Adhanom: Mwisho wa corona unakaribia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa dunia inakaribia mwisho wa mlipuko wa maambukizi ya Corona.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa kuhusu kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 duniani, hadi sasa watu milioni 615, laki 5 na elfu 3,802 wameambukizwa ugonjwa huo, na milioni 6 laki 5 na 23 elfu na 263 wamefariki dunia.

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulionya katika ripoti kwamba umri wa kuishi, elimu na kiwango cha ubora wa maisha duniani vimerudi nyuma miaka mitano kutokana na mlipuko wa Covid-19.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom, amesema: “Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona wiki iliyopita ndiyo ya chini zaidi tangu miaka miwili iliyopita.”

Adhanom ameongeza kuwa: Mstari wa kumalizika kwa corona unaonekana, lakini kama ilivyo katika mbio za marathoni, kuona mstari wa mwisho hakuna maana ya kuacha kukimbia na kusimama; bali inabidi tufanye juhudi zaidi kufikia mstari huo wa mwisho.”

La kusikitisha ni kuwa takwimu zinasema ni asilimia 21 tu ya watu katika nchi za kipato cha chini ndio waliopata chanjo ya corona.

Miongoni mwa mabara ya dunia, Afrika ina kiwango cha chini cha chanjo na asilimia 28 tu ya wakazi wake ndio waliopokea angalau dozi moja ya chanjo ya corona.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *