Kufuatia hali ya mvutano katika uhusiano wa Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, afisa mmoja wa Israel anasema kuwa, Ikulu ya White House inamalengo ya kuiangusha serikali ya Netanyahu.
Vyombo vya habari vya Israel, vikiwataja maafisa waandamizi wasiojulikana, vimedai kuwa serikali ya Rais wa Marekani Joe Biden inatafuta kuiangusha serikali ya Benjamin Netanyahu.
Akikosoa juhudi za utawala wa Biden, afisa huyu wa Israel anasema kuwa Israel si mlinzi wa Washington, bali ni taifa huru la kidemokrasia, na ni raia wa Israel wanaochagua serikali.
Afisa huyu wa Israel pia alisema kuwa Marekani inapaswa kutafuta kupindua Hamas badala ya kupindua serikali ya Netanyahu.
Kabla ya hapo afisa mmoja wa Kizayuni aliripoti mvutano kati ya Netanyahu na Biden na kusema kuwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ameamua kuanzisha makabiliano na Joe Biden, Rais wa Marekani.
Channel 12 ya Israel imemnukuu afisa mkuu wa Israel akisema kuwa Netanyahu ana hasira kutokana na ripoti ya kijasusi ya Marekani (CIA) inayoashiria uwezekano wa yeye kupoteza madaraka.
Aliongeza kuwa baada ya ripoti ya CIA, Netanyahu aliamua kuingia katika makabiliano makali na Biden.
Tathmini ya jumuiya ya kijasusi ya Marekani ilikuwa kwamba kutokuwa na imani na uwezo wa Netanyahu kutawala kulikuwa kukiongezeka miongoni mwa wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, na alitarajia maandamano makubwa ya kujiuzulu kwake.