Afisa wa Hamas: Ofisi yetu mjini Damascus itafunguliwa tena hivi karibuni

Mkuu wa ofisi ya mahusiano ya kimataifa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) alisema Jumapili kwamba ofisi ya harakati hii huko Damascus itafunguliwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sama la Palestina, Musa Abu Marzouq aliongeza: Hamas itafungua tena ofisi yake mjini Damascus na hivi karibuni itakuwa na mwakilishi.

Mkuu wa ofisi ya uhusiano wa kimataifa ya Hamas pia alisema: Tunawasiliana na mamlaka ya Iraq kwa ajili ya safari ya ujumbe wa harakati hiyo nchini humo, na tunatumai kuwa mawasiliano haya yatatimia katika siku za usoni.

Tarehe 24 Septemba mwaka jana, Hamas ilitangaza kurejea uhusiano wake na Damascus kwa kutangaza shukurani zake kwa uungaji mkono wa Syria kwa watu wa Palestina na kadhia yao.

Tarehe 27 Oktoba mwaka huo huo, ujumbe wa viongozi wa Hamas pamoja na viongozi wa makundi mengine ya muqawama wa Palestina walikutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Katika taarifa yake, Hamas imesisitiza mtazamo wake thabiti katika haja ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ulimwengu wa Kiarabu na nchi za Kiislamu na waungaji mkono wote wa kadhia ya Palestina na harakati zake katika mwelekeo wa kuanzisha na kuboresha uhusiano imara na Jamhuri ya Kiarabu ya Syria na kutangaza. kwamba kwa lengo la kutumikia kadhia ya Palestina inarejesha uhusiano wake na nchi ndugu ya Syria, hususan kwa kutilia maanani maendeleo ya haraka ya kieneo na kimataifa yanayoizunguka.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *