Afisa wa Afrika Kusini: Nchi za Magharibi hazipasi kuzungumza kuhusu ‘haki za binadamu’

Mohamed Faizal Dawjee, Mshauri wa Mawasiliano na Mkurugenzi wa Zamani wa Vyombo vya Habari wa serikali ya Afrika Kusini amelaani msimamo wa nchi za Magharibi kuhusu vita vya Israel dhidi ya Gaza, na kusema  nchi za Magharibi “zimeshiriki katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina.”

Dawjee amesema katika Jukwaa la Diplomasia huko Antalya nchini Uturuki kwamba na hapa ninamnukuu:” Kwa hakika tunaamini kuwa nchi za Magharibi hazistahili kuzungumza nasi na kutuhubiria kuhusu haki za binadamu, ukandamizaji na uhuru kwa sababu zimepoteza haki ya kufanya hivyo kutokana na hatua yao ya kuuunga mkono na kushiriki katika mauaji ya halaiki ya Wapalestina.”

Kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na nchi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ  kuhusu mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza; Mohamed Faizal Dawjee ametilia mkazo kuwa kuna umuhimu wa kuelewa kwamba sera ya kigeni ya Afrika Kusini inasisitiza juu ya haki za binadamu, uadilifu na uhuru.

Amesema, Afrika Kusini inataka kuona haki ikitendeka, uhuru ukirejeshwa na ukandamizaji ukikomeshwa huko Gaza na Palestina kwa ujumla. Amesema, kila wanachokishuhudia sasa huko Ukanda wa Gaza kinashabihiana na kile walichokipitia nchini mwao Afrika Kusini.

Kwa hakika, viongozi wetu wengi wa Afrika Kusini waliotembelea Palestina inayokaliwa kwa mabavu walisema kile walichokishuhudia huko Gaza ni kibaya mara 10 zaidi ya kile kilichotokea Afrika Kusini,” amesema Mohamed Faizal Dawjee Mshauri wa Mawasiliano na Mkurugenzi wa Zamani wa Vyombo vya Habari wa serikali ya Afrika Kusini.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *