia. Lakini sasa ni namna gani ya kuchukua msaada kutoka kwa Allah? Na kwa ajili hii Allah amemtengeneza msaidizi wako ambaye kila siku yupo na wewe kwa ajili ya kukusaidia. Hivyo- hivyo kufunga saumu na mwezi wa Ramadhani ni kama Sala tu. Tunahitaji ushirikiano na usaidizi kwa ajili ya kufanya mambo yanayo takiwa ndani ya Ramadhani kwa sababu sisi ni dhaifu. Imam ( a) anasema kwamba tunahitaji ushirikiano, msaada kutokana na Saumu zetu ili tuviweke viungo vyetu mbali na kutokutii . udhaifu wetu ni kwamba, viungo vyetu ni dhaifu. Tuna ulimi lakini hatuwezi kuudhibiti. Unahitaji ushirikiano wako na usaidizi ili kuudhibiti, zuia viungo vyangu na kutenda maasi. N9inatakiwa kufumba macho yangu na kuzuia ulimi wangu pale inapo takiwa kufanya hivyo. Mwanadamu anaweza kufanya mambo makubwa lakini hawezi kudhibiti viungo vyake. Umepewa viungo hivi ili uvitumie kwa ajili ya furaha yako. Unatakiwa kutumia macho yako, ulimi wako, mikono yako na miguu yako sehemu ambapo kuna furaha yako, lakini haitokei hivyo. Miguu yako inabidi itembee kuelekea mahala anapotajwa Allah. Lakini haiendi? Ima Sajjad akatika ua Abu Hamza al-Thumali anawasilisha tatizo hili kwamba viungo vyangu vipo tayari kwa ajili ya kila kitu isipokuwa kuja katika uwepo wako. Je ni kwa sababu umenitenga na watu wema wenye dara na vipenzi vyako? Macho yangu yanakuwa yapo wazi wakati wa kutazama TV, Simu ya mkononi lakini pindi ninapofungua macho yangu kwa ajili ya kusoma Qur’an au mwongozo, ninahisi kizunguzungu. Je hii ni kwa sababu Ewe Mola wangu hutaki nije katika uwepo wako. Ikiwa hii ni adhabu basi ninaomba msamaha wa kusamehewa viungo vyangu vinatakiwa kuacha pindi ninapotaka kuja karibu nawe pindi ninapotia nia.

Kisha Imam Sajjad(a) anasema : hatupaswi kusikiliza hata neno moja la kipuuzi ambalo hali maana. Sio maneno machafu lakini ni maneno yale ambayo hayana malengo ndani yake kama kufanya utani na mizaha. Kisha ndani ya mwezi huu wa Ramadhani sitakiwi kuyakimbiza macho yangu katika kutazama upuuzi. Mikono yangu haitakiwi kugusa wala kushika kitu ambacho umekikataza na nahitaji msaada wako. Na vitu vyote ambavyo umeviharamisha havitakiwi kuingia matumboni mwetu, ina maana tunakuomba uyaweke matumbo yetu mbali na vyakula ambavyo umeviharamisha. Ndimi zetu hazitakiwi kuzungumzia mada na mambo ambayo umeyakataza. Na hatupaswi kuvumilia ugumu ambao hautupelekei kuwa karibu na thawabu zako. Watu huvumilia ugumu katika maisha ya dunia ili kuipata furaha. Ikiwa tutataka kuvumilia ugumu basi inatakiwa iwe kwa ajili ya kupata thawabu zako. Hatutakiwi kufanya biashara katika mambo ambayo yanatuleta karibu na urithi wako. Na hatua hizi zinatakiwa kuchukuliwa kwa msaada wako na linda matendo yangu haya na Riyaa ( kujionyesha). Pamoja na neno Riyaa kuna neno “summa” la kwanza ni Riyaa ambayo ina maana ya kujionyesha na la pi ni “Summa” ambalo lina maana ya kutia ugumu. Tunafanya baadhi ya matendo ili watu watuone na watusifie. Wengi hufanya kazi za kusaidia za ustawi wa jamii ili watu wawasifie. Hii ni Riyaa. Unatakiwa kufanya kila kitu uwezacho sio kwa nia ya kutaka watu wakusifie bali unatakiwa kufanya kwa ajili ya kutaka kupata radhi za Allah. Wale ambao wanataka umaarufu , hutangaza kila kitu ili watu waweze kuwajua. Ewe Allah ! tujaalie tuweze kuyafanya haya yote lakini yakiwa yamesafika na shiriki. Riyaa, kujionyesha, kutangazo kila unachokifanya ni Shiriki kwa sababu unacho tamani na kufurahia ni kusifiwa na watu. Sitakiwi kuweka nia katika kutenda isipokuwa kwa ajili yako wewe Allah. Inabidi uwe hatima yetu na malengo yetu. Ikiwa tutapitisha muda katikati basi hiyo itakuwa ni shiriki ndogo. Ikia utafanya mambo kwa ajili ya kuipata pepo, basi hapo Allah hayupo akilini mwako. Katika mwezi wa Ramadhani asili aya kiini cha uwepo wako ndio iwe lengo latu. Ikiwa tutampata Allah tutakuwa hatujapoteza chochote.

Hotuba ya 2
Saumu ni nyenzo muhimu ya kupata Taqwa kama ilivyo amrishwa katika mwezi huu. Ni njia yenye ufanisi mkubwa wa kumkuza mwanadamu. Sawm maana yake ni kuacha vitu vyote ambavyo vimekatazwa na Allah na unatakiwa kuviacha kwa nguvu yako ya utashi. Pindi unapokuwa umeacha kwa nguvu yako ya utashi na kuipa uimara kisha baada ya hapo unatakiwa kuwakataza wengine wasifanye ambavyo vimekatazwa na kuharamishwa Mwenyezi Mungu. Hii ndio sababu inayopelekea matokeo ya Sawm kuwa ni Taqwa na haijadiliwi ila kufunga tu ndio kupo. Katika mwezi huu wa Ramadhani tulionao Waislamu wamefanya mambo mengi ya kufanana katika hali ya mazoea lakini bado inaonekana kuachwa Taqwa kwa mujibu wa istilahi za Qur’an. Hakuna ufanisi na taathira ndani yake katika kundi lolote la watu na ushahidi ni Palestina. Kwa kipindi cha miaka 77 tunaona kinacho watokea Wapalestina, tunaona Waislamu wamebaki katika kupitia majaribu na dhiki. Leo hii wana mtihani mgumu ambapo wanatakwa kuchukua maamuzi. Watu wa itikadi kali wamepanda juu ndani ya mwaka huu na hasa ndani ya mwezi huu. Wazayuni wanashambulia makanisa na kuwaua mapadiri ambao wanawachukua wakimbizi. Papa alitangaza ya kuwa kuna dhuluma inaendelea huko Gaza lakini awali haukuwa anazingatia kuwa kuna dhuluma huko. Watoa huduma na misaada wameuliwa na hawa watu saba walioibuliwa walikuwa Wamarekani pia. U.A.E wameionya Israel ya kwamba watakata mahusiano nanyi kwa kuwaua wafanyakazi wanaotoa msaada saba lakini hawakufanya harakati yeyote kwa maelfu ya Wapalestina waliouliwa. Biden alimuita Netanyahu na kumwambia kwamba Amerika inaweza kubadilisha sera yake na wewe kwa kuwaua wafanyakazi wa kutoa misaada saba. Seneta wa Amerika waliwahi kusema kwamba waue wote kwa bomu la nyukilia.
Waislamu wapo wanatazama kama watazamaji kwa miaka 77 na viongozi wote na Serikali wamekua wakishirikiana na Wazayuni. Uingereza ilifanya kosa la jinai kwa kutoa ardhi ya Wapalestina na kuwapa Wazayuni. Kila kosa kubwa ka jinai duniani limeanzishwa na Uingereza na kumaliziwa na kukamilishwa na Amerika ni kama mwana haramu wa Uingereza. Waarabu waliwaunga mkono Waisraeli kwa kuwaua Wazayuni. Kwa muda fulani kwa sababu ya uarbu, Jamal Abdul Nasir alitengeneza mazingira lakini walipoteseka na kupoteza baadhii ya mambo walirudi nyuma. Kama utajaribu kuona mchango wa wasomi , kwa hakika imekuwa ikikatisha tamaa. Nafasi yao na mchango wao ni kama ilivyokuwa katika wakate wa Karbala. Ilikuwa ni ukatili mkubwa na ulimwengu wa Kiislamu ulibaki kimya kunako hilo. Hawakufanya lolote wakate huo na hawakuomboleza a la kufika Karbala. Imam Sajjad(a) alikuwa ni Imam kwa miaka 35 akiwa ametengwa kabisa na hakuna aliyekuwa tayari kusimama na Ahlul Bayt (a). unyonge huu na fedheha vimejirudia katika ummah.
Leo hii shukurani zetu ni kwa Allah ambaye ametuonyesha njia ya heshima na umma wetu huu pia kwa kupitia Imam Khomeini (r.a). aliweza kutikisa dhamira za Umma wa Waislamu ambapo hii ni fedheha kwa kikundi cha Wazayuni. Simama na uwasaidie ndugu zako, na ikomboe Aqsa na Palestina. Kila siku ya ukatili kwa Palestina hiyo inakuwa ni siku ya aibu na fedheha kwa Waislamu. Huu ni uharibifu wa ulimwengu wa Kiislamu na maisha baada ya dunia ( Kiyama). Imamu wa ummah alituongoza juu ya hili na kuitangaza siku ya ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa ni siku ya Quds. Haikuwa tu kwamba alitangaza basi bali alifanya kila aina ya mipangilio. Aliifikisha ujumbe kwa maulama kwamba inabidi wauamshe ummah. Watawala wanaweza kuiuza Palestina lakini sio kupata uhuru. Waarabu na nchi ambazo ni wafuasi wao kama Pakistan wanaweza kuiuza Aqsa na sio kuitafutia uhuru. Haya yalikuwa ni maono ambayo Imam Khomeini alipewa (r.a) ambayo ikiwa utaitazama historia utapata mambo kama haya ni machache. Kuna mamilioni ya wasomi ndani ya Pakistan lakini mchango wao ni upi? Wapo wanahubiri umadhehebu, chuki na ugaidi. Lakini pia kutengeneza shakhsiya kwa kupitia dini na kisha kuvumilia dhuluma kwa Palestina ni fedheha.
Imam wa sala ya Ijumaa Qom, Dr. Araf ambaye ni shakhsiya maarufu alitoa barua kwa kila mtu ambayo ndani yake alisema kila mtu ambaye ana mamlaka ya kutoa fatwa na inabidi wafanye hivyo haraka. Amewataka maulama wote wa ndani ya Uislamuu hasa kwa aliyekuwa na uwezo wa kutoa fatwa inabidi watoe fatwa ya kukata mahusiano na Israel na kisha kuwekea vikwazo bidhaa za Israel ambacho ni chanzo kikubwa cha kiuchumi kinachotoka katika ulimwengu wa Kiislamu.
Je jambo hili litatuliwa kwa kuziwekea vikwazo bidhaa za Israel? Je hili litatua tatizo la Gaza? Kwanini usiwatake watoe fatuwa ambayo Qur’an inawataka , ambayo ni Jihad. Leo hii fatwa ya vikwazo havitakiwi kinacho takiwa ni fatwa ya Jihad. Jihad inabidi ifanywe kuwa ni wajibu kwa kila Muislamu hadi ifikie hatua hakuna Mzayuni hata mmoja. Umejifunza uwezo wa kutoa fatwa kupitia masomo uliosoma , lakini fatwa ya Jihad inatolewa kutokana na machungu ya Uislamu. Umesoma Uislamu kwa ajili ya mkate, khums na Zakat. Kama alivyosema Ali(a) kuhusu shakhsiya ya mtu wa dini kwamba aachwe kwa sababu amejifunza dini ili kufunika na kuficha uhalifu wake. Hili linatakiwa na wale ambao wanasubiri fatwa za maulama. Qur’an imeshatoa fatwa na ndio sababu pindi Qur’an inapokuuliza nini kimekutokea kwamba huwezi kusimama pindi unaposikia wanawake na Watoto wakipiga kelele wakitaka msaada na uokovu. Na fatwa ya Mtume (s.a.w) imekuja kwamba yeyote atakaye msikia mtu aliyedhulumiwa akiomba msaada na kama hatamsaidia basi io Muislamu. Kuna mambo mawili ambayo hufanyika kama dawa za kutuliza maumivu, jambo la kwanza ni kwa ajili ya kukusanya misaada kwa ajili ya Palestina la pili ni kuiwekea Israel vikwazo. Msikate mahusiano na Israel bali ikate Israel katika uwepo kabisa. Imam Khomeini (r.a) alisema ni kama kansa ambayo inabidi iondolewe na kuangamizwa. Huu ndio wajibu wa ulimwengu wa Kiislamu na wasomi. Fatwa hii ambayo haikutolewa matokeo yake yamekuwa ni majanga. Kama hamtaki kufanya hili na kisha mnatoa fatwa kama Qazi Shurayhi aliyehusika kutoa fatwa ya kuuliwa Imam Husein. Na nyinyi pia mnatoa fatwa kwamba Waislamu inabidi waungane na Wazayuni na kumuua kila Mpalestina. Haya ndio maisha ya udhalili ambayo Allah hataki. Allah anaweza kusimamisha udhalimu leo lakini hii ni sheria ya Allah. Kwanza mtu inabidi atazame madhalimu kwa umakini na aone ni kwa kiasi gani na pili ni kuwapima waumini ili kuona wana imani kiasi gani kivitendo. Je unaweza kuwa muumini kwa kufanya baadhi ya ibada ndogo. Imamu Khomeini alilikabidhi darasa hili mikononi mwa watu. Watu wengi wamelifanya hili. Siku ya Quds imekuwa ikifanyika kwa takriban miaka 45 hata ndani ya Pakistan. Ndani ya Lahore pindi nilipokuwa nikija kutoka Qom, niliona kuwa ilikuwa inakatisha tamaa sana, na wasomi walikuwa hawahudhurii. Nilikuwa nalazimika kuja ndani ya siku ya Quds ili niweze kuhudhuria. Siku moja nilienda kwenye msikiti ambao maandamano yalikuwa yanaanzia. Imam wa Ijumaa alikuwa anawaambia polisi na watu na waumini kuwa hao watu waliosimama nje hawahusiani na sisi. Nilikuwa nikitazama hili na watu ambao walikuja kusali Ijumaa walirudi majumbani mwao kwa njia mkabala na waandamanaji. Kisha tuliwafuata baadhi ya maulama wa Lahore na kuwaomba kuja kushiriki nasi katika maandamano. Kisha baada ya hapo baadhi ya maulama walikuja kama wawakilishi. Kisha Maulana aliyekuja alisema katika kipindi chote cha miaka thelathini sikuwahi kushiriki hii ndio mara yangu ya kwanza. Hii ndio imekuwa tabia yetu kwa Quds. Leo hii haipo kama hivyo; watu pamoja na wasomi wameamka hata kama watawala wamekata tamaa. Watu hawatakata tamaa. Wasomi na watawala watabaki wakiwa na aibu mbele ya Allah. Tunaomba kwamba waokolewe kutoka katika udhalili huu.
Lakini ikiwa wasomi na watawala hawafanyi hivi basi hutakiwi kuaibishwa. Hii ni dini ya Imam Husein (a) ya kwamba chochote atakacho mtawala kufanya wewe unatakiwa ubakie katika msingi wa Imam Husein (a). Ikiwa msomi ataungana na Banu Umayyah, bado wewe utatakiwa kubaki na Imam Husein (a). Hutakiwi kuangalia sheria na fatwa. Waziri wetu mkuu alizungumza na aliandika barua kwenda kwa Biden lakini hakumwambia chochote kwamba unafanya makosa ya jinai Gaza. Maslahi ya hawa viongozi yapo kwenye nafasi zao na sio kwa watu. Kama wanataka kumuua kila Mpalestina basi watu wanatakiwa kufyekelea mbali na kumaliza balozi zote za Amerika katika kila nchi. Amerika anafanya ushenzi kwa kutumia kura yake ya veto na kutoruhusu kusimamishwa kwa vita. Hii ni kwa sababu wanajua kwamba Waislamu walishakufa na leo inabidi muwathibitishie ya kwamba wale ambao wanadhani wamekufa wapo hai. Wana akili timamu zenye utambuzi na watatimiza ahadi yao. Leo ni siku ya Quds inabidi uache kazi zako zote za kila siku na baada ya sala ya Ijumaa inabidi ufanye wajibu wako na uwape ujumbe Amerika, Wazayuni na hawa viongozi dhalili. Inabidi tuwaambie Wapalestina kwamba sisi hatujafa, sisi ni Mahusein na tunasimama na hawa wanaodhulumiwa dhidi ya madhalimu, kwa sababu shule na kabila la Imam ni kwamba linatufundisha kumuunga mkono anaye dhulumiwa na kumkabili dhalimu na uharibifu wake. Leo hii Israel imepima nguvu ya kila mmoja na wameichukua vita kwa kiasi cha kushambulia ubalozi wa Iran pia ambapo ni sawa na kuishambulia nchi. Uongozi wa Iran utaamua nini cha kufanya katika kujibu shambulio. Lakini sisi hatutakiwi kufikiri kama viongozi, lakini tunatakiwa kutuma ujumbe kwa kiongozi wetu kwamba kama mtaruhusu sisi tutafika Gaza na vichanga vyetu.
Niliwahi kulitaja hili hapo kabla pia kwamba tunachokifanya hakina taathira na hakiwatii shinikizo Mzayuni. Taasisi zinapaswa kufanya mambo kwa namna ambayo zitaleta shinikizo kwa Israel. Israel inataka vita isambae nje ya Gaza ili waweze kupata ulinzi. Na sisi pia tunataka ienee ulimwengu mzima lakini sio kwa namna anavyotaka Israel. Inabidi ienee katika kila mtaa ambapo kuna makampuni ya Amerika na Israel. Haya ndio matakwa yetu kwa wasomi na maulama na kama watabaki nyuma basi wataua kila Muislamu. Itakuja zamu ya mji moja hadi mwingine na watu wengine watatazama. Waislamu wote na hasa Pakistan ambao wana hamasa ya hali ya juu sasa je ni kitu gani kimetokea kwenye hamasa zao., Aqsa na Gaza zinabomolewa na kuharibiwa na hamasa ya Wapakistani haipandi? Mmefanya umadhehebu kwa hamasa na huu ulikuwa ni uhalifu. Lakini Allah atapokea hamasa leo kwa ajili ya Gaza. Tokeni nje leo na mueleze shauku na hamasa zenu. Tutaanza mkutano wa hadhara na tubaki tukiwa na nidhamu hadi mwisho. Kuna jua linachoma lakini hakuna kuchoma kwa mabomu na moto wa Gaza. Kwa sasa inabidi tuchukue hatua mbili kwa ajili ya Gaza na kisha zitabadilika na kuwa hatua ambazo zitaleta ukombozi na uokovu kwa watu wa Gaza na Palestina. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awaangamize madhalimu.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *