Afisa Mzayuni: Ukweli ni kwamba, Hatuwezi kukabiliana na mashambulizi ya Hizbullah

Mkuu wa baraza la kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Margaliot ambaye hivi karibuni aliliomba jeshi la Israel liharibu miji ya mpakani ya Lebanon, amekiri kwamba, mashambulio ya harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ni makali mno kiasi kwamba hawawezi tena kuingia na kutoka kwa urahisi katika mji huo na kitu pekee wanachoweza kufanya ni kujificha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars; Eitan Davidi amesema hayo kufuatia mashambulizi makubwa ya maroketi ya Hizbullah dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye mipaka ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, na kuongeza kwa kusema: “Hali hapa si nzuri hata kidogo na hatuwezi kuingia na kutoka wakati wowote tunapotaka.”

Kanali ya 13 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni vilevile imemnukuu mkuu huyo wa kitongoji cha walowezi wa Kizayuni wa Margaliot akisema: “Hatuwezi kuendesha gari wakati wowote tunapotaka. Tunapokuwepo Margaliot huwa tunajificha kwenye mahandaki.”

Siku chache zilizopita, Eitan Davidi aliliombia jeshi la Israel liharibu makazi ya Walebanon ya Houla, Markaba na Meiss al-Jabal. Hata hivyo matamshi hayo ya Davidi yalidhihakiwa na kuonekana kituko kwenye mitandao ya kijamii kwani Davidi na Wazayuni wenzake wamekimbia nje ya kitongoji cha Margaliot, wakati wananchi wa Lebanon kwenye miji hiyo hawakutetereka na hadi hivi sasa wako majumbani mwao.

Mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii wa mji wa Houla wa Lebanon amejibu tishio la afisa huyo wa Kizayuni na kusema: “Ikiwa Davidi na wakaazi wa Margaliot wanaweza kukaribia mipaka ya Lebanon kwa nini wanaogopa hata kutoka kwenye nyumba zao. Sisi tupo hapa mpakani… yuko wapi sasa? Mbona hatumuoni yeye na Wazayuni wenzake?

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *